Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt. Maduhu I. Kazi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Bw. Shariff Ali Shariff wakizungumza na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Dkt. Mehment Gulluoglu pamoja na wafanyabiashara kutoka Uturuki.
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Dkt. Mehment Gulluoglu ametembelea Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) akiwa ameambatana na wafanyabiashara 6 kutoka nchini Uturuki kwa lengo la kuangalia fursa za biashara na uwekezaji kwenye sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, usindikaji wa mazao ya kilimo, ujenzi, nguo, madawa, virutubishi, kutoa huduma za afya pamoja na vifaa vya umeme.
Aidha wafanyabiashara hao walitumia fursa ya kukutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt. Maduhu I. Kazi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Bw. Shariff Ali Shariff na kueleza mikakati yao mbalimbali waliyojiwekea katika kuwekeza nchini.
Viongozi hao waliwapatia taarifa mbalimbali juu ya fursa za Uwekezaji na maelekezo, taratibu na sheria ya namna ya kuwekeza nchini.
0 Comments