Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimefanya wasilisho la kutangaza fursa za Uwekezaji kwa Wawekezaji Wamarekani wenye asili ya China katika Mkutano uliojumuisha Makampuni yapatayo 11 ya wawekezaji hao uliofanyika leo tarehe 27 Agosti, 2022 kwenye hoteli ya Serena jijini Dar-es-Salaam.
Akifungua mkutano huo Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda amewakaribisha wawekezaji hao na kuwahakikishia kuwa Tanzania ni mahali salama kwa kuwekeza na kuwajulisha kuwa serikali ipo tayari kuwasaidia wawekezaji kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwani kupitia TIC Serikali imeondoa urasimu na inatoa huduma za mahala pamoja kwa wawekezaji kwa kujumuisha Taasisi nyingine zinazotoa huduma kwa wawekezaji nchini.
Akiongea kwenye mkutano huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Ndg. John Mnali amesema wawekezaji hao wamefika hapa nchini kuangalia fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta ya Madini, Utalii, Viwanda vya dawa za
Binadamu, Ujenzi, Kilimo, Burudani na sekta ya huduma haswa zinazohusu Fedha.
Amesema TIC imejipanga kuwahudumia na kuwapatia taarifa muhimu ili waweze kufanya maamuzi sahihi ya kuwekeza hapa nchini kwenye sekta walizozichagua.
Aidha, Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya China hapa nchini bwana Jingfeng Zhu amesema Tanzania ina fursa nyingi za Uwekezaji na serikali ya Tanzania imefanya maboresho makubwa kwenye mazingira ya kufanya biashara. Nchi ina ardhi kubwa na ya kutosha kufanya Uwekezaji kwenye sekta mbalimbali.
#tunarahisishauwekezaji
#utaliikilimoburudanifedha
#milangoyauwekezajiikowazi
#kaziiendelee
0 Comments