Wawekezaji raia wa Misri wamewasili nchini kwa lengo la
kuangalia fursa za uwekezaji kwenye sekta mbalimbali na wameonesha nia ya
kuwekeza kwenye sekta ya viwanda vya
kubangua korosho na uzalishaji wa mbolea.
Wawekezaji Raia wa Misri wakipata ufafanuzi kwa Maafisa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo Nchini Tanzania, Wawekezaji hao wameonesha nia ya kuwekeza kwenye zao la Korosho na Sekta ya Mbolea.
Hayo yamebainishwa na wfanyabiashara/wawekezaji
wapatao kumi baada ya kutembelea Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na
kupokelewa na Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji Bw. John Mnali kwa niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Bw. Mathew Mnali (wa pili kutoka kushoto mwenye tai nyekundu) akizungumzia fursa za uwekezaji zilizopo nchini kwa Wawekezaji Raia wa Misri waliotembelea ofisi za TIC Desemba 11, 2019.
Katika majadiliano, wawekezaji hao wamepata fursa ya kupata
taarifa na takwimu za hali ya uchumi, sababu za kuwekeza Tanzania,vivutio vya
uwekezaji (vya kikodi na visivyo vya kikodi), usaidizi wa wawekezaji kupitia
Mfumo wa Mahala Pamoja,jitihada zinazochukuliwa na serikali kuboresha miundo
mbinu ya uwekezaji nchini na fursa zilizopo kwenye sekta/maeneo mbalimbali
ikiwemo; kilimo na uongezaji thamani mazao ya kilimo, uchimbaji na uongezji
thamani madini, uunganishwaji wa magari, utengenezaji wa madawa, ufugaji na uongezaji
thamani mazao ya mifugo, uvuvi na uongezaji thamani mazao ya uvuvi, utalii,
nishati na miundo mbinu.
Wawekezaji Raia wa Misri wakifuatilia Mada ya Uwekezaji iliyowasilishwa na Afisa Uhamasishaji uwekezaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC Bi. Diana Ladislaus Mwamanga, Mada ilihusu fursa za uwekezaji zilizopo Nchini Tanzania, Wawekezaji hao wameonesha nia ya kuwekeza kwenye zao la Korosho na Sekta ya Mbolea.
Wageni hao
wamefurahishwa na mapokezi waliyopata TIC na taarifa muhimu zenye ushawishi wa kuwafanya
waamue kuwekeza nchini. Wageni hao watakuwepo kwa muda wa siku tatu ambapo pia
watatumia nafasi hiyo kutembelea Taasisi/Mamlaka mbalimbali ili kujadili namna
ambavyo watafanikisha uwekezaji wao sambamba na kutembelea Mkoa wa Mtwara ili kujionea
fursa kwenye zao la korosho.
0 Comments