Na Latiffah Kigoda TIC, Dar Es Salaam
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anaeshughulikia Uwekezaji Angellah Kairuki amesema ipo haja kwa wawekezaji
kutoka Nchini Misri kuwekeza Tanzania kwa kuwa kuna mazingira mazuri ya uwekezaji
pamoja na fursa mbalimbali kwenye sekta uwekezaji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anaeshughulikia Uwekezaji Angellah Kairuki akifanya mazungumzo na Balozi wa Misri Nchini Tanzania Bw.Mohammed Abulwafa, wengine ni Maafisa kutoka Wizarani pamoja na Maafisa kutoka katika Ubalozi huo
Kairuki amesema Ofisi yake na
Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha wawekezaji
wanapata nafasi ya kuwekeza katika sekta zote ikiwepo ya Viwanda, Kilimo,
Ujenzi, Mifugo, Dawa na Vifaa tiba na uongezaji wa thamani wa bidhaa
mbalimbali.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anaeshughulikia Uwekezaji Angellah Kairuki akisalimiana na Balozi wa Misri Nchini Tanzania Bw.Mohammed Abulwafa.
Waziri Kairuki aliyasema hayo
mapema leo alipofanya mazungumzo na Balozi wa Misri nchini Tanzania Bw.
Mohammed Abulwafa ambaye alimtembelea ofisini kwake akiambatana na Msimamizi wa
masuala ya biashara wa Ubalozi huo Bw.Mohemmed Meguid pamoja na Katibu wake
Bw.Ahmed Ghoul.
0 Comments