Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

Ni Bajeti ya kuimarisha Uwekezaji Nchini (2020/2021)


Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango Juni 11,2020 amesoma hotuba ya makadirio ya Bajeti ya Serikali ya Mwaka wa fedha 2020/2021 Bungeni Jijini Dodoma.

Na Grace Semfuko.

Wakati akisoma Bajeti hiyo alisema Sera ya bajeti hiyo ni kuhakikisha inachochea ongezeko la ajira na kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji Nchini Tanzania.

alisema Bajeti hiyo imeandaliwa kwa kuzingatia lengo kuu la kuitaka Serikali iendelee kuimarisha mazingira wezeshi ya ufanyaji wa biashara nchini

Alisema hatua hiyo ni pamoja na kuhakikisha miundombinu ya kiuchumi inaboreshwa, kuwepo kwa sera rafiki za fedha na za kikodi, mfumo mzuri wa marekebisho ya baadhi ya sekta, upatikanaji wa ardhi, vibali vya kazi na nguvu kazi yenye ujuzi pamoja na kuendelea kutilia mkazo nafasi muhimu ya kilimo katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

"Bajeti hii imeandaliwa kwa kuzingatia kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kuwezesha ujenzi na ukarabati wa miundombinu, kama ilivyo kwa nchi zingine wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, azma ya bajeti ya mwaka 2020/2021 ni kuchochea ukuaji wa uchumi ili kulinda na kuboresha maisha ya wananchi kupitia viwanda" alisema Dkt Philip Mpango.

Bajeti hiyo ya tano na ya mwisho katika utekelezaji wa mpango wa pili wa maendeleo ya Taifa wa miaka mitano 2016/2017- 2020/2021.

Alisema utekelezaji wa bajeti hiyo unahitajika katika maeneo ya vipaumbele vyenye kuchochea mageuzi ya uchumi na maendeleo ya watu ikiwepo ya ukarabati wa miundombinu iliyoharibiwa pamoja na kupambana na Homa kali ya Mapafu COVID-19.

Aidha Dkt Mpango alibainisha kuwa Serikali inaendeleza ujenzi wa miradi ya kichumi ambapo miradi inayotiliwa mkazo ni Pamoja na Ujenzi wa Viwanda vinavyotumim kwa wingi malighafi zinazopatikana nchini Tanzania zikiwepo za Kilimo, Madini na Gesi asili ili kukuza Mnyororo wa thamani.

Aliongeza kuwa miradi hiyo ni pamoja na ile ya kuchakata gesi asilia, uanzishwaji na uendelezwaji wa kanda maalum za kiuchumi na kongani za Viwanda vya kuongeza Thamani mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi.

Post a Comment

0 Comments