Na Grace Semfuko.
Serikali ya awamu ya tano
tangu kuingia madarakani November 2015 imekuwa ikiboresha mazingira na kuvutia
uwekezaji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Agellah Kairuki alisema tangu kuingia madarakani kwa Rais Dkt John
Pombe Magufuli hakuna kodi yoyote ya biashara na uwekezaji iliyoongezwa huku
kodi zaidi ya 168 zikifutwa katika kipindi cha miaka miwili zikiwepo kodi 105
za kilimo.
Hatua hiyo inaonyesha ni kwa
jinsi gani Serikali imedhamiria kukuza uchumi wa nchi kupitia biashara na
uwekezaji.
Katika kuhakikisha uwekezaji
unakua kwa kasi Serikali ya Tanzania pia inashirikiana na sekta binafsi kukuza
sekta hiyo kwani wao ndio wenye mchango mkubwa kwenye uwekezaji wa sekta
mbalimbali.
WAZIRI MKUU wa Jamhuri
ya Tanzania Kassim Majaliwa mara kwa mara huwa anasema Serikali inaendelea
kushirikiana na sekta binafsi katika kuweka mazingira wezeshi ya kuvutia
uwekezaji na biashara nchini.
Mhe.
Kassim Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wizara yake ndio yenye jukumu kubwa la kusimamia
uwekezaji, Waziri Mkuu anasema anasema mpaka
sasa, hatua mbalimbali zimeendelea kuchukuliwa kwa lengo la kuweka mazingira
wezeshi ya uwekezaji na biashara nchini.
Majaliwa alifungua Kongamano
la uwekezaji Juni 27, 2019 Jijini Dodoma na alisema ”Miongoni mwa hatua hizo
ni uwepo wa usafiri wa uhakika na wa haraka wa abiria na mizigo kwa
kujenga reli ya kiwango cha kimataifa (Standard GaugeRailway).”
Mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR
unaendelea, mradi huu ni mojawapo ya vivutio vya uwekezaji nchini Tanzania
kwani utarahisisha usafirishaji.
kwa kuwa alikuwa Dodoma
alitaja baadhi ya vivutio vitakavyorahisisha shughuli za uwekezaji kuwa ni pamoja na usafirishaji ambapo uwanja
wa ndege wa Dodoma umeboreshwa na kuruhusu ndege kubwa na ndogo kutua usiku na
mchana.
”Mashirika ya ndege yanayotoa huduma
yameongezeka na maandalizi ya awali ya ujenzi wa uwanja wa kimataifa wa ndege
katika eneo la Msalato yanaendelea.”
Waziri Mkuu amesema mkoa wa Dodoma una
barabara za kuaminika za kiwango cha lami zinazoiunganisha na mikoa mingine
pamoja na nchi jirani.
Amesema Serikali ya Awamu ya Tano
imeendelea kuboresha huduma za afya na Dodoma kuna hospitali ya Benjamin Mkapa
yenye uwezo kama wa Muhimbili na Mloganzila.
Amesema ujenzi wa mradi wa kufua umeme katika Mto Rufiji ‘Stiegler’s Gorge’wenye uwezo wa kuzalisha MW 2,115, utaongeza upatikanaji wa nishati ya uhakika nchini.
Amesema ujenzi wa mradi wa kufua umeme katika Mto Rufiji ‘Stiegler’s Gorge’wenye uwezo wa kuzalisha MW 2,115, utaongeza upatikanaji wa nishati ya uhakika nchini.
“Mradi huo utaongeza upatikanaji wa umeme wa kutosha na wa uhakika kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya viwanda na uwekezaji nchini ikiwemo na katika mkoa wa Dodoma.
Mradi
wa kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (Stigler’s Gorge) uliopo katika bonde
la Mto Rufiji ni miongoni mwa miradi mikuwa ambayo Serikali ya awamu ya tano
unatekeleza, mradi huu utasaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika ambao utaimarisha
uwekezaji wa viwanda nchini Tanzania.
Waziri Mkuu alisema Serikali itaendelea
na utekelezaji wa mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (The
Blue Print).
Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
anaeshughulikia Uwekezaji Angellah Kairuki
alizungumza na Uwekezaji TV akasema nia ya Serikali ni kuendelea kuwa na
mazingira wezeshi yanayowavutia wawekezaji nchini katika kuendelea kuchangamkia
fursa zilizopo na kupokea maoni yao ili kutatua changamoto za kiuwekezaji.
“Serikali itaendelea kuweka
mkazo mkubwa wa maboresho katika maeneo mbalimbali yatakayo kuvutia wawekezaji
ikiwani pamoja na uboreshwaji wa sekta ya mawasilino, miundombiu ya barabara na
usafirishaji ili kuwa na mazingira mazuri ya wawekezaji kuja kuwekeza nchini,”alisema
Waziri Kairuki.
Aliongeza kuwa Serikali inaanza
kutekeleza Mpango Kazi wa Uboreshaji wa Mazingira ya Biashara na Uwekezaji
ambao tayari umefanyiwa maboresho na utekelezaji wake unatarajia kuanza mapema mwaka
huu wa fedha wa 2020/ 2021.
Aidha waziri aliahidi
kuendelea kusimamia maeneo muhimu ikiwemo ushiriki wa sekta binafsi katika
maeneo ya uwekezaji na kueleza maboresho haya yatatekeleza hasa katika
kuboresha mifumo na kuwa na maziringa mazuri yanayotabirika kwa wawekezaji.
“Kwa kutambua umuhimu wa
Sekta binafsi, tutaendelea kusimamia ushiriki wao kikamilifu ili kuleta tija
pasipo kubagua sekta hiyo na kuendelea kuwa na mifumo inayotabirika kwa ajili
ya wawekezaji.
Makala imeandikwa na Grace Semfuko, Dar Es Salaam.
0 Comments