Leo Mei 20, ni siku ya nyuki
duniani.
Ni siku maalumu ya kutambua
mchango wa nyuki duniani kote, katika mazingira, kilimo, ufugaji na uzalishaji
wa asali.
Mbali na umuhimu wa asali kama chakula na dawa
katika mwili wa binadamu, nyuki kamwe hawaishii kutengeneza tu asali.
Katika mchakato wa kutengeneza asali, nyuki
hufanya kazi kubwa ya "Uchamvushaji" mashambani hivyo kuongeza
uzalishaji wa mazao kwa wingi mashambani.
Tanzania inaungana na
mataifa mengine katika kuadhimisha siku hii ya nyuki Duniani huku ikikadiriwa
kuwa kuna makundi milioni 9.2 ya nyuki wenye uwezo wa kuzalisha tani 138,000 za
asali na tani 9,200 za nta kwa mwaka.
Kwa mujibu wa Shirika la
Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) ya mwaka 2017uwezo wa kuzalisha
asali na nta kwa Tanzania unakadiriwa kuwa tani 138,000 na tani 9,200 mtawalia,
hata hivyo uzalishaji ni tani 30,393za asali na tani 1,843 za nta kwa mwaka
sawa na asilimia 22 kwa asali na asilimia 20 kwa nta kwa uwezo wan chi.aidha
inaelezwa kuwa Tanzania inazalishatani 9,380 za asali na tani 625.3 za nta
pekee kwa mwaka ambazo ni sawa na asilimia 7 tu ya rasilimali iliyopo.
Kutokana na upungufu huo wa
uzalishaji na uhitaji mkubwa wa mazao ya nyuki, Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania TFS umekuwa ukifanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha watanzania
wananufaika na fursa zilizopo kwenye sekta hiyo.
TFS inasaidia upatikanaji
wa masoko ya mazao ya nyuki ndani na nje ya Tanzania, kutoa elimu na mafunzo
mbalimbali ya ufugaji bora na wa kisasa wa nyuki, kutoa elimu kwa watanzania
walaji kuhusu umuhimu wa asali pamoja na kuanzisha maduka ya asali.
Katika mahojiano na Gazeti
la Mwananchi kuhusu maadhimisho ya siku ya nyuki Duniani mwaka huu wa 2020,
Kamishna mhifadhi wa Misitu wa TFS Profesa Dos Santos Silayo alieleza namna
ambavyo asali inachangia maendeleo ya nchi.
“TFS imeendelea kuimarisha
shughuli za ufugaji wa nyuki jambo linalosaidia uzalishaji kuongezeka kuanzia
mwaka 2015 hadi 2019, pia uzalishaji wa nta kwenye vituo vya uzalishaji vya
wakala umeongezeka kutoka kilo 4,071 hadi kufikia kilo 30,000 sa asali na nta
mtawalia” alisema Profesa Silayo.
Profesa Silayao anasema ili
kuendeleza ongezeko la uzalishaji wa mazao ya nyuki na kama sehemu ya
kuhamasisha uhifadhi na upandaji miti, Wakala umeandaa mkakati wa ufugaji wa
nyuki kibiashara ambao unalenga kuongeza ufanisi katika shughuli za ufugaji
nyuki katika vituo vyake.
Mkakati huo umewezesha wakala
huo kuongeza uwekezaji wa shughuli za nyuki ili kuongeza uzalishaji
. Sekta ya ufugaji wa nyuki
na uvunaji wa asali inahitaji uwekezaji kama ilivyo kwa sekta zingine hivyo
wadau wadau mbalimbali wanahitajika kuweka nguvu zao katika uwekezaji huu ambao
unaonyesha kuwa na tija ya kiuchumi kutokana na asali kuwa na soko kubwa la
kimataifa.
Mbali na kuwa na soko kubwa
la asali Duniani pia ufugaji wa nyuki unasaidia uhifadhi wa mazingira kutokana
na mizinga ya nyuki kutengwa kwenye misitu ambayo husaidia kuwepo kwa hali
nzuri ya hewa.
Faida nyingine ni
kuongezeka kwa pato kiuchumi hususan kwa wananchi hasa waishio vijijini ambao
ndio watunzaji wakuu wa mazingira, wakulina na wafugaji hawa wanaweza kuinua
mapato kwa njia ya ufugaji nyuki.
Pia katika baadhi ya maeneo
ufugaji wa nyuki unasaidia kupambana na uharibifu wa mazingira kwa kukata miti
hovyo, ujangili wa wanyama na uwindaji haramu ukataji miti kwa ajili ya mbao na
uchomaji makaa.
Kumekuwa na makampuni
mbalimbali binafsi ambayo yanajishughulisha na uzalishaji wa asali nchini,
lakini pia bado kuna fursa nyingi za uwekezaji kwenye sekta ya asali ili
kuongeza tija hasa kwa wakati huu ambao wananchi wengi wanatumia asali kama
kiburudisho, kiungo na dawa.
Anaandika Grace Semfuko, Dar Es Salaam.
0 Comments