Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

TIC YATEMBELEA KAMPUNI YA VISTA PHARMA (T) LIMITED

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Dkt. Maduhu Kazi amefanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Pwani ambapo ametembelea na kukagua Mradi wa Uwekezaji wa kimkakati wa kiwanda cha madawa kinachomilikiwa na mzawa aitwaye Bw. Churchil Katwaza kupitia Kampuni ya Vista Pharma (T) Limited ili kujua maendeleo ya mradi huo pia kufahamu changamoto ambazo wanakutana nazo. Ziara hii ni mojawapo ya mikakati ya-kuimarisha na kuhamasisha Uwekezaji nchini kwa mwaka wa fedha 2021/2022. Ziara hiyo imefanyika Julai, 2021. Bw. Kakwaza amesema kwamba kwa sasa kiwanda hicho kipo katika hatua za mwisho za ujenzi ambapo hivi sasa zinafungwa mashine za uzalishaji. Ufunguzi wa kiwanda hicho unatarajiwa kufanyika hivi karibuni ambapo kiwanda kitakuwa kinazalisha dawa aina ya vidonge (tables) kwa kiwango cha milioni 700 kwa mwaka na dawa za maji (syrup) chupa milioni 32 kwa mwaka. Aidha, Dkt. Maduhu alieleza kwamba mradi huo ni muhimu sana kwa nchi kwa vile unalengo la kuwanufaisha wananchi kwa kutoa ajira kwa watanzania, kurahisisha upatikanaji wa dawa hapa nchini, kulipunguzia taifa matumizi ya fedha za kigeni, kuchangia pato la taifa kwa njia mbalimbali kuleta teknologia mpya katika utengenezaji wa dawa hapa nchini. Aidha, amempongeza Bw. Katwaza, kwa uamuazi wake wa kuwekeza hapa nchini kwenye mradi kama huu unaogusa watu wengi na kwamba utapunguza tatizo la dawa nchini. Pia alifafanua kuwa Serikali kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania kinapitia sheria na kanuni mbalimbali kwa lengo la kuboresha zaidi mazingira ya uwekezaji nchini hususan katika sekta ya madawa na vifaa tiba. Changamoto zilizojitokeza kama uhaba wa maji na upungufu wa Umeme, Dkt. Madhuhu aliahidi kufuatilia ili changamoto hizi zitatuliwe kwa wakati.

Post a Comment

0 Comments