Mkutano wa uwekezaji nchini Algeria (Algeria Investment Conference) umefunguliwa hapo jana tarehe 6/11/2021 mjini Algiers na waziri wa Biashara na Mauzo ya Nje, Mh. Kamel Rezig. Mbali na waziri huyu mkutano huu pia umehudhuriwa na mawaziri wengine sita wa Algeria na waziri mmoja kutoka nje ya nchi (Namibia). Jumla ya washiriki wapatao 3,000 wakiwa kama wawekezaji/wafanyabiashara wakubwa wamehudhuria mkutano huu wa kwanza kufanyika katika nchi ya Algeria. Kwa upande wa Tanzania washiriki waliohudhuria ni pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Algeria major Generali Jacob Gideon Kingu, Daudi Riganda aliyewakilisha TIC na Alhaji Jecha na Aziz Bakari waliowakilisha ZIPA. Aidha, mwekezaji mtanzania ambaye amewekeza katika viwanda vya Kahawa Bw. Amir Hamza pia ameshiriki ili kuangalia namna ambavyo anaweza kushirikiana na makampuni ya kigeni katika kufanikisha zaidi uwekezaji wake.
Katika mkutano huu mada na mawasilisho mbalimbali yamefanyika kuhusu fursa za uwekezaji. Mkutano huu utaendelea tena katika siku yake ya pili ya leo tarehe 7/11/2021. Na siku ya tarehe 8 /11/2021 TIC itakutana na wafanyabiashara wakubwa walioalikwa na ubalozi wetu nchini Algeria ili kujifunza zaidi fursa za uwekezaji zilizopo TANZANIA, vivutio na huduma mbalimbali zinazotolewa kupitia TIC.
TIC na ZIPA zimefanya pia mikutano ya ana kwa ana na baadhi ya wawekezaji walioonesha nia ya kuwekezaji hapa nchini.
Aidha kupitia mkutano huu wa uwekezaji Mheshimiwa Balozi wetu amehojiwa na vyombo mbalimbali vya habari nchi Algeria kuelezea masuala yanayoihusu Tanzania na fursa zetu za uwekezaji sambamba na wawakilishi wa TIC na ZIPA.
0 Comments