HOTUBA YA WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2020/2021
MAFANIKIO YA SEKTA YA VIWANDA NA BIASHARA KATIKA AWAMU YA TANO
Mheshimiwa Spika;
Ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini ni jukumu jumuisha na shirikishi linalohusisha sekta mbalimbali za uchumi ambazo zinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia azma ya ujenzi wa uchumi wa viwanda. Hivyo, sekta hizo hutekeleza mipango jumuishi katika kujenga uchumi wa viwanda kwa kutumia rasilimali za fedha za Bajeti ya Serikali kwa kujenga miundombinu ya msingi na wezeshi ikiwemo miundombinu ya barabara, maji, umeme na mawasiliano. Aidha, sekta za huduma huchangia katika kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na nguvukazi yenye afya, bora na ujuzi unaohitajika. Pia uwepo wa ulinzi na usalama wa mali na watu hutoa uhakika wa mazingira ya wananchi kujishughulisha katika uzalishaji wa mazao, bidhaa na huduma. Hivi, tunapoangalia mafanikio ya utekelezaji wa Bajeti ya Sekta ya Viwanda na Biashara na hususan katika ujenzi wa uchumi wa viwanda, hatuna budi kuangalia kwa ujumla na mapana yake namna Bajeti ya Serikali inavyogharamia mipango ya sekta nyingine ambazo zinajielekeza katika kuchangia utekelezaji wa azma ya ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Mheshimiwa Spika;
Kwa ujumla wake, Sekta ya Viwanda na Biashara imefanikiwa: Kuongeza uzalishaji wa bidhaa mbalimbali muhimu nchini ikiwemo sukari, mafuta ya kula, bidhaa za chuma, saruji na marumaru na hivyo kwa kiasi kikubwa kukidhi mahitaji ya ndani ya nchi; Kuvutia ujenzi wa viwanda vipya nchini na ufufuaji wa viwanda vilivyobinafsishwa; Kuongeza maeneo ya kufanyia kazi wajasiriamali na kuboreshwa kwa maeneo ya uwekezaji; Kuendelea kuimarika mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji kupitia utekelezaji wa BLUEPRINT; na Kuimarika kwa taasisi za utafiti na maendeleo ya teknolojia kwa kuboresha maabara zake na utoaji huduma. Pia, Sekta imefanikiwa Kuimarisha udhibiti wa bidhaa na huduma nchini; Kuongezeka uwezo na ujuzi wa rasilimali watu; Kuongezeka kwa uwekezaji na mapato katika viwanda; Kuendelea kujitosheleza katika baadhi ya bidhaa nchini ambazo zilikuwa zikiagizwa kwa wingi kutoka nje; Kuendelea kutoa elimu kwa wajasiriamali; Kuzalishwa kwa teknolojia mbalimbali za kuongeza thamani ya mazao hususan za kutumika vijijini zikiwemo za kusindika alizeti, nafaka, matunda; Kuanza kutoa leseni za biashara (Kundi A na B) kwa njia ya kielektroniki na Kutoa mikopo kwa wajasiriamali kupitia Mfuko wa NEDF na kuutunisha. Vilevile, imefanikiwa kuendelea kulinda viwanda na biashara za ndani; Kuimarisha masoko ya mipakani; Kukamilisha baadhi ya majadiliano na kuendeleza majadiliano ya kibiashara kati ya nchi na nchi, kikanda na kimataifa ili kupata na kutumia fursa za masoko hayo; Kuendelea kuunganisha wakulima na fursa za masoko; na Kuendelea kutoa taarifa za masoko ya mazao ya chakula, biashara na bidhaa mbalimbali. Aidha, taasisi za sekta zimeweza kutoa gawio lake Serikalini na pia kuchangia katika Bajeti ya Serikali.
3.1. Mafanikio katika Sekta ya Viwanda
Mheshimiwa Spika;
Mheshimiwa Spika;
Sekta ya Viwanda nchini ni miongoni mwa nguzo muhimu katika ukuaji wa uchumi wa nchi. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali iliweka nguvu kubwa katika kufanikisha utekelezaji wa Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda sambamba na utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2015/162020/21 na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi 2015 – 2020. Utekelezaji huo umehamasisha na kuchochea ujenzi wa uchumi wa viwanda ili kufikia malengo ya maendeleo ya muda mrefu kama yalivyoanishwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025. Ili kuhakikisha Sekta hiyo inachangia na kuleta tija katika uchumi wa Taifa, juhudi za makusudi zimeendelea kuchukuliwa katika uongezaji thamani wa malighafi za ndani hususan katika Sekta za Kilimo, Uvuvi, Mifugo, Maliasili na Madini. Hatua hizo zinasaidia kuchangia upatikanaji wa ajira; kuongeza uzalishaji na mauzo ya bidhaa ndani na nje ya nchi; na hivyo kuongeza upatikanaji wa fedha za kigeni katika uchumi.
Mheshimiwa Spika;
Katika kipindi hicho, msisitizo umewekwa katika ujenzi wa viwanda vipya na kuimarisha viwanda vilivyopo. Mafanikio yaliyopatikana kutokana na juhudi hizo ni pamoja na uendelezaji na uanzishwaji wa viwanda vya marumaru, saruji, chuma, vinywaji, na matunda, nyama, maziwa, nguo na mavazi, bidhaa za plastiki na ngozi. Kwa muhtasari, baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano ni kama ifuatavyo:-
Uongezaji Thamani wa Mazao
Mheshimiwa Spika;
Kutokana na uhamasishaji unaofanywa na Serikali, uongezaji thamani wa mazao ambayo malighafi zake zinazalishwa kwa wingi nchini umeendelea kuongezeka ambako kumechochewa na kuendelea kwa ujenzi wa viwanda nchini. Kwa mfano, viwanda 8 vya kusindika maziwa vyenye kusindika maziwa vimeongeza uwezo wake kutoka lita 167,620 kwa siku hadi kufikia lita 194,335 kwa siku. Vilevile, viwanda 17 vya nyama vilivyojengwa vimewezesha kuongeza usindikaji wa mazao ya mifugo ambapo zimewezesha Tanzania kuwa na jumla ya viwanda 145 vya usindikaji wa mazao ya mifugo. Viwanda hivyo vinajumuisha viwanda 33 vya nyama, viwanda 99 vya maziwa na viwanda 13 vya kusindika ngozi. Pia, Serikali imewezesha ujenzi wa viwanda vitatu vya kusindika matunda na mbogamboga. Viwanda hivyo ni Kiwanda cha Elven Agri, Sayona Fruits Limited na Dabaga. Aidha, Serikali imewezesha ujenzi wa viwanda vinne vya kusindika vyakula vya Dar Worth Company Limited kinachozalisha sembe, dona na unga wa lishe; Uniliver cha kusindika Chai; Murzah Wilmar Rice Millers cha kusindika Mpunga; na Mahashree Agroprocessing Tanzania Limited cha kufungasha mazao jamii ya kunde hususan mbaazi.
Ujenzi wa Viwanda Vipya
Mheshimiwa Spika;
Serikali inaendelea kuhamasisha uendelezaji na ujenzi wa viwanda nchini. Kutokana na jitihada hizo, jumla ya viwanda vipya 8,477 vimeanzishwa nchini kati ya mwaka 2015 hadi 2019. Viwanda hivyo vipya vinajumuisha viwanda 201 vikubwa, 460 vya kati, 3,406 vidogo; na 4,410 vidogo sana. Mfano wa viwanda katika Sekta ya Ujenzi ni Kilimanjaro Cement, Fujian Hexingwang Industry Co. Ltd na KEDA Ceramic ltd; Sekta ya Dawa na Vifaa Tiba ni Kairuki Pharmaceautical Industry na Zesta Pharmaceautical Industry); Sekta ya Chakula na Vinywaji ni 21st Century Food processing Industry na Sayona Fruits Ltd; na Sekta ya Vifaa vya Umeme ni Inhemeter Co. Ltd na Europe Inc. Industry.
Ajira katika Sekta ya Uzalishaji
Ajira katika Sekta ya Uzalishaji
Mheshimiwa Spika;
Ajira katika Sekta za Uzalishaji zimeongezeka kutoka ajira 254,786 mwaka 2015 hadi kufikia ajira 306,180 mwaka 2018, ikiwa ni ongezeko la asilimia 20.2. Ongezeko hilo lilitokana na ujenzi wa viwanda vipya na upanuzi wa viwanda vilivyopo ikiwemo; Kiwanda cha Goodwill Ceramic Ltd, KEDA (Twyford), Sayona Fruits Ltd (Chalinze), Sayona Drinks Ltd (Mwanza), Kiluwa Steel Ltd (Mlandizi), Fujian Hexing Wang Industry Co. Ltd (Mkuranga), Global Packaging Ltd (Kibaha), Europe Inc. Co. Ltd (Dar es Salaam), na Azam Fruits Processing Ltd (Mkuranga). Inatarajiwa kuwa, kwa mwenendo huo viwanda hivyo vitazalisha takribani ajira 370,478 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2020.
Kujitosheleza kwa Mahitaji ya Ndani kwa Baadhi ya Bidhaa za Viwandani
Mheshimiwa Spika;
Nchi imejitosheleza katika baadhi ya bidhaa muhimu zinazozalishwa nchini zikiwemo: saruji, marumaru, nondo, mabati na vifaa vya umeme. Matokeo hayo yamefikiwa kutokana na jitihada za Wizara za kuhamasisha wawekezaji kujenga viwanda vipya pamoja na upanuzi wa viwanda vya zamani. Kwa mfano, upanuzi wa viwanda vya saruji vya Tanga Cement Ltd na Mbeya Cement Ltd na kuanza kwa uzalishaji wa viwanda vipya kikiwemo Kiwanda cha Kilimanjaro Cement Ltd cha mjini Tanga kilichoanza kazi mwaka 2017 umewezesha kuongezeka kwa uwezo wa uzalishaji saruji (installed production capacity) hadi kufikia tani milioni 9.1 kwa mwaka 2019 ikilinganishwa na tani milioni 4.7 mwaka 2015. Uzalishaji halisi (actual production capacity) ni tani milioni 7.4 ambapo mahitaji halisi nchini ni tani milioni 4.8. Hii inamaanisha kuwa viwanda hivyo vinazalisha ziada ya tani milioni 2.6 ambazo huuzwa nje ya nchi zikiwemo Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia, DRC Congo na Msumbiji.
Mheshimiwa Spika;
Kutokana na jitihada za Serikali za kuhamasisha uwekezaji wa viwanda, ujenzi wa viwanda vikubwa viwili vya marumaru vya Goodwill (T) Ceramic Co. Ltd na KEDA (T) Ceramic Co. Ltd vimeanzishwa. Kiwanda cha Goodwill (T) Ceramic Co. Ltd kina uwezo uliosimikwa wa mita za mraba milioni 18 kwa sasa uzalishaji halisi ni mita za mraba Milioni 14.4, na Kiwanda cha KEDA uwezo wa uzalishaji ni mita za mraba 28.8 na uzalishaji halisi ni mita za mraba milioni 18.
23. Mheshimiwa Spika; Uzalishaji wa bidhaa za chuma umeendelea kutosheleza mahitaji ya ndani na umesaidia katika upatikanaji wa malighafi za ujenzi wa miundombinu wezeshi ya viwanda nchini. Viwanda vikubwa vitatu vya chuma vya Kiluwa Steel (chenye uwezo wa kuzalisha tani 12,000 kwa mwaka), Lodhia Steel Industry chenye uwezo wa kuzalisha tani 3,700 na Lake Steel and Allied Products Ltd ambavyo vimeongeza idadi ya viwanda vya chuma nchini na kufikia 25 ni kielelezo cha mafanikio. Kati ya hivyo, viwanda 16 vinazalisha nondo na vina uwezo uliosimikwa wa kuzalisha tani 1,082,700 kwa mwaka, wakati mahitaji ya nondo nchini kwa mwaka ni tani 295,000.
