Dar Es Salaam.
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi amesema Serikali
imeimarisha mazingira ya uwekezaji kwa kuondoa urasimu, rushwa na baadhi ya
tozo ili kuwarahisishia wawekezaji kufanya shughuli zao kwa urahisi Zaidi.
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo Novembe 6,2019 kuhusu mafanikio ya miaka minne ya Rais Magufuli akiwa madarakani, Rais alichaguliwa na Watanzania kuongoza nchi Oktoka 25 mwaka 2015 na kuapishwa Novemba 5 mwaka huo huo wa 2015.(Picha na Grace Semfuko)
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo Novembe 6,2019 kuhusu mafanikio ya miaka minne ya Rais Magufuli akiwa madarakani. (Picha na Grace Semfuko)
Amesema Serikali imeimarisha mifumo ya Sheria na Sera za
uwekezaji ambapo sasa mwekezaji atanufaika Zaidi kutokana na kuondoa kabisa mianya
ya rushwa iliyokuwa ikiwasumbua na kusababisha wakati mwingine uwekezaji
kukwama.
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo Novembe 6,2019 kuhusu mafanikio ya miaka minne ya Rais Magufuli akiwa madarakani. (Picha na Grace Semfuko)
“Tumejitahidi sana kuweka vivutio, nchi yetu ina Amani na
utulivu, na ukiwauliza wawekezaji wengi kama kuna maeneo yalikuwa yanawakwaza
ni urasimu na rushwa,na upatikanaji wa vitu kama ardhi, umeme na dawa, sasa
hivi hayo hayapo tena” alisema Dkt Abbasi
“Nchi hii kila mwekezaji makini anajua, pale TIC tumeweka
huduma zote kwenye ofisi moja, hakuna habari ya kutoka TRA uchukue tena Uba
uende OSHA,uchukue tax uende NIDA sasa hivi mwekezaji akija pale TIC anapata
huduma zote kwa hiyo ndio siri ya kuvutia wawekezaji wengi Tanzania” alisema Dkt
Abbasi.
Rais Magufuli alichaguliwa na Watanzania Octoba 25, 2015 na kuapishwa November 5 mwaka huo huo wa 2015, na sasa anatimiza miaka minne huku Watanzania wakishuhudia akiimarisha maeneo mbalimbali yakiwepo ya uwekezaji.
Mwisho.
0 Comments