Na Latiffah Kigoda-TIC,Dar Es Salaam
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki leo
3 Oktoba,2019 ameonana na kufanya mazungumzo mafupi kwa nyakati tofauti na
Mabalozi wa nchi tatu leo katika Ofisi Ndogo za Wizara zilizopo, Dar as Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Angellah Kairuki akisalimiana na Balozi wa Denmark Nchini Tanzania Bi Mette Noergaard.
(Picha na Latiffah Kigoda-Afisa Habari TIC)
Mabalozi hao ni pamoja na Mhe. Shinichi Goto (Balozi wa Japan), Mhe.
Mette Noergaard, (Balozi wa Denmark) na Mhe. Jeroen Verhoeven (Balozi wa
Uholanzi) hapa nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Angellah Kairuki akisalimiana na Balozi wa Uholanzi Mhe.Jeroen Verhoeven.
(Picha na Latiffah Kigoda-Afisa Habari TIC)
Waziri Kairuki ametumia fursa ya kukutana na Mabalozi hao kuendelea
kuwakaribisha Wawekezaji kutoka katika nchi wanazowakilisha Mabalozi hao
hususani katika kipindi hiki ambacho Serikali ya Awamu ya Tano inafanya
jitihada za dhati katika kuboresha mazingira ya Uwekezaji na kufanya biashara
nchini.
Kwa upande wao Mabalozi hao walitumia fursa ya kukutana na Waziri huyo
wa Uwekezaji kueleza mikakati mbalimbali waliyojiwekea katika kuhakikisha
Wawekezaji wakubwa kutoka nchi zao wanachangamkia fursa mbalimbali za Uwekezaji
zilizopo Tanzania.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Angellah Kairuki akisalimiana na Balozi wa Japan Nchini Tanzania Bw.ShinichiGoto.
(Picha na Latiffah Kigoda-Afisa Habari TIC)
Balozi wa Denmark, Mhe. Mette kwa kipekee alipongeza jitihada
zinazofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) katika kusikiliza na kufanyia
kazi maoni ya wadau mbalimbali kunakolenga kuweka mazingira bora zaidi ya
Uwekezaji nchini Tanzania na kwamba wataendelea kuunga mkono jitihada hizo.
0 Comments