23. Mheshimiwa Spika; Uzalishaji wa bidhaa za chuma umeendelea kutosheleza mahitaji ya ndani na umesaidia katika upatikanaji wa malighafi za ujenzi wa miundombinu wezeshi ya viwanda nchini. Viwanda vikubwa vitatu vya chuma vya Kiluwa Steel (chenye uwezo wa kuzalisha tani 12,000 kwa mwaka), Lodhia Steel Industry chenye uwezo wa kuzalisha tani 3,700 na Lake Steel and Allied Products Ltd ambavyo vimeongeza idadi ya viwanda vya chuma nchini na kufikia 25 ni kielelezo cha mafanikio. Kati ya hivyo, viwanda 16 vinazalisha nondo na vina uwezo uliosimikwa wa kuzalisha tani 1,082,700 kwa mwaka, wakati mahitaji ya nondo nchini kwa mwaka ni tani 295,000.
Uendelezaji Maeneo Maalum ya Uwekezaji
Mheshimiwa Spika;
Wizara kupitia Mamlaka ya EPZ, imefanya tafiti tatu zenye dhana ya kufanya tathmini ya tija inayopatikana kutokana na kampuni zilizowekeza chini ya EPZA katika uchumi wa nchi. Matokeo ya tafiti hizo yameonesha uwepo wa tija katika uwekezaji wa maeneo ya SEZ. Kwa mfano, shughuli za uzalishaji zinazotokana na uwekezaji uliofanyika ndani ya BWM-SEZ zimewezesha kupatikana Dola za Marekani 127,641,683 kutokana na mauzo ya nje ya nchi; Matumizi ya wawekezaji ya Dola za Marekani 63,730,000 kwa malipo ya wafanyakazi wa ndani, malighafi, umeme, maji na gharama nyingine za kuendesha biashara; Kodi na Tozo mbalimbali zilizolipwa kupitia TRA za Dola za Marekani 7,497,100.34; na Ajira za moja kwa moja viwandani zipatazo 3,000. Tafiti na tathmini hizo zitaendelea kufanyika kwa nia ya kuboresha ufanisi wa Mamlaka na kukuza mchango wake kwa Taifa.
Mafanikio ya Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo
Kutoa Ajira kwa Watanzania Wengi
Mheshimiwa Spika;
Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo imetoa ajira kwa wingi kwa Watanzania ambapo kwa sasa imeajiri zaidi ya Watanzania milioni nane. Ajira hizo zimewezesha wahusika kujiongezea vipato na kutatua changamoto zao za kijamii na kiuchumi. Pia, imeweza kuongeza chachu katika azma ya ujenzi wa viwanda nchini ambapo takribani asilimia 99 ya viwanda vyote nchini vipo chini ya sekta hiyo. Hivyo, Sekta hiyo ni fungamanisho kubwa katika uchumi wa nchi kwa kuwa inahusisha sekta zote za uchumi. Vilevile, imebeba dhamana ya nchi ya kufikia uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda ifikapo 2025, hasa ikizingatiwa kuwa inashirikisha Watanzania wengi katika shughuli za kiuchumi. Aidha, Viwanda vingi vilivyoanzishwa vimekuwa na mchango mkubwa katika kuongeza thamani ya malighafi za Tanzania hususan zitokanazo na mazao ya kilimo.
Mitaji kwa Wajasiriamali Wadogo
Mheshimiwa Spika;
Kupitia Sekta hiyo, Wizara imefanikiwa kuchochea uanzishwaji wa shughuli za kiuchumi kwa kutumia mikopo inayotolewa na SIDO chini ya Mfuko wa Wafanyabiashara Wananchi (NEDF). Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2015 hadi Machi 2020, mtaji wa Mfuko wa NEDF umeongezeka kwa Shilingi Bilioni 2.22 kutoka Shilingi Bilioni 6.429 Machi 2016 hadi Bilioni 8.65. Ongezeko hilo limetokana na riba inayopatikana kutokana na fedha inayojizungusha (Revolving Fund) kupitia mikopo hiyo. Aidha, jumla ya wajasiriamali 17,654 wakiwemo wanawake 8,933 na wanaume 8,721 walipatiwa mikopo iliyowezesha jumla ya ajira 47,180 kupatikana.
Mheshimiwa Spika;
Mwezi Februari, 2020 yalisainiwa makubaliano kati ya SIDO, VETA, Azania Bank, NSSF na NEEC ya kuanzisha program ya kutoa mikopo kwa wajasiriamali waliohudumiwa na SIDO na wahitimu wa VETA kupitia Benki ya Azania. Makubaliano hayo yaliyofanyika chini ya uratibu wa Baraza la Uwezeshaji yanatoa nafasi kwa SIDO na VETA kuwapeleka wajasiriamali na wahitimu Benki ya Azania kuomba mikopo ya viwanda ya kuanzia Shilingi Milioni 8 hadi Milioni 500. Fedha zitakazokopeshwa kiasi cha Shilingi Bilioni 5 zimetolewa na NSSF kwa mkopeshaji ambaye ni Benki ya Azania. Program hiyo itaitwa SANVN kuwakilisha taasisi za SIDO, VETA, AZANIA BANK, NSSF na NEEC. Mwezi Aprili, 2020 vikao vya wataalam vilikamilisha Rasimu ya Mwongozo ya Utekelezaji wa Program (SANVN Viwanda Scheme – Lending Manual) na linasubiri uidhinishwe na kusambazwa ndipo utekelezaji wa program uanze.
Maeneo ya Shughuli za Uzalishaji kwa Wajasiriamali
Mheshimiwa Spika;
Serikali imefanikiwa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya wajasiriamali kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi. Suala hilo limewezesha ujenzi wa majengo ya viwanda (Industrial Shades) 12 katika Mitaa ya Viwanda ya SIDO iliyopo mikoa ya Dodoma (3), Manyara (3), Kagera (1), Mtwara (1) na Geita (4). Jumla ya viwanda 29 vimeweza kusimikwa katika majengo hayo ambapo ajira 648 zimezalishwa. Aidha, Serikali imefanikisha kusogeza karibu huduma za kusaidia na kuhamasisha wananchi kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa kujenga ofisi nne za SIDO katika mikoa mipya ya Simiyu, Katavi na Geita.
Mafanikio katika Sekta ya Biashara
Mafanikio katika Sekta ya Biashara
Mheshimiwa Spika;
Sekta ya Biashara ni nguzo muhimu katika kuwezesha upatikanaji wa fursa za biashara na masoko kwa bidhaa za Tanzania za kilimo na viwandani kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi. Biashara ni chanzo muhimu cha mapato ya Serikali na huwezesha kutawanya faida zinazopatikana kutokana na shughuli za uzalishaji. Hivyo, biashara hizo huchangia katika kuinua vipato vya wazalishaji na wafanyabiashara na kuchagiza uwekezaji kutoka ndani na nje ya nchi. Katika kipindi cha kuanzia 2015 hadi 2019, Serikali imeendelea na utekelezaji wa Sera na Mikakati ya biashara na masoko kwa kufanya mapitio ya Sera, Sheria na Taratibu mbalimbali ili ziendane na mahitaji ya Sekta kwa kipindi kilichopo na kijacho. Juhudi hizo ni pamoja na kuendelea kuimarisha mazingira ya ufanyaji biashara nchini, kuendelea kujenga miundombinu ya masoko; na kutafuta fursa nafuu za biashara kupitia majadiliano ya biashara baina ya nchi na nchi, kikanda na kimataifa.
Mheshimiwa Spika
Napenda kuchukua fursa hii kumshukuru na Kumpongeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Dkt. John Pombe Magufuli katika kipindi chake cha Uenyekiti wa SADC kwa kusimamia na kutetea lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha kuu za majadiliano. Kupitia jitihada zake, Mikutano ya SADC sasa inatumia lugha 4 za Kiingereza, Kireno, Kifaransa na Kiswahili. Kwetu sisi hiyo ni hatua kubwa na yenye manufaa kwa nchi katika Mtangamano huo wa Kikanda. Wizara itashirikiana na wadau wengi kuendelea kuuza Lugha ya Kiswahili kama bidhaa duniani kote.
Mauzo ya Bidhaa na Huduma katika Masoko ya Nje
Mheshimiwa Spika;
Katika kipindi cha miaka mitano, Sekta ya Biashara imefanikisha kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa na huduma kwenye masoko ya kikanda yanayotoa fursa za upendeleo maalum (preferential market access). Tanzania imekuwa na urari chanya wa mauzo ya bidhaa kwenda kwenye masoko ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC). Mfano, kwa upande wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka mwaka 2015 hadi mwaka 2018, Tanzania imekuwa na urari chanya wa mauzo ya bidhaa kwa wastani wa Dola za Marekani Milioni 288.04. Thamani ya bidhaa zilizoingizwa kutoka nchi za EAC ilishuka kutoka Dola za Marekani Milioni 322.80 mwaka 2015 hadi Dola za Marekani Milioni 302.93 mwaka 2018. Kukua kwa Sekta ya viwanda nchini kumesababisha kupungua kwa uingizwaji wa bidhaa kutoka EAC na SADC. Matokeo hayo, yametokana na Tanzania kujitosheleza na kuzalisha kwa ushindani bidhaa za saruji, marumaru, vyandarua, baadhi ya bidhaa za chuma kama vile nondo na mabati, mabomba ya plastiki, unga wa ngano na nafaka ikiwemo mahindi na mchele. Aidha, bidhaa zingine zilizouzwa zaidi katika Jumuiya hizo ni pamoja na chai, kahawa, sigara, madawa, vifaa tiba na madini ya Tanzanite.
Biashara katika Masoko ya Nje
Mheshimiwa Spika;
Sekta ya Biashara imefanikisha kuendelea kuimarisha mahusiano ya kibiashara na nchi za Umoja wa Ulaya na zile zilizo nje ya Umoja huo. Miongoni mwa nchi hizo ambazo Tanzania imeendelea kujiimarisha kibiashara ni pamoja na nchi za Uswisi, Denmark, Uingereza, Uholanzi, Sweden na Ujerumani. Kwa mfano, mauzo ya Tanzania nchini Uswisi yaliongezeka kutoka Dola za Marekani Milioni 153,933 mwaka 2015 hadi Dola za Marekani Milioni 257,166 mwaka 2018. Bidhaa zilizouzwa kwa wingi ni maua, mapambo, kahawa, chai, viungo, mafuta ya wanyama na mbegu, pamba na madini na vito vya thamani. Aidha, mauzo ya Tanzania yameendelea kuimarika kwenda kwenye nchi nyingine zinazotoa upendeleo maalum wa biashara ikiwemo India, China, Japan, Uturuki na Marekani. Mfano kuongezeka kwa mauzo kwenda nchini India kutoka Dola za Marekani Milioni 20,547 mwaka 2015 hadi Dola za Marekani Milioni 42,421 mwaka 2018. Bidhaa zilizouzwa zaidi ni kahawa, pamba, chai, tumbaku, samaki na bidhaa za baharini, nguo na mavazi, bidhaa za mikono (handcrafts), na ngozi na bidhaa za ngozi.
Mafanikio ya Sekta ya Masoko
Kuboresha Mazingira ya Biashara Nchini 33. Mheshimiwa Spika; Serikali imefanikiwa kuendelea na uboreshaji wa mazingira ya biashara nchini kwa kuandaa na kutekeleza Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara Nchini (Blueprint for Regulatory Reform to improve Business Environment). Mpango huo umewezesha maboresho ya tozo 173 ambapo kati ya tozo hizo, tozo 163 zimefutwa na tozo kero 10 zimepunguzwa kiwango. Kati ya tozo zilizofutwa, 114 ni za Sekta ya Kilimo na Mifugo, 5 za OSHA, 44 za TBS, GCLA,Utalii, Maji, Uvuvi na iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa-TFDA. Aidha, tozo zilizopunguzwa ni za Mamlaka za Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA). Mpango huo umewezesha kuhamisha jukumu la usimamizi wa masuala ya chakula kutoka iliyokuwa TFDA kwenda TBS, ili kuondoa muingiliano wa majukumu. Maboresho hayo yamesaidia kuondoa urasimu na kupunguza gharama za kufanya biashara. Baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kutokana na kufutwa kwa tozo ni pamoja na ongezeko la usajili wa usalama mahali pa kazi (workplace) 16,457 zilizosajiliwa kwa mwaka 2019 ikilinganishwa na mahala pa kazi 11,963 zilizosajiliwa kwa mwaka 2018. Aidha, Serikali inaendelea na maandalizi ya kutunga Sheria ya Uwezeshaji Biashara ya mwaka 2020 (Business Facilitation Act, 2020), ili kuipa nguvu ya kisheria misingi ya maboresho iliyobainishwa katika Blueprint. Rasimu ya Waraka wa Sheria hiyo imekwishawasilishwa kwenye ngazi za maamuzi Serikalini.
