Mwekezaji wa Gesi aina ya Oxygen na Nitrogen mkoani Tanga
Mohammed Noor ameishauri Serikali na Wamiliki wa Taasisi za Elimu nchini
kuwapeleka wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi kwenda kujifunza kwa vitendo
kiwandani kwake ili waweze kujiongezea ufahamu wa vitendo katika masomo yao.
Aliyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari
kiwandani hapo ana kuongeza kuwa kiwanda chake ni kipya lakini ipo haja ya
wanafunzo wa masomo ya sayansi kujifunza kwa vitendo.
“Upo umuhimu mkubwa wa Serikali pamoja na taasisi mbalimbali
za Elimu nchini hususan Wanafunzi kuanzia shule za Sekondari na Vyuoni kuleta
wanafunzi wao hapa ili wajifunze kwa vitendo, Mwanafunzi wa Sekondari Shuleni
anajifunza kwa nadharia kuhusu matumizi ya gesi mbalimbali lakini hapa atakuja
kujifunza kwa vitendo na atajionea namna inavyoandaliwa” alisema Bw. Noor.
Sambamba na hayo alisema endapo Wanafunzi wa masomo ya
sayansi watakwenda kiwandani hapo kujionea matumizi ya kisayansi yanayofanyika
katika eneo hilo watahamasika zaidi kulipenda somo hilo.
“ Wanafunzi wakijionea kwa matendo itasaidia sana kuongeza
ari ya kujisomea na hatomaye kuongeza wataalamu katika sekta ya gesi” alisema.
0 Comments