Uwekezaji ni suala muhimu katika kukuza uchumi wa Nchi
yoyote Duniani, Uwekezaji unafanyika ili kuongeza mapato ya nchi na wananchi
wake kutokana na uanzishwaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo
imekuwa ikiajiri kundi kubwa la watu hususan Vijana ambao ndio nguvu kazi ya
Taifa husika.
Na Grace Semfuko.
Mara nyingi uwekezaji katika sekta binafsi ndio unaopigiwa chapuo kwenye nchi
nyingi Duniani kwani Serikali za Mataifa hayo pekee haziwezi kutoa ajira kwa
kundi lote la Vijana walio katika umri wa kuajirika.
Tanzania imejidhatiti katika kusimamia uwekezaji ipasavyo
kwani tunaona kumekuwa na maboresho mbalimbali yanayofanyika hususan katika
Serikali ya awamu ya tano, maboresho hayo ni kama vile kuimarisha Sheria za
Uwekezaji ambazo zinamlinda Mwekezaji na wakati huo huo zinalipatia Taifa fedha
kutokana na Uwekezaji huo.
Maboresho
hayo ni pamoja na yale ya mazingira ya biashara na uwekezaji nchini, ikiwemo
kuanza kutekeleza Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (Blueprint) na
kuanzisha Wizara Maalum ya Uwekezaji iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu
ambapo marekebisho ya sheria mbalimbali yamefanywa na kupunguza urasimu katika
kutoa vibali na pia kufuta tozo kero 173 huku kati ya hizo, tozo 114 zinahusu sekta ya
kilimo, uvuvi na mifugo, tozo 54 za sekta nyingine mbalimbali, na tozo 5
zilikuwa zikitozwa na Wakala wa Usalama na Afya mahali pa Kazi (OSHA).
Juni 16 wakati
akifunga Bunge la 11 na la mwisho katika kipindi cha miaka mitano ya utawala wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli alisema mafanikio makubwa yamepatikana kwenye nyanja za biashara na
uwekezaji ambapo Biashara yetu ya nje imeongezeka kutoka Shilingi Trilioni 11.5
mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi trilioni 16.6 mwaka 2018/2019.
Alisema jambo la
kufurahisha zaidi ni kwamba, Tanzania imekuwa na urari chanya wa mauzo ya
bidhaa kwenye masoko ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na
nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).
Alitolea mfano kwa upande wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kutoka mwaka 2015 hadi mwaka 2018, Tanzania imekuwa na urari chanya wa mauzo ya bidhaa kwa wastani wa Dola za Marekani milioni 288.04.
Alizungumzia pia uwekezaji ambapo alisema Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesajili miradi mipya 1,307 yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 14.607 ikiwa ni zaidi ya shilingi trilioni 30 za kitanzania na miradi hiyo mingi ikikamilika itatoa ajira 183,503.
Alitolea mfano kwa upande wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kutoka mwaka 2015 hadi mwaka 2018, Tanzania imekuwa na urari chanya wa mauzo ya bidhaa kwa wastani wa Dola za Marekani milioni 288.04.
Alizungumzia pia uwekezaji ambapo alisema Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesajili miradi mipya 1,307 yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 14.607 ikiwa ni zaidi ya shilingi trilioni 30 za kitanzania na miradi hiyo mingi ikikamilika itatoa ajira 183,503.
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ni kituo chenye dhamana ya
kusimamia uwekezaji nchini Tanzania, kituo hiki kilianzishwa mwaka 1997 kwa
Sheria ya Uwekezaji Tanzania ili kiwe ni Taasisi kuu ya Serikali ya kuratibu,
kuhimiza, kukuza na kuwezesha uwekezaji nchini Tanzania na kuishauri kuhusu
sera ya uwekezaji na masuala yanayohusiana na uwekezaji.
Taasisi hii inashughulika na uwekezaji wote wenye mtaji
usiopungua USD 300,000 iwapo mmiliki ni mgeni au USD 100,000 iwapo mmiliki ni
mwananchi.
Aidha shughuli za uwekezaji zinazohusu uchimbaji wa madini na petroli zinafuata utaratibu ulioidhinishwa kwenye sheria husika.
Hata hivyo taasisi hii inasaidia wawekezaji wote kupata vibali, idhini nk. vinavyotakiwa kwa mujibu wa sheria nyingine ili kuanzisha na kuendesha uwekezaji nchini Tanzania.