Kudhibiti Upotevu wa Mazao baada ya Mavuno
Mheshimiwa Spika;
Wizara kupitia Bodi ya Stakabadhi za Ghala imeendelea kuhamasisha Sekta Binafsi kujenga miundombinu ya masoko ikiwa ni pamoja na ujenzi wa ghala katika maeneo mbalimbali nchini. Katika mwaka 2019/2020, ghala zifuatazo zimejengwa na zinatumika kuhifadhi mazao ya kilimo yakiwemo korosho, ufuta, dengu, kakao, mbaazi na choroko. Ghala zilizojengwa zinapatikana katika Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi linalomilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma linalomilikiwa na Chama cha Ushirika cha Umoja Amcos Tunduru na Wilaya ya Kondoa Mkoa wa Dodoma linalomilikiwa na Chama cha Ushirika Pabu, Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara linalomilikiwa na Chama cha Ushirika Rivaku. Kutokana na hatua hizo, Serikali imefanikisha kupunguza upotevu wa mazao baada ya uzalishaji (post harvest loss), kuongeza uhai wa muda wa matumizi wa bidhaa za kilimo (shelf life) na kuweka mfumo wenye uwazi na rahisi kwa wanunuzi.
Mheshimiwa Spika;
Msimu wa mwaka 2019/2020, Wizara kupitia Bodi ya Stakabadhi za Ghala inayosimamia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala imesajili jumla ya ghala 51 zenye ujazo wa kati ya Mita za Ujazo 300 hadi 10,000. Jumla ya Kilo 240,218,696 zilihifadhiwa kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala katika Mikoa ya Ruvuma, Pwani, Lindi, Mtwara, Manyara, Mbeya, Shinyanga, Mwanza, Tabora, Songwe, Kilimanjaro na Dodoma (Kiambatisho Na. 3). Juhudi hizo zimesaidia kuongezeka mauzo ya bidhaa kutokana na kukamilika kwa Mfumo wa Mauzo ya Bidhaa kwa Njia ya Kielektroniki wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX). Jumla ya tani 519.89 zimeuzwa kupitia Mfumo huo. Kati ya hizo, tani 431.481 ziliuzwa Wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma wakati tani 88.41 ziliuzwa Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara. Aidha, Bodi inatarajia kuongeza mazao ya pamba, mahindi, choroko, kahawa, dengu na mbaazi katika Soko la Bidhaa Tanzania (TMX).
Kuimarisha Mifumo ya Uzalishaji na Masoko 36. Mheshimiwa Spika; Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali likiwemo Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), Bodi ya Kahawa, Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Vyama vya Ushirika imefanikisha kuweka mifumo madhubuti ya uzalishaji na upatikanaji wa masoko ya bidhaa za kilimo. Vyama vya Ushirika vilivyoshirikishwa ni pamoja na vyama vya Ushirika vya: Kagera (KCU); Karagwe (KDCU); na Ngara (NCU). Aidha, wadau hao wamesaidia kuongeza uwazi na ushindani wa soko ambao umeendelea kuimarisha bei za mazao na kuleta manufaa kwa wakulima.
Vituo vya Mipakani
Mheshimiwa Spika;
Tanzania imeendelea kutumia fursa yake ya kijiografia (strategic geographical location) kupanua wigo wa fursa za biashara na masoko kati ya Tanzania na nchi jirani. Katika kutekeleza jukumu hilo, Serikali imewezesha kuanzishwa kwa vituo 8. Vituo hivyo ni-: Holili/Taveta (Tanzania na Kenya); Sirari/Isebania (Tanzania na Kenya); Namanga/Namanga (Tanzania na Kenya); Kabanga/Kobero (Tanzania na Burundi); Rusumo/Rusumo (Tanzania na Rwanda); Mutukula/Mtukula (Tanzania na Uganda); Horohoro/Lungalunga (Tanzania na Kenya); na Kituo cha Tunduma/Nakonde (Tanzania na Zambia). Aidha, kituo kimoja kipya cha Kasumulo/Songwe (Tanzania na Malawi) kipo katika hatua ya ujenzi ambapo kikikamilika kitahudumia mpaka kati ya Tanzania na Malawi.
Mfumo wa Usajili wa Shughuli za Biashara kwa Njia ya Mtandao
Mheshimiwa Spika; Wizara imefanikisha kuongezeka kwa uanzishwaji na ufanyaji biashara nchini kutokana na kurahisishwa kwa taratibu za kusajili biashara nchini. Hatua ambazo Serikali imechukua ni kuboresha na kuimarisha matumizi ya Mfumo wa Usajili wa Majina ya Biashara, Makampuni, Alama za Biashara na Huduma, Hataza, Leseni za Viwanda na Leseni za Biashara kwa njia ya mtandao (Online Registration System-ORS) kupitia tovuti ya BRELA (www.brela.go.tz), na Dirisha la Taifa la Biashara (National Business Portal - NBP). Hadi kufikia Machi, 2020, Wakala imesajili Makampuni 7,549, Majina ya Biashara 12,627, Alama za Biashara na Huduma 1,970, Hataza 55, Leseni za Viwanda 200 na Leseni za Biashara 9,927.
Kuhuisha Soko la Biashara ya Zao la Tumbaku
Mheshimiwa Spika;
Wizara imefanikiwa kuhuisha soko la zao la Sekta ya Tumbaku baada ya Serikali kufikia muafaka na wanunuzi wakuu wa zao hilo kuhusiana na madai ya ukiukwaji wa taratibu za ushindani. Hadi sasa kampuni ya JTI Leaf Services Limited katika Mpango wake wa ununuzi imethibitisha kununua tumbaku yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 12.6 kwa mwaka 2019/2020, Dola za Marekani milioni 14.1 kwa mwaka 2020/2021, Dola za Marekani milioni 15 kwa mwaka 2021/2022 na Dola za Marekani milioni 15.5 kwa mwaka 2022/2023. Wizara kupitia Tume ya Ushindani (FCC) imeendelea kufanyia kazi jumla ya mashauri tisa (9) yanayohusu makubaliano yanayofifisha ushindani (5), miunganiko ya kampuni yaliyofanyika bila kutoa taarifa kwa Tume (2), makubaliano ya siri (1) na matumizi mabaya ya nguvu (abuse of dominance) (1). Katika mashauri yanahusu makubaliano yanayofifisha ushindani (AntiCompetitive Agreements) kutoka katika sekta ndogo ya Tumbaku, Tume imeendelea kufanya majadiliano na mmoja wa watuhumiwa aliyeomba kumalizika kwa shauri lake kwa njia ya suluhu (settlement proceeding). Aidha, Tume inaendelea kufanya uchambuzi wa utetezi wa kimaandishi wa watuhumiwa katika mashauri aliyobaki katika mashauri yanayohusu matumizi mabaya ya nguvu za soko (Abuse of Dominance) kutoka katika Sekta Ndogo za Kufukiza (fumigation) na Sekta ya Saruji, Tume imeandaa rasimu ya maamuzi ya awali (provisional findings) kwa shauri kutoka Sekta Ndogo ya Kufukiza. Tume inaendelea kufanya uchunguzi kwa shauri kutoka Sekta Ndogo ya Saruji.
UTEKELEZAJI WA BAJETI YA WIZARA KWA MWAKA 2019/2020 4.1. Bajeti Iliyoidhinishwa na Kupokelewa kwa Mwaka 2019/2020
Mheshimiwa Spika;
Kwa ujumla Sekta ya Viwanda ni Mtambuka ambapo utekelezaji wake hutegemea sekta nyingine za uzalishaji wa malighafi kama Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Pia, Sekta zinazosimamia upatikanaji wa miundombinu wezeshi kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda kama vile Sekta za: Ujenzi; Nishati; Maji; na Usafirishaji. Kutokana na umuhimu wa Sekta hizo katika kuendeleza na kukuza Sekta ya Viwanda Nchini, Serikali katika kipindi cha miaka mitano imewekeza rasilimali nyingi katika sekta hizo ikiwa ni jitihada za kuweka msingi bora wa kuendeleza Sekta ya Viwanda nchini.
Mheshimiwa Spika; Katika mwaka 2019/2020, Wizara (Fungu 44 & 60) iliidhinishiwa matumizi ya jumla ya Shilingi 100,384,738,648. Kati ya hizo, Shilingi 51,500,000,000 ni za Matumizi ya Maendeleo na Shilingi 48,884,738,648 za Matumizi ya Kawaida. Aidha, Wizara iliidhinishiwa kukusanya jumla ya Shilingi 14,300,000 (inayojumuisha Fungu 44 Shilingi 5,300,000 na Fungu 60 Shilingi 9,000,000) kutokana na uuzaji wa nyaraka za zabuni na marejesho ya mishahara endapo mtumishi ataacha kazi. Hadi kufikia tarehe 31 Machi, 2020, Wizara haikufanikiwa kukusanya kiasi chochote kutoka vyanzo hivyo. Pia, hadi kufikia mwezi Machi, 2020, Wizara ilipokea jumla ya Shilingi 33,812,276,737.40 ambazo ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Aidha, Wizara haikupata fedha kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. 4.2. Utekelezaji wa Malengo ya Bajeti kwa Mwaka 2019/2020 4.2.1. Sekta ya Viwanda i) Usajili wa Viwanda Vipya.
Mheshimiwa Spika;
Katika mwaka 2019/2020, jumla miradi mipya 303 imesajiliwa. Kati ya hiyo, miradi 95 ilisajiliwa chini ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), leseni za viwanda 177 (vikubwa 138 na vidogo 39) zilitolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) pamoja na viwanda 25 vilivyopewa leseni za muda vimepewa leseni za kudumu na miradi sita (6) ilisajiliwa chini ya Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Kuzalisha Bidhaa kwa Mauzo ya Nje (EPZA).
Ulinzi wa Viwanda vya Ndani
Mheshimiwa Spika;
Serikali imeendelea kuvilinda viwanda vya ndani kwa kuhakikisha vinapata malighafi ya kutosha kwa kutoza ushuru mkubwa, kuweka katazo kwa baadhi ya malighafi kwenda nje ya nchi na kutoa vibali maalum kwa baadhi ya bidhaa. Kwa mfano, Serikali imeweka:- Ushuru mkubwa kwenye malighafi ya ngozi, korosho, mafuta ghafi ya kula na mchuzi wa zabibu; Katazo kwa baadhi ya malighafi kwenda nje ya nchi kama vile chuma chakavu (steel scrap metal); na vibali maalum kwa maziwa ya mtindi, sukari na clinker. Lengo la jitihada hizo ni kuhamasisha uwekezaji kwenye Sekta ya Viwanda vinavyozalisha ajira nyingi katika mnyororo mzima wa thamani. Vilevile, Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (Tanzania Revenue Authority-TRA), na vyombo vya ulinzi na usalama vinahakikisha kuwa bidhaa zinazoingia nchini zinalipa ushuru stahiki ili kuwa na ushindani ulio wa haki sokoni. Hii ni pamoja na kuimarisha ulinzi wa mipaka yetu ili kuhakikisha kuwa hakuna bidhaa zinazopita njia za panya.
Mheshimiwa Spika;
Wizara kupitia Taasisi zake, imekuwa ikichukua hatua kadhaa katika kulinda viwanda na wafanyabiashara nchini. Kwanza, kuhakikisha kuwa bidhaa zinazoingizwa nchini zinakidhi viwango vya ubora. Bidhaa ambazo hazikidhi viwango hurudishwa au kuteketezwa kulingana na taratibu za kisheria. Pili, kulinda alama na nembo za bidhaa dhidi ya wafanyabiashara wadanganyifu wanaogushi au kutumia bila ridhaa ya mmiliki. FCC, kupitia Sheria ya Ushindani 2003, wanazuia mienendo na vitendo vinavyofifisha ushindani katika soko na hivyo, kuwapa wenye viwanda na Sekta Binafsi kwa ujumla imani ya kuwekeza na kufanya biashara zao bila kuathirika na wafanyabiashara wadanganyifu. Tatu, kutoza kodi kwenye bidhaa zinazoingizwa nchini katika kiwango cha asilimia 10 kwa bidhaa ghafi na asilimia 25 kwa bidhaa zilizo tayari kutumiwa na mlaji. Aidha, viwango hivi vinaweza kutozwa kwa asilimia zaidi ya 25 kulingana na umuhimu wa bidhaa husika.
