Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

Fursa za Uwekezaji zilizopo Mkoa wa Kigoma


FURSA ZA UWEKEZAJI ZILIZOKO KATIKA MKOA WA KIGOMA

Na Grace Semfuko.

Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa Mikoa ya Tanzania Bara yenye fursa nyingi sana za uwekezaji.

Jiografia ya Mkoa wa Kigoma inaufanya kuwa Mkoa wa kimkakati katika kuvutia uwekezaji na maendeleo ya biashara za ndani na za kimataifa kutokana na kupakana na Nchi jirani za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zambia. 

Mkoa umezungukwa na Ziwa Tanganyika pia unaunganishwa na Mikoa ya Tabora, Shinyanga, Singida, Dodoma, Morogoro, Pwani na Dar es salaam kwa Reli ya Kati. 

Ziwa Tanganyika na Reli ya Kati ni fursa ya usafirishaji rahisi na nafuu wa bidhaa, malighafi na watu.

Aidha, jiografia ya mkoa pamoja na miundombinu iliyopo ni kuchochea cha maendeleo ya viwanda na biashara kutoka ndani na nje ya mkoa na nchi za Maziwa Makuu.

Mkoa unapata mvua za kutosha kuanzia 600mm hadi 1200mm kwa mwaka na unayo ardhi ya kutosha yenye rutuba inayofaa kwa kilimo ambapo hekta 776,21 sawa na 42.3% ya eneo linalofaa kwa kilimo hazijatumika., kiasi hicho cha ardhi yenye rutuba ni fursa kwa uwekezaji wa kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na biashara na vitalu vya mifugo ufugaji wa mifugo.

Uwepo wa mito ya asili na maporomoko ya maji, madini mbalimbali (Chuma, makaa ya mawe, chumvi, chokaa, shaba, dhahabu, almasi na chuma) ni fursa kwa uwekezaji katika tafiti na uchimbaji na uchakataji wa madini.

Mpango wa serikali wa kuufungua Mkoa wa Kigoma kwa kutekeleza miradi kama vile upanuzi wa uwanja wa ndege wa kigoma, uboreshaji wa reli ya kati kwa kiwango cha“standard gauge” upanuzi wa Bandari na ujenzi wa Barabara za Kidahwe-Nyakanazi na Uvinza-Tabora kwa kiwango cha lami utachochea zaidi uwekezaji katika Mkoa wa Kigoma.

Hivyo Mkoa unakaribisha Wawekezaji kuchangamkia fursa adimu za uwekezaji katika Mkoa wa Kigoma.

Baadhi ya fursa za uwekezaji zimeanishwa kisekta kama ifuatavyo;

Sekta ya Kilimo, MifugonaUvuvi

Kilimo


Kilimo cha michikichi kwa ajili ya mawese ni fursa ya kuanzisha kiwanda cha kuchakata matunda ya michikichi ambayo hutupatia mafuta ya mawese na bidhaa zingine kama vile sabuni. 

Michikichi ni mimea ambayo hutoa matunda na kisha hukamuliwa na kutoa mafuta ya mawese ambayo hupatikana kwa wingi Mkoani Kigoma, Mkoani humo michikichi hupandwa sana katika maeneo ya Bubango Kigoma mjini, Kakonko, Kamala, and Mahembe.Pia wilaya za Kibondo, Kasulu na Uvinza kuna zaidi ya hekta 200,000 za ardhi zinazofaa kwa zao la michikichi, kwa sasa uzalishaji ni wastani wa tani 30,010.

Matunda ya mchikichi kwa mwaka, wawekezaji wanakaribishwa kuwekeza kwenye kilimo cha kisasa cha michikichi na uchakataji wa matunda ya michikichi katika Mkoa wa Kigoma.

Zao la Michikichi

Kilimo cha zao la muhogo 
Ustawi wa zao la Muhogo ni fursa kwa kupanua kilimo cha zao la muhogo na uanzishaji wa kiwanda cha kuchakata mazao ya kilimo kama muhogo, zao la muhogo ni zao ambalo hutupatia bidhaa ya unga kwa ajili ya chakula, na unga wake hutumika sana maeneo mbalimbali ya Tanzania, maeneo yanayolima zao la muhogo kwa wingi ni Mahembe, Kazuramimba na Kidahwe, Kibondo, Kasulu, Buhigwe, Uvinza na Kakonko, sehemu hizo zina idadi kubwa ya wakulima wa zao hilo la muhogo na katika sehemu hizo miundo mbinu ya barabara, maji, huduma ya umeme zinaimarishwa.

