Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimepokea wawekezaji kutoka kampuni ya HG Group wa nchini Misri waliofika kuangalia fursa za Uwekezaji zinazopatikana kwenye Sekta ya Kilimo haswa kwenye  uzalishaji wa vifaranga na ufugaji wa kuku wa nyama na mayai, kilimo cha mazao mchanganyiko, ufugaji wa ng'ombe wa maziwa na uchakataji wa bidhaa za maziwa.

Makam Mwenyekiti wa kampuni ya HG Group ndugu Mohamed Hegazy na Meneja wa Elsabeel ndugu Mohamed Ab Elatif Hegazy waliambatana na Balozi wa Tanzania nchini Misri Mhe. Emmanuel J. Nchimbi na kupokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Dkt. Maduhu I. Kazi katika ofisi za TIC makao makuu Jijini Dar es Salaam.

Wawekezaji hawa ni moja ya wazalishaji wakubwa wa mayai nchini Misri ambapo wanazalisha mayai milioni 250 kwa mwaka ambayo ni sawa na asilimia 37 ya mayai yanayozalishwa Misri.

Wawekezaji hao pia  wanazalisha mazao mbalimbali huko Misri ikiwa ni pamoja na machungwa, maembe ufugaji wa samaki na ndizi.

Pia wanaviwanda vikubwa vya kutengeneza yogati, samli na maziwa.
Vilevile wamefanya uwekezaji mkubwa kwenye kufanya tafiti mbalimbali ambapo wameweza kuwa na maabara mbalimbali zinazofanya tafiti kuhusu mazao kama ndizi na pia kuweza kuvumbua bridi yao ya kipekee ya kuku iitwayo HG Bro.


 

Post a Comment

0 Comments