Uendelezaji wa Viwanda Vilivyo binafsishwa
Mheshimiwa Spika; Katika kufuatilia viwanda vilivyobinafsishwa, Wizara kwa kushirikiana na Msajili wa Hazina imekuwa ikifuatilia utendaji kazi katika viwanda vilivyobinafsishwa ambapo kati ya viwanda 156 na Shirika moja vilivyofanyiwa tathmini, viwanda 88 vinafanya kazi na viwanda 68 havifanyi kazi. Kati ya viwanda 68 ambavyo havifanyi kazi, viwanda vitatu vimefanyiwa maboresho ili kuendelea na uzalishaji; viwanda 30 vinakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo; ukosefu wa mitaji ya uendeshaji; uchakavu wa mitambo na mashine; uchakavu wa majengo ya viwanda; uvamizi wa maeneo ya viwanda kutoka kwa jamii inayozunguka viwanda; na matumizi ya teknolojia zilizopitwa na wakati. Serikali inaendelea kuvifuatilia viwanda vilivyobinafsishwa ambavyo vilikuwa havifanyi kazi vizuri na vinahusu mazao ya kimkakati (mfano Kiwanda cha Chai Mponde)ili viweze kuzalisha kwa tija. Aidha, tararibu za kisheria za utwaaji rasmi wa viwanda ambavyo vimetelekezwa bila kuendelezwa kwa muda mrefu zinaendelelea ili viweze kutangazwa tena kwa ajili ya uwekezaji na kuendelea kuzalisha.
Uendelezaji wa Viwanda ambavyo Havikubinafsishwa
Mheshimiwa Spika;
Viwanda 7 ambavyo havikubinafsishwa kutokana na sababu mbalimbali vimeendelea kuwa mali ya umma chini ya Msajili wa Hazina. Aidha, kati ya viwanda vinne vilivyokabidhiwa kwa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, viwanda vitatu (3) katika mikoa ya Iringa, Arusha na Dodoma. Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina inaendelea kutafuta wawekezaji wapya wenye nia ya kuwekeza kwa maslahi mapana ya maendeleo ya nchi yetu.
Uendelezaji wa Viwanda Vinavyomilikiwa na Serikali
Kiwanda cha Viuadudu Kibaha
Mheshimiwa Spika;
Serikali inamiliki Kiwanda cha Viuadudu cha Kibaha kwa asilimia 100 kupitia Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC). Kiwanda hicho kina uwezo wa kutengeneza lita milioni 6 za dawa ya viuadudu aina ya Bactivec na Griselef kwa mwaka. Hadi sasa, Kiwanda kimetengeneza lita 677,000 za viuadudu kwa ajili ya kuua viluilui wa aina mbalimbali za mbu hususan wanaoeneza Malaria. Kiwanda hicho ni mahsusi kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za kupambana na ugonjwa wa Malaria nchini. Aidha, Kiwanda kimefanya mauzo ya dawa za viuadudu kwa soko la ndani na nje ambapo, Ofisi ya RaisTAMISEMI kupitia Halmashauri mbalimbali nchini zimekuwa zikinunua dawa kutoka kiwandani kwa nyakati tofauti. Vilevile, nchi za SADC mfano, Angola zimenunua lita 106,000. Hivyo, jumla ya mauzo ya ndani na nje ni takribani lita 500,000. Hata hivyo, Kiwanda kinaendelea na uzalishaji wa dawa kadri ya mahitaji yanavyojitokeza. Hivi karibuni kiwanda kimeingia mkataba wa kuuza Lita 45,785.67 za viuadudu nchini Kenya, zenye thamani ya Dola za Marekani 231,619.44. Sambamba na hilo, NDC kwa kushirikiana na wadau mbalimbali linaendelea kukisaidia Kiwanda kukamilisha taratibu za usajili wa dawa ya kibaiolojia kwa ajili ya kuua wadudu waharibifu kwenye zao la pamba ili kupanua wigo wa kibiashara.
Mradi wa Matrekta Aina ya URSUS
Mheshimiwa Spika;
NDC imeendelea kuunganisha matrekta aina ya URSUS na zana zake na ujenzi wa kiwanda kipya cha kuunganisha matrekta katika eneo la TAMCO Kibaha. Hadi kufikia Machi, 2020 jumla ya matrekta 822 yalikuwa yamepokelewa kutoka nchini Poland na kuunganishwa. Kati ya hayo, matrekta 724, majembe ya kulimia 511 na majembe ya kusawazisha 233 yalikuwa yameuzwa katika mikoa mbalimbali nchini. Hivi sasa, ujenzi wa jengo jipya la kiwanda umekamilika na kazi inayotarajiwa kufanyika ni ufungaji wa mitambo mara baada ya kutolewa bandarini.
Uendelezaji wa Maeneo Maalum ya Uwekezaji
Mheshimiwa Spika;
Wizara kupitia Mamlaka ya EPZ imeendelea kusimamia uendelezaji wa eneo la Kurasini Trade and Logistic Centre ambapo imefanikiwa kupata Hati Miliki ya eneo la Mradi mwezi Desemba, 2019. EPZA imepokea mahitaji (specifications) kutoka Bodi ya Chai (TBT), Bodi ya Kahawa (TCB), Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) kwa ajili ya uwekezaji ambao utakidhi uendeshaji wa shughuli za kuchakata, kufungasha na kuhifadhi mazao ya kilimo kwa ajili ya mauzo kwenda nchi za nje. Usimamizi wa uendelezaji wa Mradi utaendelea kufanyika kulingana na upatikanaji wa fedha.
Mheshimiwa Spika;
Mheshimiwa Spika;
Wizara kupitia Mamlaka ya EPZ imekua ikihamasisha ushiriki wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika uendelezaji wa Maeneo ya SEZ ili kuiwezesha Mikoa husika kutumia Maeneo ya SEZ kama chanzo cha mapato na mbinu mojawapo ya kuchochea shughuli za kiuchumi katika mikoa husika. Katika Mkakati huo, Mikoa imekua ikihamasishwa kushiriki katika kutenga, kumiliki na kuendeleza maeneo ya SEZ kupitia mafunzo ya uendelezaji wa Maeneo Maalum ya Kiuchumi yanayotolewa na EPZA. Hadi sasa, mafanikio yamepatikana katika mikoa ya Arusha, Geita, Mwanza, Kigoma na Songwe ambayo imekwisha pokea mafunzo na imetenga maeneo yatakayoendelezwa kama Maeneo Maalum ya Kiuchumi.
Mheshimiwa Spika;
Wizara kupitia Mamlaka ya EPZ imeendelea na juhudi za kusimamia maendeleo ya SEZ. Mara baada ya eneo kuwa limeendelezwa, shughuli kubwa ya usimamizi inahusisha jukumu la kuhamasisha uwekezaji katika maeneo ya SEZ ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje. Uhamasishaji huo umechochea na kuvutia uwekezaji na usajili wa leseni za uwekezaji ambapo katika kipindi cha mwaka 2019/2020 EPZA imesajili kampuni sita. Ongezeko hilo limewezesha jumla ya uwekezaji uliopo katika viwanda vilivyo chini ya EPZA kuongezeka kutoka viwanda 163 hadi viwanda 169 vikichangia ongezeko la mtaji unaokadiriwa kutoka Dola za Marekani Bilioni 2.353 hadi Dola za Marekani Bilioni 2.379. Mauzo ya nje yanakadiriwa kuongezeka kutoka Dola za Marekani Bilioni 2.247 hadi takriban Dola za Marekani Bilioni 2.266 na fursa za ajira za moja kwa moja kutoka 56,442 hadi 57,342.
Kutoa Huduma za Kitaalam Viwandani
Mheshimiwa Spika;
Wizara kupitia TIRDO imeendelea kuwa Mshauri Elekezi katika mradi wa ujenzi wa kiwanda kikubwa cha Karanga Leather Industries kilichopo Moshi cha kuzalisha bidhaa za ngozi kama vile; viatu, mikanda, soli za viatu, mikoba, mabegi na mipira ya ngozi pamoja na kuongeza thamani katika ngozi kwa ajili ya uuzwaji nje ya nchi. Kiwanda hicho cha ubia kati ya PSSSF na Jeshi la Magereza kitakuwa na uwezo wa kuzalisha jozi za viatu 2,800 kwa siku kwa mwaka wa kwanza hadi kufikia jozi 8,000 kwa siku baada ya miaka mitano. Katika awamu ya kwanza ujenzi wa Kiwanda umefikia asilimia 94. Pia, TIRDO imeendelea kuwa Mshauri Elekezi katika ujenzi wa kiwanda cha vifaa tiba kutokana na zao la pamba kitakachojengwa katika Mmkoa wa Simiyu kwa uwekezaji wa NHIF na WCF.
Mheshimiwa Spika;
Mheshimiwa Spika;
Wizara kupitia TIRDO imefanikiwa kuhakiki ubora wa sampuli za bidhaa mbalimbali za chakula na maji zipatazo 174 kutoka viwandani, wajasiriamali na kampuni mbalimbali hapa nchini. Viwanda hivyo ni pamoja na Masasi Food Industries, Kilimanjaro Natureripe, Darsh Company, Njombe Vegetable processing facility. Taasisi za kiserikali kama Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) pia wameweza kuhudumiwa na maabara hiyo. Vilevile, wazalishaji wa bidhaa za mifugo kama vile Kiliagro & Livestock Products na Rulenge Agricultural Products Co Ltd wameweza kuhakikiwa bidhaa zao za nyama ya kuku na nguruwe kwa ajili ya kupata uhakika wa ubora. Aidha, TIRDO imefanikiwa kutoa mafunzo ya uzalishaji chumvi yenye ubora unaokidhi viwango vya ubora vya nchi yetu na vya kimataifa kwa wazalishaji wa chumvi wa jumuiya ya uzalishaji na mashamba ya chumvi Wawi- Pemba.
Mheshimiwa Spika;
Wizara kupitia TIRDO, imefanikiwa kutoa huduma za ukaguzi wa mazingira ili kupunguza uharibifu wa mazingira katika viwanda vinavyozalisha bidhaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na upimaji wa kiwango cha uchafuzi wa hewa, maji, udongo na kubaini kelele hatarishi. Viwanda na taasisi zilizopata huduma hizo ni pamoja na Kilimanjaro Biochem Ltd, Serengeti Breweries Ltd, Huatan Investment, na TANESCO (Mtwara Gas Power Plant pamoja na Kinyerezi Gas Power Plant). Vilevile, Viwanja vya Ndege vya Arusha na Bukoba vilinufaika na huduma hizo.
Mheshimiwa Spika;
Mheshimiwa Spika;
Katika kuendelea kuvisaidia viwanda na mamlaka za maji kupunguza gharama za uendeshaji kupitia ufanisi wa matumizi ya nishati ya umeme, Wizara kupitia TIRDO imetoa ushauri kupitia tathmini za matumizi ya nishati. Kwa mfano, Mamlaka ya Maji Safi na Taka ya Tanga walipatiwa huduma hiyo. Aidha, majadiliano yanaendelea na Mamlaka ya Maji Safi na Taka ya Chalinze ili kuwapatia huduma hiyo.
