Sekta ya kilimo ni muhimu
kwa uchumi wa Taifa letu, na ni muhimu kwa Mtanzania mmoja mmoja kutokana na kuwa
ni nguzo ya uhai wa viumbe kutokana na uzalishaji wa chakula ambacho kila mmoja
wetu hukitumia..yaani uwe Tajiri au Masikini utaitegemea tu sekta hii kwani
uhai wako ndipo ulipo.
Anaandika
Grace Semfuko.
Asilimia kubwa ya
Watanzania waishio vijijini hutegemea sekta hii kama shughuli kuu ya kiuchumi
na ndio maana shughuli nyingi za kilimo hufanywa huko Vijijini, inakadiriwa
kuwa zaidi ya robo tatu ya Watanzania wanajishughulisha na kilimo cha mazao
mbalimbali yakiwepo ya chakula pamoja nay ale ya kibiashara.
Kahawa ni mojawapo ya mazao makuu ya biashara nchini
Tanzania.
Kahawa ni zao muhimu la
kibiashara ambalo hulimwa katika Mikoa ya Kaskazini na Nyanda za Juu Kusini.
Mikoa inayolima Kahawa ni pamoja na Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Tanga,
Morogoro, Mbeya, Songwe, Iringa na Ruvuma katika Wilaya ya Mbinga, Kigoma,
Tarime na Bukoba.
Zao la Kahawa hulimwa
kama zao la kibiashara mbali na kuwapatia watu kipato kikubwa ambacho
huwasaidia katika kutatua changamoto mbalimbali za kiuchumi pia husaidia katika
kupambana na umasikini.
Taasisi ya Utafiti wa
Kahawa Tanzania (TaCRI) imekuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya Kahawa kuwa
yenye manufaa na endelevu, TaCRI
imetafiti na kuainisha teknolojia muafaka za kilimo cha kahawa ambapo
tayari imeshatoa aina 19 za kahawa aina ya Arabika na Robusta ambazo
hazishambuliwi na magonjwa ya Chulebuni (CBD) na kutu ya majani ambazo
zimesaidia kuongeza tija kwa mti.
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji
wa Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TaCRI) Dkt Deusdedit Kilambo anasema
taasisi hiyo imekuwa ikitoa mafunzo katika ngazi ya vyama vya msingi vya
ushirika (AMCOS) yanayohusu kilimo bora cha zao hilo ili kuinua zaidi kilimo
bora cha zao hilo ili kuinua zaidi kilimo cha kahawa.
Kwa mujibu wa Dkt
Kilambo Taasisi yake imejipanga kukidhi mahitaji ya miche ya kahawa kitaifa kwa
kushiriki katika uzalishaji wa miche milioni sita kwa mwaka kwa kushirikiana na
vyama vya msingi pamoja na wadau wengine.
Dkt Kilambo anasema
TaCRI imejipanga kuzalisha miche zaidi, kutoa mafunzo kwa Wakulima na maafisa
ugani ili kuendesha kilimo cha Kahawa kibiashara.
Anabainisha kuwa uwepo
wa maabara ya kisasa katika kituo chao ambayo hupima hali ya udongo imekuwa na
msaada mkubwa kwao kutokana na kufanya uchanganuzi wa udongo wa mimea na kutoa
ushauri unaofaa katika kuongeza tija ya zao la kahawa kwa wakulima.
Kwa upande wake Mtafiti
wa usambazaji wa teknolojia na mafunzo TaCRI Bi Sofia Malinga anasema mafunzo
hayo yanahusisha kufanya utafiti wa kuendeleza zao la kahawa kupitia mipango
mbalimbali ambapo tayari taasisi hiyo imetoa aina 19 bora za kahawa aina ya
Arabika na 4 aina ya Robustaambazo hazishambuliwi na magonjwa ya chulebuni (CBD)
na kutu ya majani.
“TaCRI imetoa aina hizo
mpya za kahawa ambazo ni mafanikio ya kipekee kwani zimekuwa ni mkombozi mkubwa
kwa mkulima na chimbuko kubwa la mapinduzi ya kijani kwani uwepo wa mbegu hizo
mpya umechangia katika kuongeza ubora wa kahawa ikiwa ni pamoja na kumuonngezea
mkulima kipato” anasema Maliga.
Anafafanua kuwa TaCRI
imetafiti na kupendekeza teknolojia muafaka za kuzalisha miche aina bota ya
chotara ambapo wanazalisha miche kwa njia ya chupa.
Akizungumza katika
ufunguzi wa maonesho ya 26 ya nanenane Kanda ya Kaskazini, Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro Dkt. Anna Mgwira anawataka maofisa ugani wa mikoa ya Kanda hiyo
kuacha utamaduni wa kuandaa maonesho kama nia ya kuwaridhisha viongozi na
Wananchi wanaotembelea maonesho hayo na badala yake waendane na uhalisia wa
bidhaa zinazozalishwa na Wakulima Vijijini.
Nae Mrajis wa Msaidizi
wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Kilimanjaro John Henjewele anasema moja kati ya
msisitizo wa Serikali ya awamu ya tano ni kuwataka Wakulima kuzalisha mazao
yenye tija ya kiuchumi ili kuondokana na umasikini.
“Mkakati wa Serikali ni
kuhakikisha mazao matano ya kimkakati ambayo ni Kahawa, Korosho, Tumbaku, Pamba
na Chai uzalishaji wake unaongezeka” alisema Henjewele alipotembelea banda la
TaCRI kwenye maonyesho ya Kilimo.
0 Comments