Kampuni ya Elsewedy Industrial Development na Property International leo imesaini makubaliano ya makabidhiano ya ardhi ya eneo litakalotumika na Kampuni ya Elsewedy Industrial development kufanya utekelezaji wa ujenzi wa viwanda yaani Industrial Park huku serikali ikishuhudia utiaji saini makubaliano hayo.
Katika makabidhiano hayo Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema makabidhiano hayo ni hatua kubwa ya kuanza utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo ambao ni wa kimkakati na unaotegemea kuzalisha ajira zipatazo 50,000 katika eneo la ukubwa wa mita za mraba milioni 2.2.
Akiongea na waandishi wa habari Katibu Mkuu Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara amesema Fursa ya Ujenzi Viwanda 100 Kigamboni yafunguka kwani Mwekezaji amekamilisha taratibu za upatikanaji Ardhi na kuahidi kuwa Kazi ndio imeanza Mradi huo unaiweka Tanzania katika Ramani ya Vinara wa Uchumi Shindani Afrika.
Akiongea na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Dkt. Maduhu Kazi amesema juhudi kadhaa zimefanyika katika upatikaji wa ardhi hiyo na TIC itahakikisha hatua za haraka zinafanyika kurahisisha umilikishwaji wa Ardhi hiyo na utoaji wa hati ya upangaji kwa Mwekezaji yaani Derivative Rights ili aanze utekelezaji wa mradi huo wa kimkakati kwa nchi yetu.
#tunarahisishauwekezaji
#wekezatanzania
#kaziiendelee
0 Comments