Uendelezaji wa Teknolojia na Utafiti
Mheshimiwa Spika;
Wizara kupitia TIRDO imebuni na kutengeneza mashine kwa ajili ya kiwanda cha mfano cha kubangua korosho chenye uwezo wa kubangua kilo 300 kwa saa. Hadi sasa, tayari mashine imekamilika kwa asilimia 88. Lengo la Serikali ni kuhakikisha inabangua kiasi kikubwa cha korosho hapa nchini ili kutoa ajira nyingi kwa wananchi na kuhakikisha malighafi zinaongezewa thamani kabla ya kuuzwa nje ya nchi. Vilevile, TIRDO imebuni na kutengeneza mashine kwa ajili ya kiwanda cha mfano cha kuchakata mawese ambapo hadi sasa kazi zilizofanyika kama ifuatavyo: Kufanya tathmini ya malighafi iliyopo Mkoa wa Kigoma, kubaini ubora wa mawese yanayozalishwa, kubaini teknolojia inayotumika kwa sasa na teknolojia mpya inayohitajika na kununua mashine moja ya mfano kwa ajili ya kuifanyia utafiti utakaowezesha kuanza kutengeneza hapa nchini. TIRDO pia inatekeleza mradi wa ubunifu na usambazaji wa vitofali lishe vya kuzalishia uyoga wenye virutubisho (mushroom substrate blocks).
Mheshimiwa Spika;
Kituo cha CAMARTEC kimeendelea kushirikiana na Intermech Engineering katika utafiti na ubunifu wa kipandio kinachovutwa na trekta la magurudumu mawili (power tiller). Katika ushirikiano huo, CAMARTEC imefanya majaribio ya kipandio hicho na kuainisha maeneo yanayohitaji kufanyiwa maboresho. Hadi sasa, CAMARTEC inaendelea kuandaa mpango wa kufanya majaribio na maboresho ya teknolojia nyingine. Pia, CAMARTEC imefanikiwa kubuni na kuunda sampuli kifani (Prototypes) na uzalishaji wa mashine kwa ajili ya wateja. Mashine zilizotengenezwa ni Mashine ya kupura na kupepeta alizeti (3); Mashine ya kupukuchua mahindi (2); Mashine ya kupandia (11); Mashine ya kukata majani ya kulisha mifugo iendeshwayo kwa umeme (5); Mashine za kupura mazao mchanganyiko (3); Mashine ya kusaga karanga (1); na Mashine za kufyatua matofali ya udongo saruji.
Mheshimiwa Spika;
Kituo cha CAMARTEC kimekamilisha Mradi wa ujenzi wa mtambo wa biogesi wenye mita za ujazo katika Shule ya Genezareth iliyoko Kinyamwenda Singida. Mradi huo unakusudiwa kuzalisha nishati safi ya kupikia, mbolea hai kwa matumizi ya kuotesha mazao shambani kwa ajili ya matumizi ya shule na pia kusaidia kutibu taka zinazozalishwa chooni. Aidha, Kituo kimekamilisha zoezi la uhakiki wa mitambo ya biogesi iliyoripotiwa kujengwa wakati wa utekelezaji wa Programu ya Uenezi wa mitambo ya Biogesi kwa Ngazi ya Kaya Tanzania (TDBP). Zoezi linahusisha mitambo iliyojengwa chini ya Programu ikiwa ni mtekelezaji na pia Watekelezaji Wenza (IPs) wengine watano (5). Katika mwaka 2019/2020, jumla ya mitambo 259 ya TDBP na mitambo 817 ya watekelezaji wenza wa TDBP ilikuwa imehakikiwa.
Mheshimiwa Spika;
Kituo cha CAMARTEC kimekamilisha awamu ya tatu ya mafunzo ya ujasiriamali katika Biogesi kwa wanawake vijana 100 wa jamii za kifugaji kutoka Wilayani Ngorongoro. Mafunzo hayo yamejumuisha Biashara katika Sekta ya Biogesi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mitambo ya biogesi na matumizi ya mbolea hai (bioslurry) inayotoka kwenye mtambo wa biogesi. Pia, Kituo kilitoa mafunzo kwa vitendo kwa wakulima kuhusu teknolojia za kukata na kufunga majani ya malisho ya mifugo zinavyofanya kazi katika Halmashauri ya Meru Wilaya ya Arumeru. Aidha, wakulima zaidi ya 15 wa Mbozi, Mkoani Songwe walielimishwa namna ya kutumia kipandio (Planter) kikubwa cha mazao mbalimbali kinachovutwa na trekta.
Mheshimiwa Spika
Kituo cha CAMARTEC kimefanya ukarabati wa mitambo ya biogesi iliyojengwa chini ya ufadhili wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika Shule ya St. Bakanja Wilayani Buhigwe, Kigoma na Shule ya Queen of Apostles Wilayani Ushirombo, Mkoani Geita umefanyika na mitambo inafanya kazi vizuri. Aidha, Kituo kimefanya tathimini ya kazi ya marekebisho ya mitambo ya biogesi na mifumo yake yanayohitajika kufanyika kwenye Mradi wa REA kwa maeneo ya Kambi ya JKT Mlale Songea- Ruvuma na Gereza la Namajani lililoko Masasi – Mtwara na kuwasilisha taarifa REA kwa hatua stahiki.
Mheshimiwa Spika;
Mheshimiwa Spika;
Wizara kupitia TEMDO imeweza kusanifu uundaji wa mtambo wa kuchakata na kukausha muhogo ambapo mpaka sasa asilimia 40 ya utengenezaji na uundaji wa mashine imekamilika.
Uendelezaji wa Miradi ya Kimkakati na ya Kielelezo
Mheshimiwa Spika;
Mradi wa Eneo Maalum la Kiuchumi Bagamoyo (Bagamoyo Special Economic Zone Project) ni mradi wa kielelezo wa Taifa kwa mujibu wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2nd FYDP). Kimkakati, mradi unaojumuisha uendelezaji wa eneo la Bandari (Sea Port) kwenye eneo la Hekta 800 na Uendelezaji wa Eneo Maalum la Viwanda (Portside Industrial Zone) kwenye eneo la Hekta 9000. Mradi wa Eneo Maalum la Viwanda litaendelezwa kwa kuhusisha uendelezaji wa eneo la viwanda na uendelezaji wa Kituo cha kisasa cha Technolojia (High Technology Park).
Mheshimiwa Spika;
Katika eneo la Viwanda, Mamlaka ya EPZA imetoa leseni kwa jumla ya Makampuni kumi na moja ili kufanya uwekezaji. Hadi kufikia mwezi Februari 2020, makampuni mawili (Africa Dragon Enterprises Limited na Phiss Tannery Limited) yameanza uzalishaji na makampuni mengine yapo kwenye hatua mbalimbali za uendelezaji. Mchango unaotarajiwa kutokana na makampuni hayo ni kuwekeza mtaji unaokadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 67.34, ajira za moja kwa moja 1,651 na mauzo ya nje yanakadiriwa kuwa Dola za Kimarekani milioni 78.56 kwa mwaka. Aidha, Kampuni moja kati ya mawili yaliyoanza uzalishaji (African Dragon Limited), imeshachangia kodi ya Shilingi bilioni 9.86 katika kipindi cha miaka mitatu (2017 – 2019).
Mheshimiwa Spika;
Katika eneo la mradi wa Kituo cha kisasa cha Technolojia (High Technology Park) kwenye eneo la Bagamoyo SEZ, Mamlaka ya EPZ imeingia mkataba wa ushirikiano na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kuendeleza mradi huu katika eneo la hekta 175. Aidha, Serikali kupitia Mamlaka ya EPZ inashirikiana na Serikali ya Korea Kusini kupitia program ya ‘KSP- Knowledge Sharing Program’, inayoratibiwa na Korea Exim Bank yenye lengo la kufadhili uendelezaji wa miundombinu ya mradi.
Mheshimiwa Spika;
Kwa msingi huo, Mradi wa Bagamoyo SEZ unaendelea kutekelezwa katika maeneo ya Eneo Maalum la Viwanda (Portside Industrial Zone) na Kituo cha kisasa cha Technolojia (High Technology Park). Aidha, kuhusu eneo la Bandari (Sea Port), Wawekezaji waliojitokeza wa Kampuni ya Merchants Port Holdings Company Limited (CMPort) ya China na Mfuko wa Hifadhi ya Hazina wa Serikali ya Oman - State General Reserve Fund-SGRF, walishaanza majadiliano na kukubaliana katika baadhi ya masuala. Hata hivyo, kuna masula kadhaa ambayo Serikali imeweka msimamo wake na unahitaji maamuzi ya mwekezaji ili majadiliano yaweze kuendelea.
Mheshimiwa Spika,
Mheshimiwa Spika,
vilevile, Serikali imejielekeza katika kutekeleza Mradi wa chuma cha Liganga na makaa ya mawe ya Mchuchuma. Aidha, tafiti mbalimbali zilibainisha aina ya madini ya chuma (Magnetite Iron Ore) katika mwamba wa Liganga yanahitaji teknolojia maalum ya kuchenjua chuma na mchanganyiko wa madini mengine yakiwepo Vanadium na Titanium ambayo yana thamani kubwa. Mwaka 2010, mwekezaji Sichuan Hangda Group Ltd alipatikana na kuingia Mkataba wa Ubia na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC). Serikali inaangalia njia bora ya kuwezesha mradi huo kutekelezwa ikiwa ni pamoja na kurejea mikataba ya uwekezaji kwa kuzingatia Sheria Na. 5 ya Mamlaka ya Nchi ya Uangalizi wa Utajiri wa Asili ya mwaka 2017 na Sheria Na. 6 ya Mamlaka ya Nchi juu ya Majadiliano ya Mikataba yenye Masharti hasi ili uwekezaji huo uwe na maslahi mapana kwa nchi.
Mheshimiwa Spika;
Katika mwaka 2019/2020, Wizara kupitia TIRDO inaendelea kufanya “Techno Economic Study” katika Mradi wa Magadi Soda Engaruka. Lengo la utafiti huo ni kubainisha kiasi cha mahitaji ya magadi nchini, thamani ya uwekezaji utakaofanyika na faida za mradi huo kwa ujumla. Makadirio ya awali ya rasilimali magadi (brine) yameonesha uwepo wa kiasi cha mita za ujazo Bilioni 4.68. Aidha, ilibanika kuwa rasilimali hiyo inajiongeza kwa kiasi cha mita za ujazo wa milioni 1.9 kwa mwaka. Uhakiki wa rasilimali hii unaendelea sambamba na ukamilishaji wa upembuzi yakinifu wa mradi na athari ya mradi katika mazingira na jamii. Utafiti huo unategemewa kukamilika mwisho mwa mwezi Aprili, 2020.
Mheshimiwa Spika;
Katika mwaka 2019/2020 Wizara kupitia NDC imekamilisha upimaji wa eneo la TAMCO. Jumla ya ekari 201.04 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda na miundombinu. Kati ya hizo, ekari 43.04 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vya kutengeneza madawa ya binadamu; Ekari 55 kwa ajili ya viwanda vya kuunganisha magari; Ekari 94 kwa ajili ya viwanda vya nguo na mavazi; na Ekari 9 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika eneo hilo.
Mapitio ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda
Mapitio ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda
Mheshimiwa Spika;
Mapitio ya Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda (SIDP, 19962020) yanaendelea na tayari Wizara imekamilisha Tathmini na mapitio ya Awali ya Sera hiyo. Kwa sasa Wizara ipo katika hatua ya kuchambua wasilisho hilo ili kuwezesha hatua za tathmini za kina na uchambuzi ili hatimaye kumwezesha Mshauri Mwelekezi kukamilisha uandishi wa Research Background Paper na hivyoo kuwezesha maandalizi ya rasimu ya Sera na Mkakati wake. Utaratibu huo unalenga kuleta ufanisi na kuwa na uratibu unaozingatia mfumo wenye mwongozo wa usimamiaji wa utungaji sera Serikalini. Sera hiyo inategemewa kukamilishwa ndani ya mwaka 2020.
Utekelezaji wa Mikakati Mbalimbali ya Uendelezaji Viwanda Nchini
Mheshimiwa Spika;
Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Ngozi wa mwaka 20162020 umejikita katika kuendeleza mnyororo wa thamani wa zao la Ngozi. Katika kutekeleza mkakati huo, Serikali imetoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye malighafi na vifaa vinavyotumika kutengenezea viatu na bidhaa za ngozi vinavyoingizwa kutoka nje ya nchi. Lengo likiwa ni kupunguza gharama za uzalishaji kwa viwanda vya ngozi na kuvutia uwekezaji. Fursa hiyo imetumiwa na kiwanda cha Karanga Leather Industries ambacho hivi karibuni kimeingiza mashine na vifuasi (accessories). Vilevile, Kiwanda cha ACE leather Morogoro kimetumia fursa hiyo kuingiza mashine na vifuasi ili kusindika ngozi hadi hatua ya mwisho. Mkakati huo pia umehamasisha taasisi za umma na shule kununua bidhaa za ngozi hususan viatu kutoka viwanda vya ndani kulingana na upatikanaji. Kwa sasa maandalizi ya kuhuisha mkakati huo yanaendelea.
