Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

KIOO kampuni yenye uwekezaji wa aina yake nchini

Na Grace Semfuko, Dar es Salaam.
Kiwanda cha kutengeneza chupa  maarufu kama Kioo Limited kimetembelewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji Angellah Kairuki ili kuangalia shughuli za uzalishaji zinazofanywa na kiwanda hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji Angellah Kairuki akikagua moja ya mtambo wa kutengenezea chupa wa kiwanda cha utengenezaji wa chupa cha Kioo limited kilichopo Chang'ombe Jijini Dar Es Salaam Desemba 16,2019 (Picha na Grace Semfuko)

Kiwanda hicho cha pekee nchini na Afrika  kimeanzishwa mwaka 1961 na kinazalisha vifungashio/ chupa za soda, konyagi, mvinyo. Chupa hizo huuzwa kwenye kampuni mbalimbali  nchini na nje ya nchi barani Afrika.


Moja ya mitambo ya kutengeneza chupa uliopo katika Kiwanda cha Kioo Limited kilichopo Chang'ombe Jijini Dar Es Salaam ambacho kilitembelewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji Angellah Kairuki Desemba 16,2019 (Picha na Grace Semfuko)

Akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda hicho Waziri Kairuki alisema uwekezaji huo kwa muda wote umekuwa na tija ya kiuchumi kwa Taifa na kuwataka wawekezaji hao kupanua uwekezaji wao kwenye miradi mingine nchini hususan kiwanda cha sukari, utalii na mengineyo.

“Kioo limited mnafanya kazi kubwa na nzuri, makampuni kama Pepsi, Cocacola na makampuni makubwa ya bia yanafanya kazi na nyie ambapo mnawazalishia  vifungashio (chupa) kwa ajili ya bidhaa zao. Nawaomba pia muwekeze kwenye maeneo mengine, tupo tayari kuwasaidia” alisema Kairuki.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji Angellah Kairuki akipata maelekezo kutoka kwa viongozi wa kiwanda cha uzalishaji wa chupa cha Kioo Limited kilichopo Jijini Dar Es Salaam, Kairuki alifanya ziara kwenye kiwanda hicho Desemba 19,2019 (Picha na Grace Semfuko)

Kampuni ya kioo imeirikia mwito wa Waziri kwa kuonesha nia ya kuwekeza kwenye kiwanda cha kuzalisha sukari inayotumika viwandani.

Kampuni ya Kioo kama mojawapo ya uwekezaji  imesajiliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC na inapata vivutio vya uwekezaji vya kodi na visivyo vya kikodi. Waziri ameielekeza kampuni hiyo kuwasilisha changamoto walizonazo kupitia TIC ikiwamo tatizo la vibali.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji Angellah Kairuki akipata maelekezo kutoka kwa viongozi wa kiwanda cha uzalishaji wa chupa cha Kioo Limited kilichopo Jijini Dar Es Salaam, Kairuki alifanya ziara kwenye kiwanda hicho Desemba 19,2019 (Picha na Grace Semfuko).


Post a Comment

0 Comments