Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

TBL,Vodacom zang'ara Kampuni kubwa Afrika


Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na Vodacom zimetajwa kuwa miongoni mwa Kampuni kubwa 250 Barani Afrika mwaka huu.
Tathmini iliyofanywa na kampuni ya Tom Minney ya Afrika Kusini na kutolewa Mei 16 inaonyesha kampuni hizo ndizo zinazoongoza kwa thamani kubwa nchini.
Ripoti hiyo iliyotolewa Mwezi Machi mwaka huu inaonyesha TBL inashika nafasi ya 75 hivyo kuongoza nchini wakati Vodacom ikiwa ya 98 ikishika nafasi ya pili kwa Tanzania na kuwa kampuni pekee zilizomo kati ya 100 za kwanza.

Hata hivyo kwenye nafasi ya 105 ipo kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) wakati nafasi ya 134 ni Benki ya NMB.

Orodha hiyo pia inajumuisha Kampuni ya Saruji ya Twiga (Tanzania Portland Cement) hivyo kufunga Pazia la Tanzania kwenye orodha hiyo ya kampuni 250.

Tathmini hiyo inayozingatia kampuni zilizoorodheshwa kwenye soko la hisa inaonyesha TBL ina thamani ya dola Bilioni 1.39 sawa na Sh. Trilioni 3.2 wakati Vodacom ikiwa na Dola Milioni  827 za Marekani sawa na Shilingi Trilioni 1.9 za kitanzania.

Thanai ya TCC ripoti hiyo inasema ni dola milioni 738 sawa na shilingi Trilioni 1.7 na Benki ya NMB dola milioni 508 sawa na wastani wa shilingi trilioni 1.2. Kampuni ya Twiga imethaminishwa kwa dola 170 milioni (Sh.390 Bilioni).

Afrika Mashariki ina kampuni 17 kwenye orodha hiyo mwaka huu zikiwa zimepungua kutoka 21 za mwaka jana hivyo jumla ya mtaji wake nao kushuka kutoka dola bilioni 26.3 mpaka kufikia dola bilioni 20.2

Kenya iliongoza kwa idadi kubwa ya kampuni 11 baada ya kupungua tatu mwaka huu zikiwa na jumla ya mtaji wa dola bilioni 16 kutoka dola bilioni 21 lakini safaricom ikiendelea kuongoza kwa mtaji wa dola bilioni 10. Uganda ikiendelea kubaki nazo mbili zilizokuwepo mwaka jana pia.

Ikiwa na Kampuni 100 zilizopungua kutoka 109, Afrika Kusini iliongoza orodha hiyo kwa idadi kubwa ikifuatiwa na Misri alafu Morocco kwenye nafasi ya tatu.

Afrika Kaskazini ilikuwa na Kampuni nyingi zaidi ya 83 kutoka 70 za mwaka jana. Tunisia 12 na Misri 41.

Afrika Magharibi ina kampuni 27 zenye jumla ya mtaji wa dola bilioni 36.5 za mwaka jana.

Orodha ya Kampuni hizo inapatikana kwenye link hii

https://africanbusinessmagazine.com/top-250-african-companies/africas-top-250-companies-in-2020/




Post a Comment

0 Comments