Mheshimiwa Spika;.
Katika kutekeleza Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Mafuta ya Alizeti wa mwaka 2016-2020, Wizara kupitia TEMDO imeweza kutengeneza mtambo(prototype) wa kukamua mafuta (Oil refinery Machine). Hadi sasa mtambo huo umefanyiwa majaribio ya mwisho ili kutengenezwa na kuwapa wadau kama vile SIDO watakaoweza kutengeneza mitambo mingi kibiashara (commercialization). Pia, TEMDO imeendelea kutengeneza kwa majaribio teknolojia zilizokwishahakikiwa na kusambaza teknolojia /mashine ya kukamua mbegu za alizeti kwa wajasiriamali (Sunflower seeds pressing machine/Oil expelling machine).
Mheshimiwa Spika,
Mheshimiwa Spika,
CAMARTEC imeendelea na utaratibu wa kuhaulisha mashine ya kupura na kupepeta alizeti kwa wajasiriamali wadogo. Lengo ni kuwezesha teknolojia hizo kusambazwa kwa wakulima pamoja na kuwezesha upatikanaji wake kirahisi katika maeneo ambayo zao la alizeti linalimwa kwa wingi hapa nchini. Kwa sasa, Wizara imeanza maandalizi ya kufanya tathmini ya utekelezaji wa mkakati huo ambao unafikia ukomo mwaka 2020.
Mheshimiwa Spika;
Mheshimiwa Spika;
Mkakati wa Pamba hadi Mavazi wa mwaka 2016-2020 unalenga uongezaji thamani zao la pamba hadi mavazi unaochochea uanzishwaji wa viwanda vya nguo na mavazi na vinavyotoa huduma (auxiliary industries). Viwanda hivyo ni pamoja na viwanda vya kutengeneza vifungo, lebo na zipu. Hivi sasa, Wizara imeanza hatua za uhuishaji wa Mkakati huo ambao utekelezaji wake unaishia mwezi Juni, 2020. Katika hatua hizo, mwezi Julai, 2019 Wizara ilifanya tathmini ya sekta hiyo na kubaini kuwa inakabiliwa changamoto mbalimbali zikiwemo tija ndogo katika uzalishaji wa pamba nchini, na teknolojia hafifu katika utengenezaji wa bidhaa mwambata zinazoweza kuzalishwa kutokana na uchambuaji wa pamba mbegu. Tathmini hiyo ni msingi wa kufanya marejeo ya Mkakati huo.
Uendelezaji wa Sekta Ndogo ya Mafuta ya Mawese
Mheshimiwa Spika
Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na wataalam kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuendeleza Viwanda (UNIDO) na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) ilifanya uchambuzi wa mnyororo mzima wa zao la mchikichi. Lengo lilikuwa kubaini changamoto zinazokabili zao hilo, kupendekeza suluhisho na kuwezesha kuchangia katika upatikanaji wa mafuta ya kula nchini. Pamoja na uchambuzi huo, Wizara kupitia taasisi zake za utafiti wa viwanda (TIRDO, CAMARTEC, TEMDO) na SIDO zilifanya uchambuzi zaidi na kuandaa maandiko (concept papers) ya teknolojia rahisi ya kuchakata chikichi. xiii) Uongezaji Tija na Ufanisi wa Uzalishaji katika Viwanda
Mheshimiwa Spika;
Katika kuimarisha uratibu wa shughuli za KAIZEN, Wizara iliandaa na kukamilisha miongozo ya kufundishia na kutoa huduma za KAIZEN kwa ufanisi (KAIZEN Consultancy Services & KAIZEN Technical Guideline). Miongozo hiyo inasaidia kudhibiti ubora wa huduma za KAIZEN zinazofikishwa kwa walengwa. Vilevile, Wizara ilikamilisha maandalizi ya Mpango wa Taifa wa kueneza falsafa ya KAIZEN Nchini (Framework for Quality and Productivity Improvement (KAIZEN) in Manufacturing Sector – FKM, 20202030). Mbali na kueneza KAIZEN nchini, mpango huo unahamasisha pia kuoanishwa kwa KAIZEN kwenye uendelezaji wa Kongano za Viwanda ili ziweze kuhimili ushindani.
Mheshimiwa Spika;
Mheshimiwa Spika;
Katika kipindi cha mwaka 2019/2020, Wizara imeendesha mafunzo ya uongezaji endelevu wa tija na ubora kwa kutumia falsafa ya KAIZEN. Juhudi hizo ziliwezesha kuongeza idadi ya wakufunzi kutoka 91 hadi 130 watakaosaidia kueneza falsafa hiyo viwandani. Lengo ni kuwezesha viwanda vilivyoko nchini na vile vitakavyoanzishwa viwe na ukuaji endelevu. Aidha, zaidi ya viwanda 102 (asilimia 25 Viwanda vikubwa na asilimia 75 ni viwanda vidogo) katika mikoa 8 vimenufaika na mafunzo kwa vitendo. 77. Mheshimiwa Spika: Katika mwaka 2019/2020, Wizara ilifanya tathimini ya hali ya utekelezaji wa Mradi wa KAIZEN. Tathmini hiyo ilibaini yafuatayo:- Kubadilika kwa maeneo ya kazi kuwa yenye staha; Kuongezeka kwa ubora na tija kwa bidhaa kwa viwanda vilivyopata mafunzo; Kuokoa muda wa utendaji kazi (lead time reduction); na Kubadilika kwa mtazamo wa watumishi viwandani katika utendaji kazi kuwa mzuri zaidi. Viwanda vilivyofanyiwa mafunzo viliweza kuokoa takribani Shilingi 368,609,000 kwa kutekeleza falsafa ya KAIZEN ipasavyo katika maeneo yao.
Mheshimiwa Spika: Katika kuhamasisha uenezaji wa falsafa ya KAIZEN nchini, Wizara imeendelea kuratibu Mashindano ya KAIZEN Kitaifa na kushiriki Kimataifa. Katika mashindano ya Kimataifa yaliyofanyika nchini Tunisia mwaka 2019, Tanzania ilipata ushindi wa kwanza kati ya Mataifa 16 yaliyoshiriki. Aidha, katika mashindano ya Kitaifa yaliyofanyika mwezi Februari, 2020 Kiwanda cha Shelly’s Pharmaceuticals kilipata ushindi wa kwanza kwa viwanda vikubwa na kwa upande wa viwanda vidogo, Kiwanda cha Tanzania Brush Products Ltd kilipata ushindi wa kwanza. Navipongeza viwanda hivyo kwa ushindi walioupata, ambapo kupitia ushindi huo vitaiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya KAIZEN Barani Afrika yatakayofanyika nchini Afrika Kusini mwezi Septemba, 2020. Juhudi hizo zimeipatia Tanzania fursa ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya KAIZEN Barani Afrika kwa mwaka 2021 yatakayohusisha zaidi ya nchi 16. Mashindano hayo yatakuwa ni fursa ya kuvutia wawekezaji, kutangaza vivutio vya utalii na hatimaye kuchangia ukuaji wa uchumi.
Hali ya Uzalishaji Bidhaa Viwandani
Uzalishaji wa Sukari
Mheshimwa Spika;
Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi ya kuwavutia wenye viwanda vya sukari nchini kuwekeza katika kuongeza ukubwa wa mashamba kwa nia ya kuongeza uzalishaji sukari nchini. Hadi sasa, Kiwanda cha Kagera Sugar kina mpango wa kuongeza kilimo cha Miwa hekari 14,000 katika shamba la Kitengule ambapo kiwanda kitaongeza uzalishaji wa Sukari kutoka Tani 80,000 za sasa hadi kufikia Tani 180,000 katika kipindi cha miaka 5 ijayo. Vilevile, Kiwanda cha Mtibwa Sugar hivi sasa kinaendelea na ujenzi wa mabwawa ambapo utakapokamilika kiwanda kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 100,000 kutoka 30,000 zinazozalishwa sasa. Aidha, Kiwanda cha Kilombero Sugar kipo katika majadiliano na Serikali kwa lengo la kuongeza uwezo wa uzalishaji. Kupitia Mpango huo, Kiwanda kitaongeza uzalishaji wa Sukari kupitia wakulima wadogo ‘Outgrower Scheme’, uzalishaji unatarajiwa kuongezeka hadi kufikia Tani 265,000 kutoka 120,000 za sasa kwa kipindi cha miaka 5.
Mheshimwa Spika;
ili kuongeza uzalishaji zaidi kwa lengo la kukidhi mahitaji ya ndani na kuuza ziada nje ya nchi, Serikali imeendelea kuhamasisha uwekezaji katika miradi mipya ya kilimo cha miwa na uzalishaji wa sukari kwa viwanda vikubwa na vidogo. Miradi hiyo ni pamoja: Bagamoyo ambapo kupitia mradi huo tani 35,000 ya Sukari zitazalishwa; na Mradi wa Mkulazi unatarajia kuzalisha tani 50,000. Wawekezaji wengine ambao wapo kwenye hatua ya kuhaulisha maeneo ya ardhi kama vile Nkusu Theo ya Ruvuma na Ray Sugar ya Mtwara. Wawekezaji kutoka Mauritius kwa ajili ya mradi wa shamba uliopo Rifiji hivi sasa wako kwenye mazungumzo na Serikali. Aidha, Wizara yangu inaendelea kuhamasisha uchakataji wa miwa na kutengeneza sukari kupitia wajasiriamali wadogo na wa kati. Tayari taasisi ya TEMDO inaendelea na kubuni mtambo rahisi kulingana na mazingira yao ili kuwawezesha wajasiriamali hao kuchakata miwa na kutengeneza sukari kwa teknolojia nafuu. Suala hilo litatia chachu jitihada za kukabiliana na tatizo la sukari nchini na kutoa ajira kwa Watanzania kupitia Sekta ya
55
Viwanda Vidogo ambayo kitakwimu ndio inatoa ajira nyingi nchini.
81. Mheshimiwa Spika; Makadirio ya uzalishaji wa sukari kwa msimu wa mwaka 2019/2020 yalikuwa tani 345,296 kwa viwanda vya ndani sawa na asilimia 73.46 ya kiasi cha sukari inayokadiriwa kwa matumizi ya kawaida. Aidha, hadi kufikia mwezi Aprili, 2020 uzalishaji wa sukari nchini, ulikuwa jumla ya tani 298, 949, wakati mahitaji ya sukari kwa mwaka ni wastani wa tani 635,000. Kati ya mahitaji hayo, tani 470,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na tani 165,000 kwa matumizi ya viwandani. Makadirio hayo yametokana na ukweli kwamba kiasi cha mahitaji ya sukari ya matumizi ya kawaida kwa mwezi ni wastani wa tani 38,000.
b) Uzalishaji Dawa na Vifaa Tiba 82. Mheshimiwa Spika; Sekta ya Viwanda vya Dawa na Vifaa Tiba ina jumla ya viwanda 14 ambapo viwanda 12 vinatengeneza dawa za binadamu, viwanda viwili dawa za mifugo na kiwanda kimoja kinatengeneza vifaa tiba. Wizara ilichukua hatua za makusudi ili kuhakikisha Sekta hiyo inaongeza uwekezaji kwenye Viwanda vya Dawa na Vifaa Tiba ikiwa ni sambamba na kuongeza ufanisi wa viwanda vilivyopo ili kufikia asilimia 60 ya uzalishaji wa Dawa na Vifaa Tiba Nchini ifikapo Mwaka 2025. Hatua hizo ni:
56
Kuunda Kamati ya Kitaifa inayoshughulikia Sekta ya Viwanda vya Dawa na Vifaa Tiba (NPCC); na Kuweka vivutio vya uwekezaji kwa lengo la kuhamasisha wawekezaji wa ndani na Nje ya Nchi (Kiambatisho Na. 4).