Aidha shughuli za uwekezaji zinazohusu uchimbaji wa madini na petroli zinafuata utaratibu ulioidhinishwa kwenye sheria husika.
Hata hivyo taasisi hii inasaidia wawekezaji wote kupata vibali, idhini nk. vinavyotakiwa kwa mujibu wa sheria nyingine ili kuanzisha na kuendesha uwekezaji nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa Kituo hiki Bw. Geoffrey Mwambe Juni 2-6 ,
2020 alifanya ziara yake kwenye Kanda ya Kaskazini katika mikoa ya Arusha,
Kilimanjaro na Tanga, ziara hii ilikuwa na lengo la kukagua shughuli za
uwekezaji ikiwepo kuangalia mafanikio na changamoto za Wawekezaji na
kuzitafutia ufumbuzi.
Miradi iliyotembelewa katika ziara hiyo ni pamoja na ile ya
uzalishaji wa viwandani pamoja na sekta ya utalii ambapo alianzia katika Mkoa
wa Arusha kwenye Kiwanda cha Galaxy Tanzania Limited ambacho kipo eneo la Unga
Limited, kiwanda hiki kinazalisha Maziwa katika ngazi mbalimbali yakiwepo
Maziwa halisi na mtindi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw.Geoffrey Mwambe akionyeshwa moja ya bidhaa ya maziwa inayozalishwa katika Kiwanda cha Galaxy Company Tanzania Limited kilichopo katika eneo la Unga Limited Jijini Arusha.(Picha na Grace Semfuko)
Akiwa Kiwandani hapo Mwambe aliwataka Watanzania kunywa maziwa kwa wingi kwani takwimu zinaonesha unywaji wa maziwa kwa hapa nchini ni wa chini kiwango ambacho hakikubaliki kimataifa.
Akiwa Kiwandani hapo Mwambe aliwataka Watanzania kunywa maziwa kwa wingi kwani takwimu zinaonesha unywaji wa maziwa kwa hapa nchini ni wa chini kiwango ambacho hakikubaliki kimataifa.
Alibainisha kuwa takwimu za mpaka
kufikia mwaka 2017 inakadiriwa kuwa Tanzania ni nchi ya pili Barani Afrika
kuwa na mifugo mingi ikitanguliwa na nchi ya Ethiopia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe akiwa katika kikao cha pamoja na wamiliki wa kiwanda cha Galaxy Tanzania Limited kilichopo Unga Limited Jijini Arusha, Mwambe alitembelea kiwanda hicho hivi karibuni akiwa katika ziara yake ya kuangalia shughuli za uwekezaji katika Kanda ya Kaskazini (Picha na Grace Semfuko)
Alisema ingawa Tanzania inashika nafasi ya pili Barani Afrika kuwa na idadi hiyo kubwa ya mifugo, lakini ni ya 132 kwa nafasi ya unywaji wa maziwa kwa mtu mmoja kwani kiwango cha unywaji wa bidhaa hiyo ni lita 40.29 tu kwa mwaka ikiwa ni pungufu ya zaidi ya mara nne ya kiwango kilichopendekezwa na Shirika la Chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) cha lita 200 kwa mwaka.
Takwimu za mpaka kufikia Mei 2020 inaonyesha kuwa licha ya uzalishaji na usindikaji wa maziwa kuongezeka nchini, bado mwenendo wa unywaji wa maziwa kwa mwananchi mmoja mmoja siyo wa kuridhisha.
Meneja wa Kampuni hiyo Bw. Irfan Virjee alisema tangu kujiunga kwao na TIC wamepata manufaa makubwa katika uwekezaji wao kwa sababu wamekuwa wakipata vivutio mbalimbali vya kiuwekezaji ambavyo vimewawezesha kuendesha biashara hiyo kwa faida.
"Nawasihi wamiliki wengine wa maeneo ya uwekezaji, wajiunge na TIC kwani wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha wawekezaji tunaendelea, mfano sisi tumeagiza mashine mbalimbali kwa gharama nafuu kabisa kutokana na punguzo la kodi za mashine hizo kwa hapa Tanzania" alisema Virjee.

