Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

Mwambe akabidhi Ofisi kwa Dkt.Kazi, asema alipambana na Rushwa, asisitiza utafiti

Na Grace Semfuko,Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa Zamani wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Bw. Geoffrey Mwambe amekabidhi rasmi ofisi kwa Mkurugenzi wa sasa wa Kituo hicho Dkt. Maduhu Isaac Kazi.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli alimteua Dk. Kazi Julai 12, 2020 kuwa Mkurugenzi wa Kituo hicho akichukua nafasi ya Bw. Mwambe.
Mkurugenzi wa Zamanı wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe (kulis) akimkabidhi nyaraka Mkurugenzi wa sasa wa Kituo hicho Dkt. Maduhu Isaac Kazi (kushoto) katika hafla ya makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika kwenye ofisi ya Kituo hicho Jijini Dar Es Salaam.

Katika Makabidhiano hayo Mwambe alisema alipambana kuhakikisha wafanyakazi wa taasisi hiyo wanafanya kazi kwa weledi na kuepukana na vitendo vya rushwa.

“Nilipambana kuhakikisha hakuna rushwa kwa wafanyakazi wa taasisi hii, na tulifanikiwa sana, tumefanya kazi kwa uaminifu na nikuhakikishie Mkurugenzi wafanyakazi hawa ni waaminifu sana” alisema Mwambe.


Mkurugenzi wa Zamanı wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe akizungumza wakati akikabidhi ofisi kwa  Mkurugenzi wa sasa wa Kituo hicho Dkt. Maduhu Isaac Kazi (mwenye koti aliyeketi)  makabidhiano ya ofisi yalifanyika kwenye ofisi ya Kituo hicho Jijini Dar Es Salaam.

Alisema wawekezaji wanaipenda TIC na wanaikubali sana na hivyo kumwomba kuendeleza ufanisi katika kusimamia uwekezaji.

“Wawekezaji wanaipenda sana TIC, wana imani kubwa na taasisi hii, na hii inatokana na misingi iliyowekwa na Serikali kushirikiana nasi katika kuwasimamia, naomba tuendelee kuwasaidia” Mwambe alimwambia Mkurugenzi Mpya wa TIC Dkt. Maduhu Kazi.

Aidha alisema suala la utafiti kwenye uwekezaji kwa taasisi hiyo ni muhimu ili kujua takwimu za uwekezaji na mahitaji ya uwekezaji kwa ujumla.

“Tulijitahidi kufanya kazi za utafiti vizuri, lakini ipo haja ya tafiti zaidi ili kujua mahitaji halisi ya uwekezaji katika maeneo mbalimbali,changamoto kwa upande huu ni rasilimali watu, lakini hawa waliopo wanafanya kazi nzuri sana” alisema Mwambe.
Mkurugenzi wa sasa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Dkt. Maduhu Isaac Kazi akizungumza wakati wa makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika kwenye ofisi za Taasisi hiyo, Bw. Geoffrey Mwambe alimkabidhi Dkt Kazi Ofisi hiyo Jijini Dar Es Salaam.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa sasa wa TIC Dkt. Maduhu Isaac Kazi ampongeza Bw. Mwambe kwa kazi aliyoifanya alipokuwa TIC na kumwahidi kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa na kusimamia masuala yote ya uwekezaji ipasavyo.


 Mkurugenzi wa Zamanı wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe akizungumza na Wafanyakazi wa kituo hicho, Mwambe aliwaaga wafanyakazi hao na kuwataka kushirikiana vizuri na Mkurugenzi wa sasa wa Kituo hicho Dkt. Maduhu Isaac Kazi.


“Nimepata ushirikiano mkubwa sana tangu nilipowasili hapa TIC, rushwa ni mojawapo ya masuala ambayo niliahidi tangu mwanzo kuyashughulikia, na niliwaambia wafanyakazi nilipokuja kwa mara ya kwanza,nayashughulikia! nikuhakikishie uliyoyaacha nitayaendeleza” alisema Dkt Maduhu.

Post a Comment

0 Comments