Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

Katibu Mkuu aridhishwa na kazi za TIC

Na Grace Semfuko TIC, Dar Es Salaam 
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu Bw. Tixon Tuyangine Nzunda ameridhishwa na kazi inayofanywa na Huduma za Mahala Pamoja zinazofanywa ndani ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)


Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu Bw. Tixon Tuyangine Nzunda akiagana na Viongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea huduma za mahala pamoja kituoni hapo.(Picha zote na Grace Semfuko)

Kituo hicho cha Uwekezaji Tanzania TIC kinatoa huduma za mahala pamoja ambazo zinajumuisha za Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)
Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Idara ya Uhamiaji, Wizara ya Ardhi, Shirika la Viwango Tanzania TBS, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira NEMC, Wakala wa Usalama na Afya mahala pa kazi OSHA, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Mamlaka ya Vitambulisho Vya Taifa (NIDA) 


Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu Bw. Tixon Tuyangine Nzunda akisikiliza maoni ya Wafanyakazi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) mara baada ya kutembelea huduma za mahala pamoja zinazofanywa ndani ya kituo hicho kilichopo ndani ya Ofisi za TIC Makao Makuu Barabara ya Shaban Robert Jijini Dar Es Salaam October 17,2019, kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa TIC Bw. Matthew Mnali.

Nzunda Oktoba 17 alifanya ziara ya kutembelea kituo hicho kilichopo ndani ya ofisi za Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu Bw. Tixon Tuyangine Nzunda akisikiliza baadhi ya Wafanyakazi wa Huduma za Mahala Pamoja zilizopo TIC Makao Makuu Barabara ya Shaban Robert Jijini Dar Es Salaam.

lengo la ziara hiyo ya Katibu Mkuu ni kujitambulisha kwa wafanyakazi wa TIC pamoja na kukagua kazi zinazofanywa na kituo hicho katika kufanikisha shughuli za uwekezaji Nchini.



Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu Bw. Tixon Tuyangine Nzunda akisikiliza baadhi ya Wafanyakazi wa Huduma za Mahala Pamoja zilizopo TIC Makao Makuu Barabara ya Shaban Robert Jijini Dar Es Salaam.




Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu Bw. Tixon Tuyangine Nzunda akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC mara baada ya kumaliza kutembelea na kukagua shughuli za uwekezaji zinazofanywa na Kituo hicho.

Post a Comment

0 Comments