Sehemu kubwa ya muhogo ghafi (Makopa) unaozalishwa inauzwa nchi jirani ya Burundi, kwa takwimu za mwaka 2015, eneo linalolimwa muhogo katika Mkoa kwa sasa ni hekta 126,933 na wastani wa uzalishaji kwa mwaka ni tani 545,922.



 Kilimo cha zao la Muhogo kinacholimwa Mkoani Kigoma.

Baadhi ya fursa za uwekezaji katika Mkoa wa Kigoma kwenye kilimo cha zao la pamba Ustawi wa kilimo cha Pamba ni fursa kwa kupanua kilimo cha pamba na uanzishaji wa kiwanda cha nguo.

Mkoa wa Kigoma katika Wilaya ya Kakonko na Kibondo vijiji ishirini vimetambulika kuwa na uzalishaji wa pamba kwa eneo zaidi ya hekta 230 kwa kakonko na hekta 14,000 kwa Wilaya ya Kibondo.

Kwa sasa wastani wa pamba inayozalishwa katika Mkoa ni tani 93 kwa mwaka na eneo linalotumika kwa kilimo cha pamba linakadiriliwa kuwa hekta 66.

Miundombinu ya barabara, maji, bandari na kiwanja cha Ndege katika Mkoa vinapatikana.

Zao la Pamba



Kilimo cha Matunda.
Mkoani kigoma Uwepo wa uzalishaji mkubwa wa matunda ya aina mbalimbali ni fursa kwa uanzishaji wa kiwanda cha kusindika matunda. Mkoa wa Kigoma katika maeneo yake ya Wilaya za Kasulu, Buhigwe, Kibondo kuna Zaidi ya hekta 1,350 zinazofaa kwa uzalishaji wa matunda.

Miongoni mwa matunda mbalimbali yanayozalishwa kwa wingi Mkoani Kigoma 

Kilimo cha zao la Kahawa
Ustawi wa zao la kahawa ni fursa kwa uanzishaji wa kiwanda cha kubangua na kusindika  kahawa.

Aidha, zao la kahawa katika Mkoa linalimwa sana katika maeneo ya mnanila na Manyovu wilayani Buhigwe,  na  Kalinzi Wilayani Kigoma ambapo zao hili linastawi kwa wingi.

Kakonko kuna hekta 89 zinazofaa kwa kilimo cha kahawa. Kwa sasa jumla ya tani 12,409  zinazalishwa kwa mwaka ambapo eneo linlotumika linakadiriwa kuwa hekta 13,956. Maeneo yanayofaa kwa kilimo cha kahawa mengi yako Wilaya za Buhigwe, Kigoma, Kasulu na Kibondo na Kakonko.

Baadhi ya fursa za uwekezaji katika Mkoa wa Kigoma, zao la Kahawa aina ya Arabica linalostawi kwa wingi Mkoani Kigoma.

Aidha Halmashauri ya Uvinza kwa kushirikiana na TACRI-TANZANIA COFFEE RESEARCH INSTITUTE (Taasisiya utafiti ya kahawa) ilifanya utafiti wa udongo ili kubaini kwa uhakika eneo linalofaa kwa kahawa. Utafiti ulionyesha  kuwa maeneo yanayofaa ni mengi hivyo bado kuna fursa kubwa ya kuwekeza katika zao hilo.

Kahawa pia zinalimwa Kigoma

Kilimo cha zao la Mpunga
Mkoa una Hekta 50,952 zinazofaa kwa kilimo cha Mpunga na mazao mbalimbali yanayofaa kilimo cha umwagiliaji. Kwa sasa ni Hekta 8,219.5 tu sawa na 16% ndizo zinazotumika. 

Hivyo 84% ya eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji ambalo halijatumika ni fursa kwa uwekezaji wa kilimo cha umwagiliaji na kilimo cha zao la mpunga.

Zao la Mpunga

Kilimo cha zao la Miwa Mkoani Kigoma
Kilimo cha zao la Miwa  Mkoa unayo Ardhi yenye ukubwa wa takribani hekta 200,000 zinazofaa kwa uwekezaji wa kilimo cha zao la miwa, Wilaya ya Kibondo imetenga hekta 471 kwa ajili ya uzalishaji na usindikaji wa zao la miwa. Wilaya ya Kasulu ina Zaidi ya hekta 100,000 zinazofaa kwa uwekezaji huo.