83. Mheshimiwa Spika, Ili kuvutia wawekezaji katika sekta hiyo, Serikali imefanya yafuatayo: kuondoa VAT kwa vifungashio vya dawa zinazozalishwa nje na ndani ya nchi; kushusha kodi ya mapato kwa asilimia 30 ambayo imesaidia kuhamasisha uwekezaji mpya na upanuzi wa viwanda, kwa muda wa miaka miwili kwa miradi mipya ya viwanda vya dawa; na Kuweka upendeleo maalum kwa ununuzi wa dawa zinazozalishwa na viwanda vya ndani kupitia MSD.
xv) Jitihada za Wizara katika Vita Dhidi ya COVID-19 84. Mheshimiwa Spika; Katika kukabiliana na janga la ugonjwa wa Covid-19 unaosababisha homa kali ya mapafu, Mwezi Machi 2020, Wizara ilikutana na wazalishaji wa malighafi ya kutengeneza vitakasa mikono (ethanol) na wazalishaji wa bidhaa hizo. Lengo likiwa ni kujadiliana na wenye viwanda pamoja na wadau wengine namna ya kufanikisha utengenezaji na upatikanaji wa vifaa kinga vya kuzuia usambaaji wa ugonjwa huo. Viwanda hivyo vimeitikia wito
57
wa kuunga mkono Serikali katika vita dhidi ya ugonjwa huo. Kwa mfano Kiwanda cha Kilombero Sugar Ltd kinachomilikiwa kwa ubia na Serikali kilichangia jumla ya lita 30,000 za Ethanol kwa ajili ya kutengeneza vitakasa mikono ambapo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilipewa lita 20,000 na kiasi kilichobaki zilipewa Taasisi za SIDO na TIRDO. Mwitikio huo, umeweza kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vya kutengeneza barakoa, vitakasa mikono, sabuni za kunawa mikono na disinfectants, ili kuongeza upatikanaji wa bidhaa hizo. Hadi sasa, kuna jumla ya viwanda na taasisi 12 ambazo zinatengeneza vifaa tiba kama Barakoa, Vitakasa mikono na mavazi maalum kwa watoa huduma za afya (Kiambatisho Na 5). Aidha, Viwanda vidogo 55 vya nguo na mavazi pia vimeunga mkono kwa kuanza kutengeneza barakoa kwa kutumia malighafi ya kitambaa. Vivyo hivyo, viwanda vya kutengeneza vitakasa mikono vilivyosajiliwa hadi sasa vimefikia 40.
85. Mheshimiwa Spika; Wizara inaendelea kufuatilia maelekezo ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa katika kikao chake na wadau wa Sekta Ndogo ya Viwanda vya Dawa na Vifaa Tiba Nchini kilichofanyika Jijini Dar es Salaam mwaka 2018. Katika kutekeleza agizo hilo, wawekezaji 11 wanaendelea na ujenzi wa
58
viwanda vya Dawa na Vifaa Tiba na ujenzi umefikia hatua mbalimbali kama inavyoonekana katika Kiambatisho Na. 6. Lengo la Serikali ni kuokoa fedha ambazo zinatumika kuagiza dawa na vifaa tiba hivyo nje ya nchi na hivyo kuendelea kutengeneza ajira hapa nchini. Aidha lengo hilo linakusudia kuhakikisha afya za Watanzania zinakuwa ni suala la kipaombele wakati wote.
86. Mheshimiwa Spika; Vilevile, Wizara kupitia TIRDO imeweza kutengeneza mtambo unaotumika kuzalisha bioethanol inayotokana na zao la muhogo ambayo inafaa kutumika kwa matumizi mbalimbali ya hospitali, viwanda vya pombe na majiko. Kutokana na bioethanol hiyo, TIRDO imeweza kutengeneza kitakasa mikono (sanitizer) ambacho tayari kinatumika kwa wanajamii kwa matumizi ya kujikinga na kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19). Mpaka sasa, TIRDO imeweza kutengeneza lita 202 za vitakasa mikono na kuwafikia watu mbalimbali kwa ajili ya matumizi.
87. Mheshimiwa Spika; Wizara inaendelea na kazi ya ufanyaji tathmini ya mahitaji ya vitakasa mikono nchini kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Mkemia Mkuu wa Serikali, Wazalishaji wa Ethanol, TMDA na TPMA. Aidha, kupatikana kwa takwimu halisi
59
kutasaidia Serikali kufanya maamuzi ya haraka hususan ya kuagiza Ethanol ambayo ni malighafi muhimu katika kutengenezea vitakasa mikono.
88. Mheshimiwa Spika; Napenda kuchukua nafasi hii kutoa onyo kwa wafanyabiashara wanaotumia mazingira ya ugonjwa huo kama fursa ya kujinufaisha badala ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupambana na Janga hili kuacha mara moja vitendo hivyo. Nawasihi wajielekeze katika kulinda afya za wananchi wetu kwani Serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vya aina hiyo.
i) Jitihada za kuwalinda Wakulima Dhidi ya Mifumo ya Kinyonyaji katika Soko
89. Mheshimiwa Spika; Kipekee naomba nimpongeze Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali anayoingoza kwa namna alivyosimama imara na kuweka msimamo thabiti dhidi ya mifumo ya kumnyonya mkulima katika mazao mbalimbali na hususan korosho na pamba. Wizara itahakikisha kupitia taasisi zake ikiwemo FCC inasimamia maeneo mengine kuharibu mifumo ya aina hiyo iliyowekwa na wafanyabishara wasio waaminifu kwa lengo la kumnyonya mkulima. Mheshimiwa Rais ni mfano wa kuigwa katika utendaji wetu
60
hasa katika kuhakikisha haki za wakulima na wananchi wanyonge zinalindwa. Na hii inadhihirisha utayari wake katika kuhamasisha wananchi kufanya kazi kwa kujituma na hivyo kuakisi kauli yake ya “HAPA KAZI TU”.
ii) Kuendeleza Teknolojia za Uongezaji Thamani Mazao ya Kimkakati
90. Mheshimiwa Spika; Katika kuhakikisha Mazao ya kimkakati yanaongezwa thamani, Wizara kupitia taasisi zake za utafiti imeendelea kubuni teknolojia mbalimbali rafiki ambazo zitatumika katika kuongeza thamani ya Mazao ya Kimkakati yaani, Korosho, Chikichi, Mkonge, Zabibu, Miwa kwa ajili ya kutengeneza sukari, mbegu za mafuta hususan alizeti na karanga na Mazao ya Ngozi. Jitihada hizo zinaenda sambamba na utekelezaji wa Mradi wa ASDP II kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Sekta nyingine za uzalishaji katika kuhakikisha kuwa tunaongeza thamani ya mazao hayo kabla ya kuuzwa ili kuhakikisha mkulima anapata soko la uhakika na bei shindani .
iii) Teknolojia ya Kupura na Kupepeta Alizeti
91. Mheshimiwa Spika; Wizara kupitia Kituo cha CAMARTEC inaendelea na utaratibu wa kuhawilisha teknolojia za mashine ya kupura na
61
kupepeta alizeti kwa Makau Engineering ambaye ni mjasiriamali mdogo. Lengo ni kuwezesha teknolojia hiyo iliyobuniwa na CAMARTEC kuweza kusambazwa kwa wakulima na kuwezesha upatikanaji wa teknolojia hiyo kirahisi kutokana na mahitaji yake katika maeneo ambayo zao la alizeti linalimwa kwa wingi hapa nchini. Hivi sasa wakulima wa zao hilo wanatumia mbinu za kizamani ambazo zinabakisha alizeti nyingi kwenye upuraji. Vilevile, mbinu hizo zinapunguza ubora wa alizeti inayovunwa na kumsababishia mkulima hasara. iv) Uendelezaji wa Sekta Ndogo ya Mafuta ya Mawese
92. Mheshimiwa Spika; Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na wataalam kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuendeleza Viwanda (UNIDO) na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) ilifanya uchambuzi wa mnyororo mzima wa zao la mchikichi. Lengo lilikuwa kubaini changamoto zinazokabili zao hilo, kupendekeza suluhisho na kuwezesha kuchangia katika upatikanaji wa mafuta ya kula nchini. Pamoja na uchambuzi huo, Wizara kupitia taasisi zake za utafiti wa viwanda (TIRDO, CAMARTEC, TEMDO) na SIDO zilifanya uchambuzi zaidi na kuandaa maandiko (concept papers) ya teknolojia rahisi ya kuchakata chikichi.
62
v) Upatikanaji wa Teknolojia Rahisi za Kuchakata na Kuongeza Thamani Mazao ya Kimkakati kwa Wajasiriamali Wadogo
93. Mheshimiwa Spika; katika kuhakikisha upatikanaji wa Sukari unakuwa wa uhakika na wakutabirika, Wizara kupitia taasisi ya TEMDO inaendelea kubuni mtambo wa kukamua miwa na kutengeneza Sukari kwa ajili ya wajasiriamali wa kati na wadogo. Tayari baadhi ya wajasiriamali wameonesha nia ya kupata teknolojia hiyo pindi itakapokamilika. Suala hilo litasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na upungufu wa Sukari nchini na kuongeza ajira kwa kuwa itahamasisha wananchi wengi kujihusisha na kilimo cha miwa.
Upatikanaji wa Teknolojia Rahisi za Kuchakata Mkonge
94. Mheshimiwa Spika; Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea na jitihada za dhati kufufua zao la Mkonge ambalo lilikuwa moja ya mazao ya biashara yaliyokuwa yanaliingizia Taifa fedha nyingi za kigeni na kuchangamsha uchumi wa Mikoa ya Tanga na Morogoro. Wizara inaenda na kasi hiyo ili kuhakikisha jitihada hizo zinakuwa na faida kubwa kwa mkulima na Taifa kwa ujumla. Hivyo, Wizara kupitia TEMDO iko katika hatua
63
ya kukamilisha mashine ndogo (Korona) kwa ajili ya kuchakata mkonge. Lengo ni kuwarahisishia wajasiriamali wadogo kuchakata Mkonge ili kupata nyuzi. Kukamilika kwa mashine hiyo na kusambazwa kwa wajasiriamali itasaidia wakulima kuuza nyuzi badala ya Mkonge ghafi. Utamaduni tuliozoea wa kuuza malighafi ambayo huuzwa kwa bei ya chini ulisababisha kwa kipindi kirefu kuwakatisha tamaa wakulima na kupunguza uzalishaji na wengine kuacha kabisa kilimo cha Mkonge. Upatikanaji wa Teknolojia Rahisi za Kuchakata Zabibu 95. Mheshimiwa Spika; Wizara inaendelea kuhakikisha zao la zabibu zinapata soko la uhakika ili kuhamamisha ulimaji wa zao hilo. Katika jitihada hizo Bunge kupitia Sheria ya fedha ya mwaka 2019 ilipunguza baadhi ya tozo katika Mvinyo ili kuleta chachu kwa Kampuni kubwa kununua mchuzi wa Zabibu kwa wazalishaji wadogo na wa kati wa mchuzi. Sambamba na hilo, Wizara kupitia TEMDO imebuni teknolojia ya kukamua mchuzi wa zabibu (Grapes Distemer) ambayo ikikamilika itaongeza kasi ya uongezaji thamani zao hilo na hivyo wakulima wadogo kupata soko la uhakika la zao hilo.
64
Uendelezaji na Uongezaji Thamani katika Zao la Ngozi
96. Mheshimiwa Spika; Wizara kupitia TIRDO imefanikiwa kutoa mafunzo kwa wafugaji zaidi ya mia mbili (200) katika Halmashauri za Wilaya za Arumeru, Arusha, Longido na Monduli juu ya namna ya kuongeza thamani katika ngozi (Skin and hide value addition) kwa kutumia teknolojia zilizopo hapa nchini ambazo zilikuwa hazijulikani kwa wafugaji. Mafunzo hayo yamesaidia kuongeza thamani kwenye bidhaa za ngozi pamoja na kuwaongezea kipato wafugaji kupitia bei bora za ngozi.
4.2.2. Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo i) Mapitio ya Sera ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo
97. Mheshimiwa Spika; Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaendelea kufanya marejeo ya Sera ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo ya mwaka 2003. Kwa sasa, Wizara inakamilisha kufanya tafiti katika maeneo mawili ambayo ni Rural Industrialization na Technology and Innovation. Baada ya kukamilika kwa tafiti hizo uandishi wa Sera hiyo pamoja na Mkakati wa Utekelezaji wake utaanza.
