Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Juni 16, 2020 amefunga rasmi Bunge la 11 la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na kueleza kuwa katikia kipindi cha miaka mitano ya
uongozi wake, Sekta ya Uwekezaji imekuwa.
Na Grace Semfuko, Dar es Salaam.
Aidha amesema wastani wa
ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka shilingi Bilioni 850 mwaka 2014/15 hadi
kufikia shilingi Trilioni 1.3 mwaka 2018/2019.
Rais amesema mafanikio hayo ya
uwekezaji nchini yamekuja kufuatia kuwepo kwa mpango wa kuboresha mfumo wa
udhibiti wa biashara (Blue Print) ambapo sheria mbalimbali zimerekebishwa na kurahisisha ufanyaji wa biashara na uwekezaji nchini.
Amesema katika kipindi cha uongozi
wake jumla ya tozo na kodi mbalimbali 173 zimefutwa zikiwepo tozo 114
zinazohusu kilimo, mifugo na uvuvi na tozo nyingine mbalimbali.
“Wakati nazindua bunge hili
niliahidi kukuza uchumi, tumejitahidi kutekeleza ahadi hiyo kwa kukuza sekta
kuu za uchumi za uwekezaji, kuhusu sekta ya Viwanda ni viwanda vipya 8477
ambapo vikubwa ni 201 vya kati 460 vidogo 3,406 na vidogo sana ni 4460 hii
imengeza idadi ya viwanda nchini, viwanda hivi vimeifanya nchi yetu
kuzalisha ajira 482,601” alisema Rais Magufuli.
Aidha katika kuimarisha uwekezaji
wa viwanda Rais amesema katika kipindi chake hicho Serikali imefanikiwa
kupunguza tatizo la kukatika katika kwa umeme na katika kipindi hicho Tanzania
haikuwahi kuingia gizani.
“Kwa kuzima mitambo ya kuzalisha
umeme wa mafuta wa symbion, kwa kuzima mitambo ya IPTL, Aggreko na Symbion
tumeokoa Shilingi Bilioni 719 kwa mwaka na hii ndio imewezesha TANESCO sasa
ianze kujiendesha yenyewe” alisema Rais Magufuli.
Kuhusu sekta ya mawasiliano Rais
Magufuli alisema Serikali imeboresha usikivu wa simu kutoka asilimia 79 ya
mwaka 2015 hadi asilimia 94 mwaka 2019, pia idadi ya watumiaji wa simu na data
imeongezeka, hii imechangiwa na kupungua kwa gharama za kupiga simu kwa dakika
kutoka shilingi 267 kwa mwaka 2014/15 hadi shilingi 40 kwa sasa hivi alisema
Rais Magufuli.
Katika Sekta ya afya Rais
Magufuli alisema Serikali yake imefanikiwa kuongeza vituo cya kutolea huduma za
afya ambapo Hospitali za Wilaya zimeongezeka na kufikia 71 na hospitali 10 za
mikoa huku hospitali za rufaa za kanda zikiwa ni tatu ambapo watumishi ni zaidi
ya watumishi 1,000 wameajiriwa kupitia ongezeko la hospitaloi hiyo.
“Tumefanikiwa kusomesha madaktari
bingwa 301 ambao wameongeza huduma za wagonjwa wa moyo, figo na sikio, vifo vya
watoto wachanga chini ya siku 28 vimepungua kutoka vifo 8 kwa mwaka 2015 hadi
kufikia 7 kwa vizazi 1,000, na wagonjwa kutoka nje ya nchi sasa wameanza kuja
kutibiwa Tanzania hususan wagonjwa wa moyo” alisema Rais Magufuli.
0 Comments