Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

Tuwaelimishe Wawekezaji wanapojikwaa, tusiwe Mahakimu-Mwambe

Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC Bw. Geoffrey Mwambe amezishauri Taasisi zinazohusika na masuala ya uwekezaji Nchini zijikite katika kufanikisha, kuwezesha na kuelimisha Wawekezaji badala ya kuwa wadhibiti,watafutaji makosa na mahakimu wa wawekezaji ambao wanabainika kuwa na makossa katika uendeshaji kwenye maeneo yao ya Uwekezaji.

Anaandika Grace Semfuko-Arusha.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe (mwenye Koti) akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Kampuni ya Harsho Group ya Mkoani Kilimanjaro aliyekuwa akifafanua jinsi vifungashio vinavyotengenezwa katika kiwanda chake. (Picha na Grace Semfuko)


Aliyasema hayo katika ziara yake Kanda ya Kaskazini aliyoianza Juni 4 hadi 8, 2020 ambapo akiwa kwenye kiwanda cha kutengeneza vifungashio na vyakula vya mifugo cha Harsho Tanzania Limited kinachomilikiwa na Mtanzania Mzalendo Mwambe alisema ni muhimu Taasisi zote zinazohusika na Uwekezaji ziwe ni mwongozo kwa wawekezaji nchini.

"Naziomba sana Taasisi zinazohusika na Uwekezaji zikiwepo za masuala ya Afya, mazingira ya aina yoyote, thathmini ya sekta zote ziwe ni mshauri na mtoaji wa elimu kwa wawekezaji wetu, kama wamekosea tuwaelimishe, tusiwe chanzo cha kuwatafutia sababu na kuwapa adhabu, wakati mwingine ni wa kuwaelimisha tu hawa" alisema Mwambe.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe akikagua moja ya vifungashio vinavyotengenezwa katika Kiwanda cha Harsho Tanzania Limited kilichopo Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro, Mwambe alifanya ziara katika Kiwanda hicho Juni 5,2020 (Picha na Grace Semfuko)
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe akipata maelezo katika Kiwanda cha Harsho Tanzania Limited kilichopo Wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro(Picha na Grace Semfuko)  
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe akipata maelezo kuhusu mashine za Kiwanda cha Harsho Tanzania Limited kinavyofanya kazi (Na Grace Semfuko)
Mkurugenzi wa Kampuni ya Harsho Group inayomiliki Viwanda mbalimbali Mkoani Kilimanjaro Bw. Harold Shoo (Mwenye Fulana Nyeupa) akimwonesha Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe (aliyevaa Koti) vazi maalum la kujikinga  (Personal Protective Equipment PPE) wakati wa kutoa huduma za afya, Vazi hilo maalum ni miongoni mwa bidhaa zinazotengenezwa katika Kiwanda cha Harsho kilichopo Wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro ambapo Mwambe na Ujumbe wake kutoka TIC walitembelea Kiwanda hicho Juni 5,2020 (Picha na Grace Semfuko.)



Alisema kumekuwa na baadhi ya Taasisi ambazo zinafurahia kusikia Mwekezaji amefanya kosa fulani ili mradi tu alipe faini au adhabu, tunawarudisha nyuma, tutoe elimu kuhusu makosa wanayofanya, aliongeza.

Aliyasema hayo mara baada ya Mwekezaji wa Kiwanda hicho Bw. Harold Shoo kumweleza kuwa anakabiliwa na changamoto ya baadhi ya Watendaji wa Taasisi hizo kumfikia kiwandani na kumsumbua kwa mambo mbalimbali ambayo yalihitaji tu kusaidiwa kueleweshwa.

"Baadhi ya Taasisi zimekuwa ni kikwazo kwa uwekezaji huu, utakuta leo wanakuja taasisi hii wanakwambia mbona hujafanya hivi, kesho wanakuja wengine wanakwambia mengine na ksdhalika na kadhalika, mambo mengine hata hatuyajui, lakini wakituelewesha tunafanya tunahitaji tu kueleweshwa, sio kwamba tunajua kila kitu katika uwekezaji, Tunaomba ufukishe kilio chetu hiki kwa Taasisi hizi ili wakija waje kutuelewesha na sio kutupa adhabu" alisema Shoo Mkurugenzi wa Kiwanda cha Harsho kilichopo Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro.

Mwisho.




Post a Comment

0 Comments