Baadhi ya wawekezaji kutoka Saudi Arabia wakifuatilia mkutano |
Ujumbe
wa wafanyabiashara na maafisa wa Serikali wapatao 15 kutoka Saudi Arabia
wamewasili nchini kwa lengo la kuangalia fursa za biashara na uwekezaji.
Wafanyabiashara waliowasili wanawakilisha makampuni yapatayo saba kwenye sekata
za ujenzi, nishati, viwanda, makazi, madawa na tehama. Wafanyabiashara hao
watakuwa nchini kwa muda wa siku mbili ili kupata taarifa za awali za biashara na
uwekezaji zitakazowashawishi kuwekeza nchini.
![]() |
Majina ya makampuni kutoka Saudi Arabia |
Ili
kuhakikisha kwamba wafanyabiashara hao wanapata taarifa za awali juu ya fursa
za biashara na uwekezaji zilizopo nchini sambamba na namna ambavyo watasaidiwa kuanzisha miradi yao hapa nchini Taasisi
ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) kwa
kushirikisha Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Ubalozi wa Saudi Arabia nchini wameandaa
mkutano wa biashara ‘business meeting’
tarehe 30 Januari, 2019 New Afrika Hotel. Siku ya pili wafanya biashara hao
wataendelea na mikitano ya ana kwa ana pamoja na kutembelea baadhi ya viwanda.
Afisa Uhamasishaji Uwekezaji wa TIC Bi. Diana Ladislaus akitoa mada ya mazingira na fursa za uwekezaji |
Mkutano
huo uliandaliwa katika sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza asubuhi ilihusisha wafanyabiashara
hao pamoja na taasisi za serikali na sekta binafsi za Tanzania kwa lengo la
kutoa mawasilisho na kuendesha mijadala mbalimbali fursa za biashara na
uwekezaji pamoja na taratibu za kuanzisha miradi nchini. Taasisi za Serikali na sekta binafsi
zilizoshiriki ni pamoja na TIC, BRELA, SIDO na TCCIA. Kituo cha Uwekezaji Tanzania
kilipata nafasi ya kutoa mada juu ya fursa na mazingira ya uwekezaji nchini na mada
iliwasilishwa na Bi. Diana Ladislaus, Afisa Uhamasishaji Uwekezaji.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji wa TIC Bw. John Mnali akizungumza na vyombo vya habari wakati wa mkutano wa kibiashara na wawekezaji kutoka Saudi Arabia. |
Sehemu ya
pili ya mkutano huo ilifanyika mchana ikihusisha mikutano ya ana kwa ana ‘B2B meetings’ kati ya wawakilishi wa makampuni
ya Kitanzania na Saudi Arabia kwa lengo la kujadili fursa za uwekezaji,
biashara na uanzishaji wa miradi ya pamoja/ubia.
![]() |
Sehemu ya wafanyabiashara wa Kitanzania wakijadilianana wafanyabiashara wa Saudi Arabia kuhusu fursa za biashara na uwekezaji |
Kituo
cha Uwekezaji Tanzania kimefurahishwa na ujio wa wafanyabiashara hao kwa matarajio
kwamba endapo watafikia maamuzi ya kuanzisha
miradi yao, nchi itanufaika kwa kuongeza pato la Taifa kupitia ajira
zitakazozalishwa, kodi itakayokusanywa, uzalishaji wa bidhaa nchini na kuvutia
tekinolojia mpya.
0 Comments