Na
Grace Semfuko Dar Es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia
Uwekezaji Angellah Kairuki, Waziri wa Mambo ya Bahari na Uwekezaji wa Indonesia
Bw. Luhut Binsar Panjaitan na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, na
wameshuhudia utiaji wa saini wa makubaliano ya ushirikiano baina ya Shirika la
Madini Tanzania STAMICO na Kampuni ya TP
Timah PTK inayomilikiwa na serikali ya Indonesia.
Utiaji saini huo umefanywa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Madini Tanzania STAMICO Dkt. Venance Mwasse na Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Biashara wa Kampuni PT. Timah TBK ya nchini Indonesia Bw.Trenggono
Sutioso yaliyofanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam mapema
Desemba 17, 2019.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia
Uwekezaji Angellah Kairuki, Waziri wa Mambo ya Bahari na Uwekezaji wa Indonesia
Bw. Luhut Binsar Panjaitan na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, na
wakishuhudia utiaji wa saini wa makubaliano ya ushirikiano baina ya Shirika la
Madini Tanzania STAMICO na Kampuni ya TP
Timah PTK inayomilikiwa na serikali ya Indonesia(Picha zote na Grace Semfuko)
Kampuni ya TP Timah PTK inamilikiwa na serikali ya
Indonesia kwa asilimia 65 na asilimia 35 zilizobaki zinamilikiwa na wananchi
kupitia mfuko wa hisa wa nchi hiyo.
Taasisi hizi mbili, zimeingia makubaliano
yatakayowezesha ushirikiano katika shughuli za utafiti wa madini, uwekezaji,
uchimbaji na uendelezaji wa sekta ya madini kwa ujumla.
Kwa Kuanzia kampuni zitashirikiana katika
kuendeleza leseni 15 zinazomilikiwa na Stamico zenye aina mbalimbali za madini
yakiwemo madini ya Bati (Tin), chuma, rare earth na phosphate.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia
Uwekezaji Tanzania Angellah Kairuki akimkabidhi zawadi ya picha ya kuchora Waziri wa Mambo ya Bahari na Uwekezaji wa Indonesia
Bw. Luhut Binsar Panjaitan mara baada ya nchi hizo mbili kusaini makubaliano ya ushirikiano baina ya Shirika la
Madini Tanzania STAMICO na Kampuni ya TP
Timah PTK inayomilikiwa na serikali ya Indonesia.
Kabla ya kutia saini makubaliano hayo Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Uwekezaji Angellah Kairuki alimwambia
Waziri Panjaitan wa Indonesia kuwa Tanzania inazo fursa nyingi za uwekezaji na
kuna haja ya kuwekeza kwenye fursa hizo.
Kairuki alizitaja baadhi ya fursa kuwa ni pamoja na
Sekta ya Viwanda, Utalii hususan kwenye mahoteli na camp kwenye hifadhi za
wanyama, uvuvi wa kina kirefu cha bahari na maziwa na kilimo hususan kwenye
uzalishaji wa miwa kwa ajili ya sukari ya majumbani na viwandani pamoja na uzalishaji wa mafuta ya
kupikia.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia
Uwekezaji Tanzania Angellah Kairuki na Balozi wa Tanzania Nchini Indonesia Ramadhan Dau wakifuatilia majadiliano katika kikao cha kusaini makubaliano ya ushirikiano baina ya Shirika la
Madini Tanzania STAMICO na Kampuni ya TP
Timah PTK inayomilikiwa na serikali ya Indonesia.
“Tanzania tunazo fursa nyingi kwenye uwekezaji,
tuna ardhi ya kutosha, hali nzuri ya hewa, Amani na utulivu wa kisiasa, kwa
upande wa bahari tunayo fursa ya uwekezaji kwenye uvuvi wa kina kirefu cha
bahari na maziwa, na pia kwenye kilimo tunazo fursa za uzalishaji wa sukati na
kilimo cha miwa pamoja na sekta ya mafuta ya kula” alisema Kairuki.
Kwa upande wake Naibu Waziri Nyongo alisema uamuzi
wa serikali ya Indonesia wa kuonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya madini
nchini ni wenye tija na manufaa kwa Taifa.
Waziri wa Mambo ya Bahari na Uwekezaji wa Indonesia
Bw. Luhut Binsar Panjaitan akifuatilia kwa makini mjadala katika kikao cha kusaini makubaliano ya ushirikiano baina ya Shirika la
Madini Tanzania STAMICO na Kampuni ya TP
Timah PTK inayomilikiwa na serikali ya Indonesia.
Nyongo alisema, Serikali ya Awamu ya Tano
imejipanga katika kuwasaidia na kuwalinda wawekezaji wa nje na ndani ya nchi na
hivyo amewahakikishia usalama wa mali waliyowekeza nchini.
“Tanzania ni
moja ya nchi zinazosifika kwa kuwa na mazingira salama na sera nzuri kwa uwekezaji”.
Alisisitiza.
Wajumbe wa kikao cha kusaini makubaliano ya ushirikiano baina ya Shirika la
Madini Tanzania STAMICO na Kampuni ya TP
Timah PTK inayomilikiwa na serikali ya Indonesia wakijadiliana jambo katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dar Es Salaam.
Aidha, Nyongo ameeleza kuwa sekta ya Madini nchini
ni moja ya sekta zinazokuwa kwa kazi huku ikisifika kwa kuwa na utajiri mkubwa
wa rasilimali madini yakiwemo madini ya metali, madini ya viwanda pamoja na
madini ya ujenzi.
Pamoja na uwepo wa madini hayo, Tanzania ni mahala
pekee yanapopatikana madini adhimu duniani, madini ya tanzanite. Pamoja na hayo
Tanzania nchi ya nne katika uzalishaji wa madini ya Dhahabu ikiongozwa na
Afrika Kusini, Ghana na Mali.
Baadhi ya Viongozi wakiwa katika kikao hicho cha kusaini makubaliano ya ushirikiano baina ya Shirika la
Madini Tanzania STAMICO na Kampuni ya TP
Timah PTK inayomilikiwa na serikali ya Indonesia.
Waziri wa Mambo ya Bahari na Uwekezaji wa Indonesia
Bw. Luhut Binsar Panjaitan akifuatilia kwa makini mjadala katika kikao cha kusaini makubaliano ya ushirikiano baina ya Shirika la
Madini Tanzania STAMICO na Kampuni ya TP
Timah PTK inayomilikiwa na serikali ya Indonesia.
Maafisa kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC wakifuatilia kwa makini mjadala katika kikao cha kusaini makubaliano ya ushirikiano baina ya Shirika la
Madini Tanzania STAMICO na Kampuni ya TP
Timah PTK inayomilikiwa na serikali ya Indonesia.
Wengine walioshuhudia uingiaji wa makubaliano hayo ni Balozi wa
Tanzania nchini Indonesia, Dkt Ramadhan Dau, Waziri wa Bahari na Uwekezaji
nchini Indonesia, Luhut Binsar Panjaitan, watendaji kutoka Stamico na Tume ya
Madini.
0 Comments