65
Wizara inatarajia kukamilisha Sera ifikapo mwishoni mwa mwaka 2020.
ii) Upatikanaji wa Huduma za Fedha kwa Wajasiriamali
98. Mheshimiwa Spika; Upatikanaji wa mitaji kwa wajasiriamali wadogo ni nyenzo muhimu katika kuanzisha na kuendeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi. Wizara, kupitia SIDO imekuwa ikitoa mikopo kwa wajasiriamali kupitia Mfuko wa Wafanyabishara Wananchi (National Entrepreneurship Development Fund - NEDF). Katika kipindi cha Julai 2019 hadi Machi 2020 jumla ya mikopo 2,020 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 3.885 ilitolewa kwa wajasiriamali mbalimbali kote nchini. Kati ya mikopo hiyo, asilimia 51.3 ilitotolewa kwa wanawake na asilimia 48.7 ilitolewa kwa wanaume. Aidha, asilimia 39.2 ya mikopo hiyo ilitolewa maeneo ya vijijini na asilimia 60.2, ilitolewa mijini. Mikopo hiyo imekuwa chachu ya uendelezaji viwanda ambapo jumla ya shilingi Bilioni 1.374 zilizokopeshwa ziliwezesha kuanzishwa kwa viwanda 551 na kuwezesha ajira 6,193 kupatikana.
iii) Uzalishaji na Usambazaji wa Teknolojia
99. Mheshimiwa Spika; Wizara kupitia Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo nchini,
66
imewasaidia na kuwaendeleza wajasiriamali 42 wenye ubunifu wa teknolojia na mawazo ya bidhaa mpya kupitia programu ya kiatamizi (Incubation Programme). Wajasiriamali hao hupatiwa huduma mbalimbali kama vile maeneo ya kufanyia kazi, mafunzo, ushauri wa kiufundi pamoja na mitaji ili waweze kukua na kufikia viwango vya kujitegemea sambamba na kuzalisha bidhaa bora zenye kukubalika sokoni.
100. Mheshimiwa Spika; Katika mwaka 2019/2020, jumla ya teknolojia na mawazo ya bidhaa mpya 25 yalihudumiwa katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Kilimanjaro, Mbeya, Mara, Manyara na Tanga. Teknolojia hizo zilihusu utengenezaji wa sabuni, mafuta ya losheni, utengenezaji wa kemikali za viwandani, usindikaji vyakula, uchakataji na utengenezaji wa bidhaa za ngozi, utengenezaji wa mkaa mbadala (briquettes) na utengenezaji wa zana za kilimo. Bidhaa na zana hizo zimeweza kuingia sokoni na kutumiwa na wananchi kadri ya mahitaji yao. Jitihada za uendelezaji teknolojia imejitokeza pia kwa taasisi zetu kuingia katika uzalishaji wa sanitizer kama njia ya kupambana na kujilinda na corona. Kupitia wajasiriamali wake, SIDO imetengeneza mtambo wa kutakasa mwili mzima ambao utafaa sana kuwekwa kwenye maeneo ya maofisi, vivuko, stendi za mabasi, vituo vya mipakani, nk. UNDP kwa
67
kuona jitihada na nguvu hizo imeonesha interest ya kununua kati ya mitambo 50 na 100 ili iweze kutumika kwenye maeneo mbali mbali ya umma.
101. Mheshimiwa Spika; Karakana zilizoko katika Ofisi za SIDO mikoani ziliweza kutambua au kuzalisha jumla ya teknolojia mpya 272 na kusambaza kwa wajasiriamali. Teknolojia hizo zilihusu ubanguaji wa korosho, usindikaji wa mihogo, ukamuaji wa mafuta ya mawese, usindikaji na ufungashaji wa vyakula mbalimbali, utengenezaji wa sabuni na vitakasa mikono, usindikaji wa ngozi na utengenezaji wa chaki, usindikaji wa asali, mitambo ya kuvunia mpunga, mahindi na mtama, mashine za kuchakata tangawizi, kutengeneza misumari na mashine za kutengeneza vyakula vya mifugo kwa kutaja maeneo machache ya teknolojia hizo. Teknolojia hizo zimeweza kurahisisha kazi kwa wakulima na zile za matumizi ya moja kwa moja zimeingia sokoni na kutumiwa na wananchi.
iv) Uendelezaji Maeneo na Majengo ya Uwekezaji wa Wajasiriamali kuendeleza Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo
102. Mheshimiwa Spika; Wizara kupitia SIDO imeendelea kupanua huduma za upatikanaji wa maeneo ya uzalishaji bidhaa kwa wajasiriamali ambapo mwezi Juni mwaka 2019
68
Wizara ilipokea Shilingi Bilioni moja toka Bajeti ya mwaka 2018/2019 kwa ajili ya ujenzi wa majengo viwanda (industrial sheds) katika mikoa ya Kigoma, Mtwara na Ruvuma. Hadi kufikia mwezi Machi, 2020 SIDO imekamilisha upembuzi yakinifu wa majengo matatu pamoja na michoro ya usanifu (architectural drawings) katika mikoa ya Mtwara (2) na Kigoma(1) na kuanza ujenzi. Kwa upande wa Mkoa wa Ruvuma, SIDO wamepata kiwanja cha ekari 19.9 katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kwa ajili ya ujenzi wa Mtaa wa Viwanda na Ofisi itakayokuwa na kituo cha mafunzo. Ukamilishaji wa majengo viwanda (industrial sheds) unategemewa kuwezesha uanzishwaji wa viwanda vipya saba vitakavyotengeneza ajira 76.
v) Uendelezaji wa Vituo vya Teknolojia
103. Mheshimiwa Spika; Wizara kupitia SIDO, inamiliki na kusimamia vituo saba vya uendelezaji teknolojia katika mikoa ya Arusha, Iringa, Kigoma, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya na Shinyanga. Vituo hivyo vimekuwa vikibuni, kutengeneza na kuendeleza teknolojia mbalimbali kulingana na mahitaji ya wajasiriamali katika maeneo hayo kwa kuzingatia mkakati wa Wilaya Moja Bidhaa Moja (One District One Product – ODOP) na fursa nyingine zinazojitokeza. Vituo hivyo viliweza
69
kutengeneza jumla ya mashine 268 na kuziuza kwa wajasiriamali.
104. Mheshimiwa Spika; Wizara kupitia SIDO imeendelea kuboresha vituo hivyo vya teknolojia kwa kufanya ukarabati wa mitambo iliyopo na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi kwa kutumia dhana ya KAIZEN katika uzalishaji ili kuongeza tija. Wizara ilipokea jumla ya Shilingi Bilioni moja mwezi Juni 2019 kutoka katika bajeti ya mwaka 2018/2019 kwa ajili ya kufanya maboresho katika vituo vya Lindi, Shinyanga na Kigoma kwa kuvinunulia baadhi ya mitambo ya kisasa. Hadi kufika mwezi Machi 2020, tayari vipimo vya mitambo hiyo(specifications) pamoja na gharama zake zimeainishwa. Kwa sasa shirika limeagiza mashine hizo za kisasa (computerized) kutoka kampuni ya Jiangsu Longshen Machine Manufacturing Co.Ltd ya China ambapo tayari malipo ya awali yamefanyika.
vi) Utoaji wa Mafunzo na Huduma za Ushauri wa Kiufundi kwa Wajasiriamali
105. Mheshimiwa Spika; Wizara imeendelea kutoa huduma za ushauri wa kiufundi kupitia SIDO hasa katika maeneo ya uthibiti wa ubora wa bidhaa, michoro ya majengo ya viwanda, ufungaji wa mashine,
70
ukarabati wa mashine, upangaji wa mashine viwandani (equipment layout) pamoja na uchaguzi wa teknolojia sahihi kulingana na aina ya bidhaa inayozalishwa na mjasiriamali. Katika mwaka 2019/2020 jumla ya wajasiriamali 5,145 walipata ushauri wa kiufundi katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Vilevile, SIDO imeendelea kutoa huduma ya mafunzo mbalimbali kwa wajasiriamali ili kuwawezesha kupata ujuzi wa kubuni, kuanzisha na kuendesha shughuli mbalimbali za kiuchumi. Kupitia ofisi zake zilizoko mikoani shirika lilitoa mafunzo kwa wajasiriamali 12,589 ambapo mafunzo hayo yalijikita katika stadi mbalimbali.
106. Mheshimiwa Spika; Wizara kupitia SIDO imeendelea kuboresha Vituo vya Mafunzo kwa wajasiriamali (Training Cum Production Centres-TPCs) kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo. Katika mwaka 2019/2020, Wizara kwa kushirikiana na Mradi wa “Local Investment Climate” (LIC) imefanya ukarabati wa jengo la mafunzo na ofisi katika TPC ya Dodoma ambayo inajihusisha na utoaji wa mafunzo ya uzalishaji bidhaa za ngozi. Aidha, Kupitia Mradi huo kituo hicho cha mafunzo ya bidhaa za ngozi kimenunuliwa mashine na vifaa vya kisasa vya uzalishaji pamoja na vifaa vya kufundishia. Wizara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo itaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ukarabati wa vituo vingine vya mafunzo na
71
uzalishaji (TPCs) vilivyopo katika ofisi za SIDO mikoani.
vii) Kuhamasisha Ujenzi wa Viwanda Vidogo Nchini
107. Mheshimiwa Spika; Wizara imeendelea kuhamasisha ujenzi wa viwanda nchini hususan viwanda vidogo na vya kati ambavyo ni rahisi kuanzishwa kutokana na uwepo wa malighafi za kutosha kwa aina hiyo ya viwanda pamoja na kutohitaji mitaji mikubwa katika uanzishwaji wake. Uhamasishaji huo umekuwa ukifanyika kupitia uongezaji wa mitaji kwa wajasiriamali kwa kuwapa mikopo kupitia Skimu ya Ukopeshaji kwa Wajasiriamali (SME Credit Guarantee Scheme-CGS) inayosimamiwa kwa pamoja kati ya SIDO na CRDB. Aidha, kupitia Mfuko wa NEDF unaosimamiwa na SIDO, wajasiriamali wamekuwa wakipatiwa mikopo kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza viwanda vidogo katika maeneo ya mijini na vijijini. Katika kipindi cha kuanzia Julai 2019 hadi Machi 2020 kupitia mifuko hii, jumla ya viwanda vipya 437 vilianzishwa na kutoa ajira 1,481. Viwanda hivyo ni pamoja na vya kusindika nafaka, korosho, mafuta ya alizeti, asali, kutengeneza bidhaa za ngozi, sabuni, chaki, vyakula vya mifugo, ushonaji na useremala.
72
108. Mheshimiwa Spika; Sambamba na utoaji mikopo kwa wajasiriamali, Wizara kupitia SIDO imekuwa ikitoa mafunzo na huduma za kiufundi kwa wenye viwanda pamoja na kuwapatia sehemu za kufanyia kazi baadhi ya wajasiriamali wenye mawazo/ubunifu wa teknolojia mbalimbali za uzalishaji mali kupitia programu ya kiatamizi (incubation programme). Huduma hizi zimehamasisha uanzishaji na uendelezaji wa viwanda pamoja na kuongeza tija katika uzalishaji wa bidhaa zenye ubora.
viii) Kuimarisha Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO)
109. Mheshimiwa Spika; Wizara imeendelea kuimarisha SIDO kwa kutoa fursa za mafunzo kwa wataalamu wake kwa kubadilishana ujuzi katika nyanja mbalimbali zikiwemo za teknolojia. Katika kipindi cha Julai 2019 hadi Machi 2020 wafanyakazi wa SIDO waliweza kwenda China, India na kushirikiana na taasisi za ndani vikiwemo vyuo vikuu vya Mbeya, SUA na Dar es Salaam kwa ajili ya kuongeza ujuzi. Aidha, Wizara itaendelea kuimarisha SIDO hususan katika maeneo ya Vituo vyake vya maendeleo ya Teknolojia (TDCs), Ujenzi na uboreshaji miundombinu katika mitaa ya viwanda ya SIDO na utumiaji wa TEHAMA
0 Comments