Na Latiffah Kigoda,TIC Dar Es Salaam.
Oktoba, 2019 kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu, Dar es Salaam, Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki amekutana na
Wawakilishi wa Wazalishaji na Wasindikaji Wakubwa wa Chai nchini ambapo pamoja
na mambo mengine amefanya nao majadiliano kuhusu mikakati ya kukuza Uwekezaji
katika sekta ndogo ya kilimo cha Chai hapa nchini.
Pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Uwekezaji Angellah Kairuki akisikiliza hoja za Wawekezaji wakubwa wa sekta ya Chai Tanzania.
(Picha na Latiffah Kigoda-Afisa Habari TIC)
Kikao hicho kilihudhuriwa na Wawakilishi kutoka katika Makampuni ya
Unilever Tea Tanzania Ltd (UTTL), Mohamed Enterprise Tanzania Ltd (MeTL),
Mufindi Tea and Coffee Tanzania Ltd (MTC), Wakulima Tea Tanzania Company
(WATCP), Rift Valley Tea Solution Ltd (under MTC) na kilihudhuriwa pia na
Wawakilishi kutoka Wizara ya Kilimo na Bodi ya Chai nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Uwekezaji Angellah Kairuki
(picha na Latiffah Kigoda-Afisa Habari TIC)
Waziri Kairuki alitumia
fursa ya kukutana na wawekezaji hao kusikiliza maoni na mapendekezo yao kuhusu
namna bora zaidi ya kukuza Uwekezaji katika sekta hiyo ndogo ili Chai ya
Tanzania iweze kuwa shindani katika soko la dunia. Nchi zote za Afrika za
Mashariki zinazalisha zao la Chai sambamba na Nchi za Ethiopia, Nigeria,
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Malawi, Afrika Kusini, Msumbiji na Zimbabwe
katika bara la Afrika ambapo Pakistani ndiyo soko kubwa zaidi la Chai Duniani.
Pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Uwekezaji Angellah Kairuki akisikiliza hoja za Wawekezaji wakubwa wa sekta ya Chai Tanzania.
(Picha na Latiffah Kigoda, Afisa Habari TIC)
0 Comments