Na Grace Semfuko
Bei za jumla na rejareja za mafuta ya petrol, dizeli na
mafuta yalliyopokelewa nchini kupitia Bandari ya Dar es Salaam zimepungua
ikilinganishwa natoleo lililopita la April 1 mwaka huu.
Taarifa kwa vyombo vya Habari iliyotolewa na Mamlaka ya
Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Jijini Dar es Salaam jana na
kusainiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Godfrey Chibulunje
ilieleza kuwa bei hizo zitaanza kutumika kuanzia leo Juni 6, 2020.
Kwa mujibu wa EWURA mabadiliko ya bei za mafuta katika soko
la ndani yanatokana na mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la Dunia na
gharama za usafirishaji (BPS Premium).
Taarifa hiyo ilieleza kuwa Mwezi Mei,2020 bei za rejareja za
petrol, dizeli na mafuta ya taa zimepungua kw ash.219 kwa lita (sawa na
asilimia 10.50), sh. 143 kwa lita (sawa na asilimia 1.17) na sh. 355 kwa lita (sawa na asilimia 18.47 mtawalia).
Ikilinganishwa na toleo la mwezi uliopita bei za jumla za petrol,
dizeli na mafuta ya taa zimepungua kwa sh 218.59 kwa lita (sawa na asilimia 7.63) na sh. 354 kwa lita (sawa na asilimia 19.69) mtawalia.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa bei za jumla za mafuta ya
petrolina dizeli katika mkoa wa Tanga zimebadilika ikilinganishwa na toleo
lililopita la April 1, 2020.
Kwa mwezi mei 2020 bei za rejareja za petrol na dizeli kwa
mikoa ya kaskazini (Tanga,Arusha, Kilimanjaro na Manyara) zimepungua kw ash.
463 kwa lita (sawa na asilimia 21.88) na sh. 377 kwa lita (sawa na asilimia 18.21) mtawalia.
Kwa kulinganisha na toleo la mwezi uliopita wa April, bei za
jumla za petroli na dizeli zimepungua kw ash. 461.82 kwa lita (sawa na asilimia
23.19) na shilingi 375.82 kwa lita (sawa na asilimia 19.33) mtawalia.
“Bei za mafuta ya taa kwa mikoa ya kaskazini zitaendelea
kuwa zile zilizochapishwa katika toleo la April 1, 2020 kwa sababu hakuna
shehena ya bidhaa hiyo iliyopokelewa nchini kupitia Babdari ya Tanga kwa mwezi
April, 2020” ilieleza taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo mwezi mei 2020, bei za jumla na
rejareja kwa mafuta ya dizeli katika mikoa ya kusini (Mtwara, Lindi na Ruvuma)
hazitabadilika ilikinganishwa na toleo lililopita la April 1, 2020 kutokana na
kutokuwepo kwa shehena ya dizeli iliyopokelewa kupitia bandari ya Mtwara.
Hata hivyo bei za mafuta ya petrol zimepungua ikilinganishwa
na toleo la mwezi uliopita.
Kwa mwezi Mei 2020 bei za jumla na rejareja za petrol zimepungua
kwa sh. 129 kwa lita (sawa na asilimia 5.67) na sh 128.14 kwa lita (sawa na
asilimia 5.99) mtawalia.
Kwa kuwa hakuna mafuta ya taa katika Babdari ya
Mtwarawamiliki wa vituo vya mafuta ya taa wa mikoa hiyo wanashauriwa kununua
mafuta hayo kutoka Dar Es Salaam na hivyo bei za rejareja za mafuta ya taa kwa
mikoa hiyo zinatokana na gharama za mafuta hayo kutokea Dae es Salaam na
kusafirishwa hadi mkoa husika.
EWURA imesisitiza kwamba bei kikomo za mafuta kwa eneo
husika zinapatikana pia kupitia simu za mkononi kwa mujibu wa sharia ya mafuta
ya mwaka 2015, bei za bidhaa za mafuta ya petrol zitaendelea kupangwa na soko
na EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za
bidhaa za mafuta.
0 Comments