Alisema ingawa Tanzania inashika nafasi ya pili Barani Afrika kuwa na idadi hiyo kubwa ya mifugo, lakini ni ya 132 kwa nafasi ya unywaji wa maziwa kwa mtu mmoja kwani kiwango cha unywaji wa bidhaa hiyo ni lita 40.29 tu kwa mwaka ikiwa ni pungufu ya zaidi ya mara nne ya kiwango kilichopendekezwa na Shirika la Chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) cha lita 200 kwa mwaka.
Kidunia nchi inayoongozwa kwa unywaji
wa maziwa ni Finlad ikikadiriwa kuwa mtu mmoja anakunywa lita 409 kwa mwaka.
Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Mifugo na Uvuvi
za mwaka 2016-2017 uzalishaji wa maziwa ulikuwa lita Bilioni 2.1, idadi hiyo
iliongezeka na kufikia lita Bilioni 2.4 kwa mwaka 2017-2018.
Aidha katika kipindi cha Julai 2017- April 2018, usindikaji wa maziwa
uliongezeka na kufikia lita milioni 52.6, kutoka lita milioni 42.1 kipindi cha Julai
2016- April 2017.
Takwimu za mpaka kufikia Mei 2020 inaonyesha kuwa licha ya uzalishaji na usindikaji wa maziwa kuongezeka nchini, bado mwenendo wa unywaji wa maziwa kwa mwananchi mmoja mmoja siyo wa kuridhisha.
Kwa wastani mtu mmoja anakunywa lita 47
za maziwa kwa mwaka ikiwa ni pungufu mara nne ya kiwango kinachopendekezwa na
Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) kwa mtu mmoja kunywa
lita 200 kwa mwaka.
Hii ndiyo hali halisi kwa takwimu chache za hivi karibuni kutoka Wizara
ya Mifugo na Uvuvi.
Kiwanda cha Maziwa cha Galaxy kimesajili uwekezaji wake katika kituo cha uwekezaji Tanzania TIC na kinafanya kazi ya uzalishaji wa maziwa ili kukidhi mahitaji ya wanywaji katika kuongeza afya na kujipatia kipato kwa wakulima na wafugaji.
Kiwanda cha Maziwa cha Galaxy kimesajili uwekezaji wake katika kituo cha uwekezaji Tanzania TIC na kinafanya kazi ya uzalishaji wa maziwa ili kukidhi mahitaji ya wanywaji katika kuongeza afya na kujipatia kipato kwa wakulima na wafugaji.
Meneja wa Kampuni hiyo Bw. Irfan Virjee alisema tangu kujiunga kwao na TIC wamepata manufaa makubwa katika uwekezaji wao kwa sababu wamekuwa wakipata vivutio mbalimbali vya kiuwekezaji ambavyo vimewawezesha kuendesha biashara hiyo kwa faida.
"Nawasihi wamiliki wengine wa maeneo ya uwekezaji, wajiunge na TIC kwani wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha wawekezaji tunaendelea, mfano sisi tumeagiza mashine mbalimbali kwa gharama nafuu kabisa kutokana na punguzo la kodi za mashine hizo kwa hapa Tanzania" alisema Virjee.
Kiwanda hicho kinachotengeneza aina
mbalimbali za maziwa yakiwepo ya ya Mtindi, Yoghurt na maziwa fresh yanayokaa
muda mrefu bila kuwekwa kwenye jokofu kilipata cheti cha uwekezaji mwezi
January mwaka 2018 baada ya kukidhi vigezo na wamewekeza kwa mtaji wa Zaidi ya
dola Milioni 2.8.
Baada ya kumaliza ziara yake katika
kiwanda cha maziwa cha Galaxy alielekea katika kiwanda cha Harsho ambacho
kinatengeneza vifungashio na vyakula vya mifugo, kiwanda hiki pia kinatengeneza
mavazi maalum yanayovaliwa na watoa huduma za afya kwa ajili ya
kujikinga na maambukizi ya magonjwa mbalimbali, mavazi hayo yamekuwa maarufu kwa jamii ya kitanzania na Duniani kote kutokana na kuvaliwa hasa na watoa huduma za afya ya homa kali ya mapafu (COVID-19)
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw.Geoffrey Mwambe akiangalia moja ya vifungashio vinavyotengenezwa katika kiwanda cha kutengeneza bidhaa hizo cha Harsho kilichopo Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro,(Picha na Grace Semfuko)
Akiwa Kiwandani hapo Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji
Tanzania TIC Bw. Geoffrey Mwambe akaziomba taasisi zinazosimamia masuala ya uwekezaji
Nchini ziwe ni taasisi za ufanikishaji wa sekta hiyo badala ya kuwa wadhibiti,
watafutaji makosa na mahakimu wa wawekezaji ambao wanabainika kuwa na
changamoto katika uwekezaji wao.