Mifugo.
Mkoa una Zaidi ya Hekta 200,000 za malisho ya mifugo na kati ya hizo, hekta80, 640 za malisho ya mifugo,  zipo Wilaya ya Kakonko. Aidha, hali ya hewa katika Mkoa inaruhusu ufugaji wa aina mbalimbali za mifugo.

Kwa takwimu za mwaka 2015 Mkoa wa Kigoma katika Wilaya zake za Kibondo, Uvinza na Kasulu ulikuwa baadhi ya fursa za uwekezaji katika Mkoa wa Kigoma, ng’ombe 586,686, mbuzi 595, 104 na kondoo 103, 346.

Hivyo uwepo wa malisho na idadi kubwa ya mifugo ni fursa kwa uanzishaji wa kiwanda cha nyama, ngozi na maziwa, aidha, Mkoa una zaidi ya hekta 1,000 zinazofaa kwa uwekezaji katika sekta ya mifugo ambapo Wilaya ya Kakonko ina hekta 806 zinazofaa kwa uwekezaji husika ambapo ujenzi wa machinjio ya kisasa (Abbatoir) na ujenzi wa kiwanda cha kusindika ngozi/ utengenezaji wa bidhaa za ngozi na usindikaji wa nyama na mazao mengine ya mifugo unaweza kufanyika.

Halmashauri ya Mji wa Kasulu ina hekta 12 kwa ajili ya ujenzi wa mnada wa kisasa wa mifugo na ujenzi wa kiwanda cha kusindika Ngozi na mazao mengine ya mifugo, 

Maeneo ya malisho ya mifugo na ng’ombe wa kiwamalishoni Wilayani Kasaulu
Uvuvi
Uwepo wa Ziwa Tanganyika na mito mbalimbali ni fursa kwa uanzishaji wa kiwanda cha kusindika mazao ya samaki. 

Mkoa wa Kigoma una eneo la kilomita za mraba 8,552 ambalo lina maji yanayofaa kwa shughuli za uvuvi. Pia ziwa Tanganyika lina aina mbalimbali za samaki kama vile migebuka, sangara, nonzi, ngegena dagaa wazuri ambao hupatikana ziwa hilo tu.

Ziwa hilo huzalisha wastani watani 45,000 mpaka 65,000 za samaki kwa mwaka. Kwa sasa “post-harvesting loss” ni 15% hivyo uwekezaji katika technolojia ya kuchakata mazao ya samaki ni mwafaka sana katika Mkoa. Aidha, ipo fursa pia ya kuwekeza katika ufugaji wa Samaki ambapo Wilaya ya Kigoma ina takribani hekta 25,000 zinazohusisha bonde la mto malagalasi na mto Lumpungu linalofaa kwa uwekezaji wa mabwawa ya ufugaji wa samaki.

Ziwa Tanganyika
Sekta ya Utalii na Maliasili Utalii Uwepo wa hifadhi ya milima ya Mahale na misitu ya Gombe yenye Sokwe adimu (Well researched Chimpanzee), hifadhi ya wanyama ya Muyowosi, njia ya biashara ya watumwa (Kigoma-Bagamoyo slave traderoute), Makumbusho ya Dkt. Livingstone na Stanley, Ziwa Tanganyika, Meli ya Mv. Lihemba, Hoteli za Kitalii (Lake Tanganyika Beach Hotel, Hill Top Hotel na Green View Hotel) ni fursa kwa uwekezaji wa Kitalii hasa katika Hoteli za Kitalii, Kampuni za kuongoza watalii, Kituo cha utalii, beach za kisasa na usafiri wa harakawamajini(Fastfarries)
Ziwa Tanganyika.

Misitu ya asili.
Uwepo wa Misitu ya asili ni fursa kwa uanzishaji wa viwanda vya kutengeneza samani za kisasa na bidhaa nyingine muhimu zitokanazo na mazao ya mistu. Aidha, Mkoa wa Kigoma una  misitu inayopatikana maeneo mbalimbali ya wilaya zake.

Mkoa una maeneo makubwa ya misitu iliyohifadhiwa na ile isiyohifadhiwa. Kuna jumla ya misitu 11 iliyohifadhiwa kisheria yenye hekta 836,736.8 (Kasulu – hekta 236,175.8; Kibondo–hekta 514,633.5; Kakonko hekta 658.08 na Uvinza – hekta 85,927.5). Misitu ambayo haijahifadhiwa inakadiriwa kufikia hekta 1,100,000.

