Na.Mwandishi
Maalum – Dar es Salaam
Jitihada za makusudi
za Serikali ya Awamu ya Tano katika kusimamia na kutekeleza sera madhubuti za
fedha na uchumi hasa katika kusimamia ukusanyaji wa mapato na matumizi,
kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, pamoja na usimamizi wa Benki, zimeelezwa
kuwa ni miongoni mwa vitu vilivyoifanya Tanzania kukua kiuchumi na
kunakoisaidia kue ndelea na ukuaji wa kasi katika siku zijazo.
Kwa mujibu wa ripoti
ndogo iliyotolewa Jijini Dar es Salaam na wataalam wa Shirika la Fedha
Ulimwenguni (IMF), waliomaliza muda wao wa kufanya utafiti hapa nchini kuanzia
tarehe 20 Februari hadi Machi 4 Mwaka huu, Tanzania ni miongoni mwa nchi chache
za Afrika zinazofanya vizuri katika ukuaji wa Uchumi.
Kiongozi wa timu hiyo
ya IMF iliyotembelea Tanzania Enrique Gelbard
amesema kiwango cha ukuaji wa uchumi katika kipindi cha miezi michache
iliyopita kinaonyesha ukuaji wa kasi kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na
serikali , kuongezeka kwa mauzo ya nje ya nchi, pamoja na kuongezeka kwa mikopo
kwa sekta binafsi.
Amesema viashiria hivyo
vitaifanya Tanzania kuendelea kukua kiuchumi katika siku zijazo katika sekta za
Ujenzi na madini, unaosaidiwa na kupungua kwa mfumuko wa bei kwa kiwango cha
asilimia 3.7 pamoja na kuimarika kwa viwango vya kubadilisha fedha za kigeni
,kadhalika na uwepo wa akiba ya kutosha ya fedha za kigeni inayoweza kufanya
manunuzi kwa kipindi cha takribani miezi mitano.
Aidha mtaalam huyo
amezungumzia kuimarika kwa uchumi hapa nchini kuwa kumesababishwa na sera
madhubuti za usimamizi wa fedha ambazo zimeleta mageuzi makubwa ya kiuchumi
hapa nchini, pia amezipongeza mamlaka husika kwa kuendelea kusimamia ukusanyaji
wa mapato.
0 Comments