Wawekezaji Wazawa chachu ya maendeleo
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Prof. Rutasitara Longinus ameendesha kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa Kituo leo tarehe 9/9/2020 ,Dar es Salaam.
Kikao hicho ni cha kwanza kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Dkt. Maduhu Kazi kukutana na Wakurugenzi wa Bodi hiyo kwa pamoja mara baada ya uteuzi wake tarehe 12/7/2020.
Bodi itaendelea kushirikiana na Menejimenti ya TIC katika kuvutia na kufanikisha masuala ya uwekezaji nchini hususan kuhamasisha na kuchochea wawekezaji wazawa kuanzisha na kusajili miradi ya uwekezaji TIC.
0 Comments