Aliyasema hayo kufuatia Mwekezaji Kiwanda hicho Bw. Harold
Shoo kumwambia kuwa taasisi hizo zimekuwa na changamoto ya kuwafuata kwa makosa
ya mara kwa mara, alibainisha kuwa wamekuwa wakiwatembelea kiwandani hapo na
kuwakagua, na wakati mwingine wanabainishiwa makosa ambayo hawayajui kutokana
na kukosa miongozo.
Mwekezaji huyu alimwomba Mwambe azishauri taasisi hizo
ziwape elimu kwani wao bado ni wachanga katika sekta ya uwekezaji nchini na wanahitaji elimu zaidi ya mazingira
ya hayo hatua ambayo itawanyanyua katika kuendesha maeneo yao ya uwekezaji.
“Niziombe Taasisi zinazohusika na kusimamia maeneo ya
uwekezaji, ziwe ni taasisi za ufanikishaji na kutoa elimu kwa wawekezaji hawa,
makosa mengine yanahitaji kuwaelimisha tu hawa wawekezaji wetu, sio kila kosa
ni lazima utoe adhabu, tunawakatisha tamaa, wawekezaji ni wetu, wanaonufaika ni
vijana wetu walioajiriwa hapa na nchi pia inanufaika kutokana na kodi
wanazolipa, wakati mwingine tunaweza kuwaelimisha tu na mbona wanaelewa”
alisema Mwambe.
Aidha Mwekezaji huyo Bw. Harold Shoo aliishukuru Serikali
kutokana na kuweka mazingira mazuri ya kibiashara na uwekezaji hatua ambayo
inawahakikishia soko la uhakika pamoja na kurahisisha upatikanaji wa vibali
mbalimbali vinavyowawezesha wao kuzalisha kwa wingi bidhaa za viwandani.
Katika ziara hiyo pia alitembelea Hifadhi ya Taifa ya
Mkomazi iliyopo Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, hifadhi hii ilipata hadhi ya
kuwa hifadhi ya Taifa mwaka 2007 na ina vivutio vingi vya utalii na uwekezaji
katika sekta hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw.Geoffrey Mwambe akisoma mojawapo ya Jarida la Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kwenye hifadhi hiyo Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro, hifadhi hiyo inavyo vivutio vingi vya Utalii na hivyo wawekezaji wanakaribishwa kuwekeza hapo (Picha na Grace Semfuko)
Kutokana na kuwepo kwa fursa hiyo
Mwambe akasema ipo haja ya kuunganisha mikakati ya soko la utalii baina ya
hifadhi hiyo na upandaji wa mlima Kilimanjaro.
Kilichompeleka
Mwambe katika hifadhi hii ya Taifa ya Mkomazi ni kuangalia vivutio vya
uwekezaji katika sekta ya Utalii.
Anasema kuna idadi ndogo sana ya Watalii licha ya kuwa na
rasilimali za kuvutia na anashauri kuwepo haja ya kuunganisha
nguvu na kuwa na masoko ya pamoja.
Aidha
Mwambe aliwaomba viongozi wa Mikoa Nchini kuendelea kuibua fursa za uwekezaji
zilizopo kwenye maeneo yao.
Hatua
hii kwa mujinu wa Mwambe itakiwezesha kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kiweze
kutengeneza mpango maalum wa kuvutia uwekezaji.
Kwa
upande wake Kamishna Msaidizi wa Hifadhi ya Taifa ya
Mkomazi Abel Mtui, anasema hifadhi hiyo inavyo vivutio muhimu vikiwepo maeneo
ya ujenzi wa hotel na camps ambazo zitawezesha watalii kuangalia wanyama na
mandhari nzuri ya hifadhi hiyo yenye Mazingira na hewa safi na hivyo aliwakaribisha
wawekezaji kuwekeza katika hifadhi hiyo.
