Kituo cha
Uwekezaji Tanzania TIC na Serikali Mkoani Tanga wanashirikiana katika kushauri
Mamlaka mbalimbali za Serikali kusimamia na kuharakisha ujenzi wa Kiwanda
kikubwa cha Cement na Ujenzi wa Mradi wa kufua umeme wa makaa ya mawe katika
Jiji la Tanga.
Anaandika Grace Semfuko kutokea Mkoani Tanga June 6,2020.
Miradi hiyo itajengwa na Kampuni ya Hengya Tanzania Limited ya China ambapo kwa upande wa Cement pekee kinatarajiwa kujengwa kiwanda kitakachozalisha ujazo wa Metrik Tani milioni saba kwa mwaka huku Umeme ukitarajiwa kuzalishwa megawatt 5,000 kwa mpango wa muda mfupi na megawatt 1,000 kwa muda wa kati.
Hayo yalibainishwa
na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey
Mwambe alipofanya ziara Mkoani Tanga ya kukagua shughuli za uwekezaji na
kutatua changamoto katika sekta hiyo ambapo alikagua maeneo ya uwekezaji
yanayosimamiwa na Kampuni hiyo ya raia wa China kutoka katika Jimbo la Jiangsu.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akifuatilia jambo katika mjadala wa ujumbe wa maafisa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) walioongozana na Mkurugenzi wa Kituo hicho Bw. Geoffrey Mwambe (hawapo pichani) walipofika Mkoani hapo kuangalia mafanikio na changamoto za uwekezaji Picha na Grace Semfuko)
Pamoja na kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda cha cement na ufuaji wa umeme, pia kampuni hiyo inatarajia kujenga eneo la viwanda ambalo Kampuni nyingine ya Magari ya Jangsu Automobile Company (JAC) ya nchini China itaweka Kiwanda cha kuunganisha magari na kufanya uwekezaji kukua kwa kasi katika Jiji la Tanga.
“Kampuni ya
Hengya ni rafiki mkubwa wa kampuni ya Jangsu Automobile Company (JAC) ambao ni
watengenezaji wa magari ambao nao tuliongea nao walete kiwanda chao hapa
nchini, kwa hiyo Hengya pamoja na kuzalisha Cement na Umeme pia tumewaomba
wajenge Indusrial Park ambayo Jangsu watakuja na kuweka kiwanda cha kuunganisha
magari”
Aliongeza kuwa
“Mimi niliwatembelea na kufanya nao mazungumzo na kwa bahati nzuri Wenyeviti wa
Makampuni haya ya Hengya na JAC walifika Tanzania wakajionea fursa zilizopo,
walionana pia na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Dkt Bashiru Alli na kupata
fursa ya kuangalia fursa mbalimbali, tunataka Tanga iwe na uwekezaji huu”
alisema Mwambe.
Mkuu wa Mkoa wa
Tanga Martine Shigela alisema baada ya Kampuni ya Henya kuonesha nia ya
kuwekeza katika Mkoa wake, walifanya vikao mbalimbali kushirikiana na wananchi
ili kusaidia mchakato mzima wa uwekezaji ambapo kwa sasa wananchi wa Amboni
wenye zaidi ya ekari 280 na wale wa Mtimbwani wenye Zaidi ya ekari 1,000
wamelipwa fidia na wawekezaji hao.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine Shigella (Mwenye Miwani) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe wakikagua baadhi ya nyaraka za Wakazi wa Mtimbwani Wilayani Mkinga Mkoani Tanga ambao wanadai Fidia ya kupisha eneo la uwekezaji (Picha na Grace Semfuko)
Alisema hayo ni
maeneo makubwa ambayo wananchi wa maeneo hayo walistahili kulipwa ingawa bado
kuna changamoto chache cha ulipaji wa fidia huo ambao umetafutiwa ufumbuzi na
Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC pamoja na Ofisi yake ambapo kuanzia juni 10
wakazi waliobaki watafanyiwa tathmini na kuanza kulipwa fidia zao na wawekezaji
hao kutoka nchini China.
“Sisi Tanga
tunataka uwekezaji huu ukue ili wakazi wetu wanufaike kiuchumi, bahati nzuri
tumefanya mazungumzo na pande zote mbili wakiwepo wawekezaji na wananchi, na
sasa watalipwa fidia, tunakishukuru Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwani kimefanya
juhudi kubwa mpaka kufikia sasa” alisema Shigella.
Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Bw. Geoffrey Mwambe (katikati) akiteta jambo na Wawekezaji wa Kampuni ya Hengya ya nchini China wanaowekeza kiwanda cha Cement na Mradi wa kufua Umeme Mkoani Tanga Tanzania(Picha na Grace Semfuko)
Katika hatua nyingine Wawekezaji wa Kampuni hiyo wiki hii wataanza kuwalipa Fidia wakazi 94 wa Mtimbwani Wilayani Mkinga Mkoani Tanga
Mwisho.
0 Comments