Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Uwekezaji Bi. Angellah Kairuki akiwasisitizia jambo washauri wa Kampuni ya Dalberg ambao wanafanya tafiti za kuibua fursa zenye mrengo wa uwekezaji kwenye mnyororo wa thamani katika Sekta mbalimbali. Picha na Latiffa Kigoda, Dar Es Salaam.
Dar es Salaam.
Washauri elekezi wa kampuni ya Dalberg inayofanya kazi zake katika nchi zaidi ya ishirini Afrika, wamefanya kikao na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji Angellah Kairuki jijini Dar es Salaam.
Kikao kimejikita kujadili namna ambavyo kampuni hiyo itakavyofanya kazi kwa kushirikisha Wizara katika kufanya utafiti na kuandaa taarifa za sekta mbalimbali (investment profiles) kwa ajili ya kuvutia uwekezaji nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Uwekezaji Bi. Angellah Kairuki akisikiliza jambo kutoka kwa mmoja wa washauri wa Kampuni ya Dalberg ambao wanafanya tafiti za kuibua fursa zenye mrengo wa uwekezaji kwenye mnyororo wa thamani katika Sekta mbalimbali. Picha na Latiffa Kigoda, Dar Es Salaam.
Mhe. Kairuki ameipongeza timu kwa hatua hiyo na kwamba Wizara na Taasisi yake, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) itawapa ushirikiano. Aidha Mhe. Kairuki amewahimiza wataalamu hao kuhakikisha kwamba tafiti na taarifa wanazoandaa zilenge kwenye sekta/maeneo ya kipaumbele na zinazoonekana kuwa na uhitaji kwa sasa. pamoja na maeneo mengine, maeneo hayo ni pamoja na eneo la Vifungashio, Kakao, Ngano, Viungo na Mbegu bora.
Hatua hiyo itafanikisha upatikanaji wa 'profiles' za mnyororo wa thamani katika sekta zitakazonadiwa kwa wawekezaji wazawa na wageni kwa lengo la kuvutia uwekezaji nchini.
0 Comments