Uwekezaji
katika sekta ya maziwa umekuwa na umuhimu mkubwa kutokana na bidhaa hiyo kuwa
na tija ya kiuchumi pamoja na kuongeza afya za wanywaji.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Bw. Geoffrey Mwambe alifanya ziara
katika Kiwanda cha Maziwa cha Galaxy kilichopo Unga Limited katika Manispaa ya
Arusha, na kubainisha kuwa takwimu za mpaka kufikia mwaka 2017 inakadiriwa kuwa Tanzania ni nchi ya pili
Barani Afrika kuwa na mifugo mingi ikitanguliwa na nchi ya Ethiopia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe (Mwenye koti jeusi) akiuliza maswali kuonyesha anahitaji kujua jambo kutoka kwa viongozi wa Kiwanda cha maziwa cha Galaxy kilichopo Unga Limited Jijini Arusha alipotembelea kiwanda hicho Juni 2,2020. (Picha na Grace Semfuko)
Alisema kwa mwaka huo wa 2017 ingawa Tanzania ilishika nafasi ya pili Afrika kuwa na idadi hiyo kubwa ya
mifugo, ilikuwa ni ya 132 kwa nafasi ya unywaji wa maziwa kwa mtu mmoja kwani kiwango kilikuwa ni kunywa lita 40.29 tu kwa mwaka.
Kidunia
nchi inayoongoza kwa unywaji wa maziwa ni Finlad ikikadiriwa kuwa mtu mmoja
anakunywa lita 409 kwa mwaka.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe akipata ufafanuzi kuhusu mashine hizo zinavyofanya kazi katika Kiwanda cha Maziwa cha Galaxy kilichopo Unga Limited Jijini Arusha (Picha na Grace Semfuko)
Kwa
mujibu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi za mwaka 2016-2017 uzalishaji wa maziwa
ulikuwa lita Bilioni 2.1 na udadi hiyo iliongezeka na kufikia lita Bilioni 2.4
kwa mwaka 2017-2018.
Aidha
katika kipindi cha Julai 2017- April 2018, usindikaji wa maziwa umeongezeka na
kufikia milioni 52.6 kutoka lita milioni 42.1 kipindi cha Julai 2016- April
2017.
Takwimu za
mpaka kufikia Mei 2020 inaonyesha kuwa licha ya
uzalishaji na usindikaji wa maziwa kuongezeka nchini bado mwenendo wa unywaji
wa maziwa kwa mwananchi mmoja mmoja siyo wa kuridhisha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe akipata ufafanuzi kuhusu mashine hizo zinavyofanya kazi katika Kiwanda cha Maziwa cha Galaxy kilichopo Unga Limited Jijini Arusha (Picha na Grace Semfuko)
Kwa wastani mtu mmoja anakunywa lita 47 za maziwa
kwa mwaka ikiwa ni pungufu mara nne ya kiwango kinachopendekezwa na Shirika la
Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) kwa mtu mmoja kunywa lita 200 kwa
mwaka.
Hii ndiyo hali halisi kwa takwimu chache za hivi
karibuni kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi
Kiwanda
cha Maziwa cha Galaxy kimesajili uwekezaji wake katika kituo cha uwekezaji
Tanzania TIC na kinafanya kazi ya uzalishaji wa maziwa ili kukidhi mahitaji ya
wanywaji katika kuongeza afya na kujipatia kipato kwa wakulima na wafugaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe akionyeshwa mojawapo ya bidhaa za Maziwa yanayotengenezwa katika Kiwanda cha Galaxy kilichopo Unga Limited Jijini Arusha (Picha na Grace Semfuko)
Nae
Meneja wa Kampuni hiyo Bw. Irfan Virjee amesema tangu kujiunga kwao na TIC
wamepata manufaa makubwa katika uwekezaji wao.
Kiwanda
hicho kinachotengeneza aina mbalimbali za maziwa yakiwepo ya ya Mtindi, Yoghurt
na maziwa fresh yanayokaa muda mrefu bila kuwekwa kwenye jokofu kilipata cheti cha uwekezaji mwezi January
mwaka 2018 baada ya kukidhi vigezo na wamewekeza kwa mtaji wa Zaidi ya dola
Milioni 2.8.
0 Comments