Pengine umeshawahi kusikia jina Chala mahali popote pale, iwe jina la Mtu au kitu fulani, sasa leo naomba nikueleze tu kwamba CHALA ni jina la Ziwa moja la maajabu lililopo Wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro, ziwa hili lipo kati ya mpaka wa Kenya na Tanzania, yaani kila nchi ina sehemu ya ziwa hilo.
Na Grace Semfuko, Rombo.
Na Grace Semfuko, Rombo.
Ziwa Chala lina fursa za Uwekezaji katika Sekta ya Utalii kutokana na
wageni wengi kuwasili katika eneo hilo kujionea maajabu ya ziwa hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)Bw. Geoffrey Mwambe akiangalia maajabu ya ziwa hilo lenye mandhari nzuri ya kuvutia, Mwambe na ujumbe wake kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania alifanya ziara ya kuangalia fursa za uwekezaji kwenye ziwa hilo.
Ziwa hili la Chala lipo kati ya Tanzania na Kenya jirani na mpaka
wa Holili. Chala ni la mtu, inasemekana Mzee huyo na Familia yake alijitenga
na jamii nyingine na kuweka makazi katika moja ya vilima
vinavyozunguka wilaya ya Rombo.
Mzee Chala inasemekana takribani miaka laki mbili iliyopita
alikaa hapo na wakati huo kulikuwa na kilima kilichokuwa na volcano
Volcano hiyo inahisiwa ililipuka dhoruba yenye kishindo kikubwa na
matokeo yake kilima kilizama chini hivyo kufanya kilima kugeuka shimo kubwa
lenye kina cha takribani mita 300!
Mzee Chala na mji wake, Watoto,wake zake, mifugo na kila kitu vyote
inasemekana vilizama kwenye shimo(cretor) hilo ambalo baadaye mkondo wa maji wa
chini kwa chini kutoka mlima mkubwa (mrefu) Afrika yaani Kilimanjaro
yalibainika kujaza shimo hilo na kuwa ziwa!
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)Bw. Geoffrey Mwambe (mwenye koti) na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Bi. Agness Hokororo (mwenye kitenge) wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Wilaya ya Rombo na Maafisa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) katika Ziwa Chala.
Mkondo huo wa chini kwa kwa chini ulijaza cretor hilo ambalo kwa sasa
Ziwa Chala badala ya kilima Chala lenye takribani ukubwa wa mita 500 urefu,
upana mita 200 na kina yaani kwenda chini mita 300 (viwanja vitatu vya mpira wa
miguu!.
Ziwa Chala linavyoonekana kwa upande mmoja eneo la Rombo.
Ziwa hilo la ajabu ambalo halina mto unaoleta maji kwa juu,
huonekana kuwa na kina kirefu kwa maana ya ujazo wa maji wakati wa
kiangazi tu, wakati ambao ukianangalia theruji ya Mlima Kilimanjaro
huonekana kupungua kwa kuyeyuka kwa joto, lakini ziwa Chala huonekana kupungua
kina au kukauka wakati wa masika yaani kipindi cha baridi ambapo Mlima
Kilimanajaro hunekana kufunikwa na theruji, hivyo kuthibitisha ziwa Chala
kukosa maji ya kulijaza!
Licha ya mambo mengine ya ajabu kuonekana katika ziwa hilo ambyo mengi
ni hadithi za viumbe vya ajabu kwa imani za mashetani,chunusi na mizimu
kuonekana na vifo vya mara kwa mara kwa watafiti na watu wanoogelea, pikiniki
na shughuli za utalii katika ziwa hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)Bw. Geoffrey Mwambe na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Bi Agness Hokororo wakielekea eneo linapoonekana Ziwa Chala.
Kuna simulizi mbalimbali za kiimani zikihusisha ziwa hilo ikiwepo ile ya
kila mwezi wa kumi na mbili ya kila mwaka, nyakati za usiku huonekana boti
lenye taa ambayo huwa linaelea majini kutoka upande mmoja kwenda
kwingine, lakini Asubuhi huwa haionekani tena.
Simulizi nyingine ni Watafiti kutoka Ulaya walipandikiza viumbe hai
kwenye ziwa hilo wakiwemo samaki wa maji baridi na mamba ili waone kama
wanaweza kuishi humo na kuzaliana kwani awali hakukuwa na viumbe hai, baada ya
mwaka mmoja wazungu hao sita walirudi kuona matokeo na kwa bahati mbaya mamba walikuwa
wakubwa walipindua mtumbwi wao na watafitti wawili kati yao wakageuzwa
kitoweo wa mamba hao!
Wazungu walikasirika wakaenda kuleta nyama zenye sumu na mamba wote
walionekana kuelea wakiwa wamekufa! kwa sasa ziwa halina mamba tena ila kuna
samaki na kuna wakati wanaoneka nyoka wakubwa kama chatu na sawaka. Wito
unatolewa kwa wizara husika, kutumia njia zake kutangaza ziwa hilo kama kivutio
cha utalii.
0 Comments