Kamishna Msaidizi wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Bw. Abel Mtui (mwenye kofia) akiwaonesha baadhi ya wanyama waliopo kwenye hifadhi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe (Katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Bi. Rosemary Senyamule (Picha na Grace Semfuko)
Hifadhi
ya Mkomazi ilipewa hadhi ya hifadhi ya Taifa Mwaka 2007
Ziara hii pia iliangazia maajabu ya
ziwa Chala lililopo Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro ambalo pamoja na mambo
mengine linahitaji uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya utalii.
Hapa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha
Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe aliwataka wawekezaji wa ndani na
nje ya nchi kutangaza fursa za uwekezaji katika Sekta ya utalii.

Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Bw.Geoffrey Mwambe akishangazwa na maajabu ya Ziwa Chala lililopo Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro.(Picha na Grace Semfuko)
Pengine umeshawahi kusikia jina Chala katika maisha yako labda kwa maana ya jina la mtu au kwa maana kidole kwa baadhi ya kabila ya kusini mwa Tanzania lakini leo Chala ni jina la ziwa la maajabu lililopo wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro mpakani mwa Tanzania na Kenya.
Pengine umeshawahi kusikia jina Chala katika maisha yako labda kwa maana ya jina la mtu au kwa maana kidole kwa baadhi ya kabila ya kusini mwa Tanzania lakini leo Chala ni jina la ziwa la maajabu lililopo wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro mpakani mwa Tanzania na Kenya.
Ziwa Chala lina fursa za Uwekezaji
katika Sekta ya Utalii kutokana na wageni wengi kuwasili katika eneo hilo
kujionea maajabu ya ziwa hilo.

Ziwa hili la Chala lipo kati
ya Tanzania na Kenya jirani na mpaka wa Holili. Chala ni la mtu, inasemekana
Mzee huyo na Familia yake alijitenga na jamii nyingine na kuweka
makazi katika moja ya vilima vinavyozunguka wilaya ya Rombo.
Mzee Chala inasemekana
takribani miaka laki mbili iliyopita alikaa hapo na wakati huo kulikuwa
na kilima kilichokuwa na volcano
Volcano hiyo inahisiwa ililipuka
dhoruba yenye kishindo kikubwa na matokeo yake kilima kilizama chini hivyo
kufanya kilima kugeuka shimo kubwa lenye kina cha takribani mita 300!
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw.Geoffrey Mwambe (Mwenye koti) na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Bi. Agness Hokororo (mwenye Kitenge) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Maafisa wa Wilaya hiyo wapotembelea kwenye Ziwa Chala ili kuangalia fursa za uwekezaji zilizopo kwenye ziwa hilo.(Picha na Grace Semfuko)
Mzee Chala na mji wake, Watoto,wake zake, mifugo na kila
kitu vyote inasemekana vilizama kwenye shimo(cretor) hilo ambalo baadaye mkondo
wa maji wa chini kwa chini kutoka mlima mkubwa (mrefu) Afrika yaani
Kilimanjaro yalibainika kujaza shimo hilo na kuwa ziwa!
Mkondo huo wa chini kwa kwa chini ulijaza cretor hilo
ambalo kwa sasa Ziwa Chala badala ya kilima Chala lenye takribani ukubwa wa
mita 500 urefu, upana mita 200 na kina yaani kwenda chini mita 300 (viwanja
vitatu vya mpira wa miguu!.
Ziwa hilo la ajabu ambalo halina mto unaoleta maji
kwa juu, huonekana kuwa na kina kirefu kwa maana ya ujazo wa maji wakati
wa kiangazi tu, wakati ambao ukianangalia theruji ya Mlima Kilimanjaro
huonekana kupungua kwa kuyeyuka kwa joto, lakini ziwa Chala huonekana kupungua
kina au kukauka wakati wa masika yaani kipindi cha baridi ambapo Mlima
Kilimanajaro hunekana kufunikwa na theruji, hivyo kuthibitisha ziwa Chala
kukosa maji ya kulijaza!
Licha ya mambo mengine ya ajabu kuonekana katika ziwa hilo
ambyo mengi ni hadithi za viumbe vya ajabu kwa imani za mashetani,chunusi na
mizimu kuonekana na vifo vya mara kwa mara kwa watafiti na watu wanoogelea,
pikiniki na shughuli za utalii katika ziwa hilo.
