Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah J. Kairuki
amekutana leo na ujumbe kutoka Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na
Kilimo Tanzania (TCCIA) ulioongozwa na Bw. Koyi Rais mpya wa Chemba hiyo.Pamoja
na mambo mengine, kikao hicho kililenga kujadili masuala mbalimbali hususan
namna Chemba hiyo inavyoweza kuendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali
katika kukuza maslahi ya Sekta Binafsi nchini.
Katika kikao hicho Bw. Koyi alifafanua kwa Waziri Kairuki namna ambavyo
TCCIA inavyoratibu maslahi ya sekta binafsi nchini ambapo kwa sasa ni moja ya
vyama vinavyosimamia sekta binafsi vyenye mtandao mpana kote nchini. Aidha,
aliongeza kuwa kupitia mtandao huo wameweza kuwaunganisha wafanyabiasahara na
wawekezaji kuanzia ngazi ya Taifa, Mikoa hadi Wilaya. Vilevile, alibainisha
kuwakama sehemu ya kupanua huduma za Chemba hiyo
| |
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anaeshughulikia Uwekezaji Angellah Kairuki akisikiliza jambo kutoka kwa Mwenyekiti wa TCCIA chemba ya Mtwara Bw.Swallah Swallah
TCCIA sasa wamefungua matawi nje ya nchi kama vile Uingereza, Uturuki,
China na Urusihatuailiyopelekea kupanua wigo na kuwafikia kwa karibu zaidi
wadau wake wa nje ya nchi na hivyo kuwarahisishia utaratibu wa kufanya biashara
na kuwekeza nchini.
Aidha, Rais huyo wa TCCIA alimweleza Waziri Kairuki kuwa yeye baada ya
kuchaguliwa kuwa Rais wa Chemba hiyo alihamasika kuomba kukutana naye kwa
kutambua umuhimu wa kufanya kazi kwa karibu na Serikali, hususaniOfisi ya
Waziri Mkuu (Uwekezaji) katika kutetea maslahi ya sekta binafsi nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anaeshughulikia Uwekezaji Angellah Kairuki akisalimiana na Rais wa TCCIA Bw. Paul Koyi wakiwa katika picha ya pamoja ya viongozi wa TCCIA ofisini kwa Waziri.
Aidha, alitumia fursa hiyo kuipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kazi
kubwa iliyofanya ya kuandaa mikutano ya mashauriano kati ya Serikali na
wafanyabiashara na wawekezaji katika mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi ambapo
alitaarifu kuwa Chemba yake ilishiriki kikamilifu katika maandalizi yake na
kuwakilishwa na viongozi wa ngazi za mikoa kwenye Mikutano. Aliongeza kuwa
Mikutano hiyo imeamsha ari ya wafanyabiashara na wawekezaji kufanya shughuli
zao kwa kujiamini huku wakitambua kuwa sasa Serikali imekuwa sikivu kwa
kusikiliza changamoto zao na kuzitatua.
Vilevile aliahidi kuwa Chemba itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu kwa
Serikali hususani katika kipindi hiki ambapo kuna mchakato wa kufanya mapitio
ya sera na sheria mbalimbali zinazolenga kuboresha mazingira ya biashara na
uwekezaji hapa nchini.
Kwa upande wake,Waziri Kairukialimshukuru Bw. Koyi na wajumbe
alioambatana naokwa kutenga muda wao kuja kuonana naye na kujadili masuala
mbalimbali yanayohusu kukuza sekta binafsi nchini. Aliongeza Serikali inatambua
umuhimu wa sekta binafsi kama injini ya uchumi na ni wajibu wake kuhakikisha
inaweka mazingira wezeshi na rafiki ili kukuza wawekezaji waliopo na kuvutia
wengine wapya wa nje na ndani ya nchini. Pia,aliwashauri kuwaasa wanachama wao
kushiriki kimamilifu katika kutoa maoni yao katika michakato ya mapitio ya sera
ya sheria stahiki ili nchi ipate sheria itakayokidhi mahitaji kwa wakati huu na
wakati ujao.
0 Comments