Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

KIKAO CHA MKURUGENZI MTENDAJI NA WATUMISHI WA TIC MAKAO MAKUU

 9 Januari, 2019: Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Geoffrey Mwambe amefanya kikao na Watumishi wote (permanent na attached staff) wa TIC makao makuu ambao pia wamewakilisha Watumishi wengine katika ofisi za kanda na kuwatakia Heri ya Mwaka Mpya huku akiwataka wachape kazi zaidi katika kuwahudumia Wawekezaji.

Katika salaam hizo, Mwambe pia amewataka Watumishi wote wafanye kazi zao za kila siku kwa ubunifu ili kuboresha huduma kwa Wawekezaji. Na kipekee kabisa amewataka Watumishi wanaohudumia wawekezaji kupitia Mfumo wa Mfumo wa Mahala Pamoja ‘One Stop Facilitation Centre ’ wafanye kazi kwa maslahi mapana ya Taifa na sio kwa ajili ya Taasisi wanazoziwakilisha ili kupunguza changamoto za upatikanaji wa huduma kwa Wawekezaji.

Mwisho, Mkurugenzi Mtendaji ameendelea kuwasisitizia Wafanyakazi wote wafanye kazi kwa weledi na kuepuka vitendo vya rushwa. Hii ni kufuatia ukweli kwamba rushwa ni adui wa maendeleo na TIC kwa mujibu wa uhalisia wake na majukumu yake, utendaji wake pia unapimwa Kimataifa katika kutoa huduma kwa wawekezaji kuanzia hatua za usajili mpaka utekelezaji wa mradi wa uwekezaji.




Post a Comment

0 Comments