Kuna simulizi mbalimbali za kiimani zikihusisha ziwa hilo
ikiwepo ile ya kila mwezi wa kumi na mbili ya kila mwaka, nyakati za usiku
huonekana boti lenye taa ambayo huwa linaelea majini kutoka upande mmoja
kwenda kwingine, lakini Asubuhi huwa haionekani tena.
Simulizi nyingine ni Watafiti kutoka Ulaya walipandikiza
viumbe hai kwenye ziwa hilo wakiwemo samaki wa maji baridi na mamba ili waone
kama wanaweza kuishi humo na kuzaliana kwani awali hakukuwa na viumbe hai,
baada ya mwaka mmoja wazungu hao sita walirudi kuona matokeo na kwa bahati
mbaya mamba walikuwa wakubwa walipindua mtumbwi wao na watafitti wawili
kati yao wakageuzwa kitoweo wa mamba hao!
Wazungu walikasirika wakaenda kuleta nyama zenye sumu na
mamba wote walionekana kuelea wakiwa wamekufa! kwa sasa ziwa halina mamba tena
ila kuna samaki na kuna wakati wanaoneka nyoka wakubwa kama chatu na sawaka.
Wito unatolewa kwa wizara husika, kutumia njia zake kutangaza ziwa hilo kama
kivutio cha utalii.
Ziara hii inamalizikia Mkoani Tanga ambako Kampuni ya
Hengya ya Nchini China inayofanya shughuli zake za uwekezaji Mkoani Tanga
nchini Tanzania ilianza kufanya tathmini ya kuwalipa fidia wakazi 94 wa
eneo la Mtimbwani Wilayani Mkinga Mkoani Tanga ambao walitoa maeneo kwa ajili
ya kupisha shughuli za uwekezaji miaka minne iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine Shigella (mwenye koti) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Bw. Geoffrey Mwambe alipomtembelea kwenye ofisi zake akiwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Tanga kuangalia changamoto na fursa za uwekezaji Mkoani humo.(Picha na Grace Semfuko)
Baadhi ya Wakazi hao walilipwa fidia hizo lakini
hawakuridhishwa huku wengine tisa wakibainisha kutolipwa kabisa fidia hizo.
Hatua hiyo inamefikiwa baada ya ziara ya mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC Bw Geoffrey Mwambe kufanya ziara
mkoani humo ya kuangalia changamoto na mafanikio ya uwekezeji.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Bw.Geoffrey Mwambe akiwa pamoja na wawekezaji wa Kampuni ya Hengya Tanzania Limited inayomilikiwa na Raia wa China, Wawekezaji hao walikuwa wakimwonyesha Mwambe eneo la Mtimbwani lililopo Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga.(Picha na Grace Semfuko)

Kampuni hiyo ilitenga maeneo mawili ya kuwekeza likiwepo la
Amboni katika Manispaa ya Tanga na Mtimbwani lililopo Wilayani Mkinga ambapo
ucheleweshwaji wa ulipaji wa fidia hizo ulitokana na uchaguzi wa eneo gani
sahihi la kuwekeza kati ya hayo mawili.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella nae akazungumzia
mchakato wa mazungumzo baina ya Serikali, Wawekezaji na Wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Bw.Geoffrey Mwambe (wa kwanza kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella (Mwenye Miwani) wakikagua baadhi ya nyaraka za wakazi wa Kijiji cha Mtimbwani Wilayani Mkinga Mkoani Tanga ambao wanadai fidia kufuatia maeneo yao kuchukuliwa na Mwekezaji wa kampuni ya Hengya inayomilikiwa na Raia wa China.(Picha na Grace Semfuko)
Ziara hiyo ya Mwambe ilileta manufaa ambapo sasa Kampuni
hiyo itawekeza katika eneo la Amboni huku eneo la Mtimbwani likitafutiwa
shughuli za uwekezaji wa kilimo cha katani.
Kampuni ya Hengya Tanzania Limited ya China inatarajia
kuwekeza katika maeneo mawili likiwepo la kiwanda cha Cement kitakachokuwa na
uwezo wa kuzalisha Metrik tani milioni saba kwa mwaka huku Umeme ukitarajiwa
kuzalishwa megawatt 5,000 kwa mpango wa muda mfupi na megawatt 1,000 kwa muda
wa kati.
Mwisho.
0 Comments