Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

TPSF; Bajeti ya 2020/2021 kuchochea Uwekezaji na Biashara Tanzania

Taasisi ya Sekta Binafsi TPSF imeridhishwa na Bajeti ya Mwaka 2020/21 iliyosomwa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na kueleza kuwa bajeti hiyo imejikita katika kupunguza gharama za uzalishaji, ufanikishaji na utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mfumo wa ufanyaji Biashara Nchini "Blue Print" pamoja na kulinda wazalishaji wa viwanda vya ndani.
Na Grace Semfuko, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa TPSF Angelina Ngalula alizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam na kubainisha kuwa bajeti hiyo imegusa maeneo mengi muhimu kwenye sekta mbalimbali za kiuchumi na kuinua Maisha ya wananchi wa Tanzania.

"Serikali imeanisha vipaumbele muhimu kwenye bajeti hii, tunaona imeainisha kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kwa kutoa asilimia 37 ya bajeti yake kitu ambacho kinachochea kwa kasi ukuaji wa sekta ya viwanda, uzalishaji wa ajira na kujenga uchumi imara wenye tija" alisema Ngalula.

Aliongeza kuwa ukuaji wa uchumi wa nchi unategemea uwepo wa taasisi binafsi ambazo ndio chachu ya ulipaji wa kodi za maendeleo pamoja na kupunguza umasikini kwa kundi kubwa la vijana ambao hupata ajira kwenye taasisi hizo.

Aliwataka Wawekezaji nchini kutumia mazingira hayo mazuri ya ufanyaji wa biashara kuwekeza Zaidi.

"Uwepo wa unafuu wa kodi na kufutwa kwa tozo mbalimbali kunafanya mazingira ya uwekezaji kuwa na ubora Zaidi, hivyo wawekezaji wazawa tumieni fursa hii iliyopo kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha ili kukuza mitaji yenu na kuongeza mzunguko wa biashara na ongezeko la ajira nchini" alisema.

Aidha alisema jatua ya Serikali ya kupendekeza kuondoa kuondolewa kwa tozo 60 za udhibiti, itarahisisha shughuli za ufanyaji wa biashara na uwekezaji nchini.

"Kulikuwa na kilio cha Wafanyabiashara na wawekezaji cha uwepo wa tozo nyingi ambazo zilikuwa kikwazo, kuondolewa kwa tozo hizo kutasaidia ongezeko la ufanyaji wa biashara na uwekezaji hali ambayo itainua uchumi wa Taifa kutokana na ukusanyaji wa kodi na kutengeneza ajira kwa vijana wa Tanzania" alisema.

Post a Comment

0 Comments