Uwepo wa eneo lenye misitu (miti) aina ya Miombo ambayo ni Rafiki wa ustawi wa nyuki. Kuna fursa ya uanzishaji kiwanda cha kuchakata mazao ya nyuki. Mkoa wa Kigoma una eneo lenye ukubwa wa zaidi ya hekta 68,764.4 linalofaa ufugaji wa nyuki lililopo Wilaya za Kibondo, Uvinza na Kasulu.

Aidha, Mkoa wa  Kigoma ni miongoni mwa mikoa maarufu kwa ufugaji wa nyuki nchini Tanzania. Hali hii inatokana na uwepo wa aina nyingi za mimea na misitu ya asili ya miombo inayotoa aina nyingi za maua ambayo ni kivutio kikubwa kwa nyuki.

Kwa sasa Mkoa una mizinga ya kisasa 6,521 na ya asili 114,825. Kwa sasa uzalishaji wa asali ni wastani watani 472 na uzalishaji wa wastani wa tani 17 mwaka.

Mizinga ya kisasa katika Kijiji cha Basanza - Uvinza na Mzinga wa asili katika Kijiji cha Mwamila -Uvinza.

Madini
Kuna aina mbalimbali za Madini katika Mkoa, madini haya ni fursa kwa uanzishaji wa migodi na viwanda vya kuchakata madini. Mkoa wa Kigoma una hazina kubwa ya madini ya mchanga, chuma, dhahabu, shaba, makaa ya mawe, chokaa. 

Madini haya yanapatikana katika maeneo mbalimbali ya Wilaya za Kibondo, Kasulu, Uvinza kama vile bulonge Kisangani na nyantole. Wilaya ya Kibondo kuna madini ya chokaa katika Kijiji cha Kitahana, Red Garnet na Rhodolite katika Kijiji cha Kumshindwi na dhahabu katika Kijiji cha Kumhasha; Uwekezaji katika shughuli za utafiti, uchimbaji na usafishaji wa dhahabu, Chokaa, Red Garnet na Rhodo lite unakaribishwa Mkoani Kigoma.

Shaba Dhahabu Makaa ya mawe 
Sekta ya Elimu Mkoa pia unayo maeneo ya kutosha kwa ajili ya uanzishwaji  wa vyuo vikuu, vyuo vya Ualimu, Vyuo vya ufundi, uanzishwaji wa sekondari za kidato cha sita na hosteli za shule za sekondari katika Halmashaurizake.

Baadhi ya fursa za uwekezaji katika Mkoa wa Kigoma

Sekta ya Afya iko fursa ya kuwekeza katika miundo mbinu na utoaji wa huduma za afya katika Mkoa na Halmashauri zilizopokatika Mkoani ambapo Wilaya ya Kankonko ina vijiji 22 ambavyo havina zahanati za serikali na tayari ekari 44 zimetengwa kwa uwekezaji huo. Vile vile kuna Kata 10 ambazo hazina vituo vya afya ambapo ekari 30 zipo tayari kwa uwekezazihuo.

Sekta ya Viwanda na Biashara Shabaha ya Mkoa wa Kigoma ni kuvutia Wawekezaji kwa ajili ya maendeleo ya Viwanda na Biashara ili kuongeza kasi ya ukuzaji wa uchumi wa Mkoa wa Kigoma na kuchangia kukuza pato la Taifa ambapo kwa minajili ya kufanikisha shabaha hiyo, Mkoa umeshandaa eneo maalumu la Kiuchumi (KiSEZ) lenye ukubwa wa hekta 20,000 na kufanikiwa kupima na kuandaa Mpango Kabambe(Master Plan) wa eneo husika na michoro mbalimbali katika eneo lenye ukubwa wa hekta 691 na kupima viwanja 401 ambavyo vipo tayari kwa uwekezaji wa Viwanda, Elimu, biashara, kilimo, Michezo, Makazi n.k. kama inavyoonekana katika mchoro wa Mpango kabambe wa matumizi ya Ardhi hiyo. 

Pia Wilaya Uvinza ina viwanja 553 vilivyopimwa viko tayari kwa uwekezaji wa ujenzi wa nyumba za makazi na biashara, pia kuna hekta 22.44 kwa ajili ya eneo la viwanda vidogovidogo, vya kati na vikubwa. 

MPANGO KABAMBE WA KIGOMA SPECIAL ECONOMIC ZONE

Mkoa una wakaribisha Wawekezaji wa ndani na nje kuja kuwekeza katika Mkoa wa Kigoma katika sekta mbalimbali kama vile kilimo, usafiri wa majini, Elimu, Afya, Madini, Utalii, Uvuvi, Viwanda na Biashara.

Post a Comment

0 Comments