Na Latiffah Kigoda- Dodoma.
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimepata fursa ya kutoa elimu ya uwekezaji kwa Waheshimiwa/Wajumbe
wa Kamati mbili za Bunge kupitia semina iliyoendeshwa 7Nov, Dodoma.
Kamati hizo ni Kamati ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma na Kamati ya Katiba na Sheria.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania Profesa Longinus Rutasitara (wa kwanza kulia)
akita na Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC Bw. Geoffrey Mwambe (wa pili) wakiandika
baadhi ya maswali ya Wabunge ili wheeze kuyajibu kwa ufasaha
Lengo la elimu hiyo ilikuwa ni kuwajengea Waheshimiwa Wabunge uelewa mpana wa masuala ya uwekezaji
ambapo walipata fursa ya kufahamu kiundani majukumu ya TIC, namna Kituo kinavyovutia uwekezaji kwa kuzingatia
Baadhi ya Wabunge walioshiriki katika Semina ya Uwekezaji iliyotolewa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania
TIC iliyofanyika Jijini Dodoma Novemba 7,2019 wakisikiliza mada ya uwekezaji iliyowasilishwa na
Mkurugenzi wa Kituo hicho Bw. Geoffrey Mwambe
hitaji la mwekezaji, sababu za kuwekeza Tanzania, vigezo vya mwekezaji kujisajili na TIC, vivutio vya uwekezaji na
namna ambavyo vinachangia kuvutia uwekezaji mpya, umuhimu wa uwepo wa dirisha la huduma za mahala pamoja
TIC kwa wawekezaji na namna linavyofanikisha uwekezaji, faida za uwekezaji, nafasi ya Tanzania katika masuala
ya uwekezaji, mgawanyo wa miradi ya uwekezaji kimkoa, namna ambavyo miundombinu mizuri inavyochangia
kuvutia uwekezaji, na namna ambavyo uharaka wa upatikanaji wa idhini(vibali,vyeti na leseni) mbalimbali za
kufanikisha uwekezaji zinavyovutia uwekezaji.
Vilevile Bw. Mwambe aliweka bayana namna ambavyo mataifa yote duniani yanavyoshindana katika kuvutia
uwekezaji, changamoto za uwekezaji na mapendekezo ya maboresho ya mazingira ya uwekezaji nchini ili kuvutia
uwekezaji zaidi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Uwekezaji Angellah Kairuki akiwasilisha mada katika
semina wa Wabunge iliyofanyika Jijini Dodoma Novemba 7, 2019, Semina hiyo iliandaliwa na Kituo cha
Uwekezaji Tanzania TIC.
Naye Mhe. Dkt. Chegeni (Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma) amezungumza kuwa,
kupitia semina wameweza kupata picha kubwa ya mwenendo na nafasi ya Tanzania kiuwekezaji duniani, Afrika na
Afrika Mashariki.
Amesema, tayari kuna mikakati na jitihada zinazochukuliwa na Serikali kuboresha mazingira ya uwekezaji lakini
tuongeze kasi ili kufanikisha uwekezaji zaidi. Semina imechangia kuwaobgezea elimu zaidi ya masuala ya uwekezaji
na kwamba watakuwa katika nafasi nzuri ya kuchangia pale hoja za masuala ya uwekezaji zitakapowasilishwa
Bungeni. Mhe. Chegeni amehimiza TIC iendelee kutoa elimu ya uwekezaji kwa wadau wote wakieleza TIC na
majukumu yake, faida za uwekezaji kwa nchi na faida za mwekezaji akijisajili na TIC katika kufanikisha uwekezaji
wake.
0 Comments