Ripoti ya Global Peace Index ya mwaka 2020 imeitaja Tanzania kushika nafasi ya kwanza kwa Amani na Utulivu kwenye nchi za Afrika Mashariki na nafasi ya sabakwa nchi zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara, kwa niaba ya Watanzania wote navipongeza vyombo vya ulinzi na usalama Rais Magufuli wakati akihutubia Bunge.
Mojawapo ya ahadi kubwa
niliyoitoa wakati nazindua Bunge ilikuwa Amani na utulivu wa nchi yetu, ninayo
furaha kulitaarifu bunge lako kwamba nimeitimiza ahadi hiyo kwa vitendo,
Muungano wetu umeendelea kuimarika, tumeweza kushughulikia changamoto za
muungano ikiwepo kufuta kodi mbalimbali.
Tumefanikiwa kulinda mapinduzi
matukufu ya Zanzibar, nchi yetu imeendelea kuwa kisiwa cha Amani na mipaka yake
imeendelea kuwa salama, tulipoingia madarakani kulikuwepo na wimbi la ujambazi
na mauaji ya kibiti, kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na jeshi la ulizni na
usalama, vitendo hivyo vilikomeshwa na sasa Tanzania iko salama.
TUENDELEE KUWEKEZA TANZANIA, HII NI KIELELEZO TOSHA KUWA WAWEKEZAJI KUWA SALAMA
0 Comments