Kampuni ya KEDA inayotengeneza Marumaru kupitia kiwanda
chake kilichopo katika Kitongoji cha Pingo, imemkabidhi box 200 za bidhaa hizo
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete.
Box hizo 200 zenye thamani ya shilingi milioni 9 zimetokana
na ombi la Mbunge huyo alipofanya ziara jimboni humo ambapo alijionea miradi
mbalimbali ikiwa kwenye hatua tofauti ambayo baadhi yake ina mahitaji ya vifaa
hivyo.
Akizungumza baada ya zoezi hilo, Ridhiwani alisema hatua
hiyo inakwenda kukamilisha miradi husika ambayo kwa asilimia kubwa inakaribia
kumalizika.
“Kwa niaba ya Wakazi wa Jimbo la Chalinze naomba nitoe
shukrani zangu za dhati kwa msaada huu ambao utaimarisha miradi yetu ya kijamii”
alisema Ridhiwani Kiwete Mbunge wa Chalinze.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Kiwanda hicho Hussein
Mramba alisema kwa kuona umuhimu wa kuimarisha miradi ya maendeleo ya kijamii
katika Jimbo hilo wameamua kutoa Marumaru hizo ili kuweka mazingira mazuri kwenye
miradi hiyo ambayo ni Kituo cha Afya na Shule mbalimbali.
0 Comments