Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

Manyanya atoa Pongezi kwa TIC kuvutia Uwekezaji.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Injinia Stellah Manyanya amesema ipo haja kwa Mamlaka za Serikali za Mikoa na Wilaya Nchini kutangaza Fursa za Uwekezaji
zilizopo kwenye maeneo yao ili kuwarahisishia Watu wenye nia ya kuwekeza nchini.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Injinia Stellah Manyanya akifafanua jambo alipotembelea banda la TIC kwenye viwanja vya nanenane Mkoani Morogoro.

Manyanya amesema kuna fursa nyingi za Uwekezaji lakini mamlaka hizo bado hazijafanya jitihada za dhati za kuzitangaza na kuzitaka kufanya hivyo ili kusaidiana na TIC katika kuvutia Uwekezaji.

"Serikali za Wilaya na Mikoa ni wakati wenu Sasa kutangaza fursa na vivutio mbalimbali vya Uwekezaji vilivyopo kwenye maeneo yenu, kuna baadhi mnafanya vizuri kutangaza vivutio hivi, kalini wengine bado, naomba tuwasaidie wenzetu wa TIC kutangaza Uwekezaji ndani ya Nchi yetu, wanafanya kazi kubwa sana, tunahitaji kuwaunga mkono.



Manyanya aliyasema hayo katika Banda la Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC alipotembelea kwenye wiki ya maonesho ya wakulima nanenane Kanda ya Mashariki Mkoani Morogoro.

Nae Afisa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC Kanda ya Mashariki Bi. Julie Muro amesema Kituo hicho kinafanya kazi kubwa ya kuvutia Uwekezaji nchini ambapo kwa sasa yamefanyika maboresho kadhaa ya kuimarisha huduma za mahala pamoja na upanuzi wa shughuli za TIC kikanda kutoka Kanda tatu za awali hadi kufikia Kanda saba ambazo zinatoa huduma kwenye mikoa yote nchini.




Post a Comment

0 Comments