Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

Maswa yatekeleza Tanzania ya Viwanda-Shemdoe

Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu imeendelea kutekeleza agizo la Rais Magufuli ailolitoa mapema mwaka 2015 alipoingia madarakani la kutaka Tanzania ya viwanda ili kukuza uchumi wa Taifa.


Wilaya hiyo tayari imejenga kadhaa vikubwa kikiwepo cha Viazilishe na kiwanda cha Chaki.


Profesa Riziki Silas Shemdoe-Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara


Hayo yalibainika katika ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Profesa Riziki Shemdoe baada ya kutembelea Kiwanda cha Viazilishe, Kiwanda cha kutengeneza Chaki pamoja na Kiwanda cha Vifungashio Wilayani humo.



“Viwanda hivi vitawanufaisha wananchi wa Wilayah ii kwa kutoa ajira na kuongeza thamani baadhi ya mazao yanayolimwa hapa, nawaombeni wananchi mzalishe kwa wingi viazi lishe kwa maana sasa soko lipo la uhakika” alisema Prof Shemdoe.



“Mmeonesha ni kwa kiasi gani mnazingatia, mmetimiza agizo la Rais wetu Mpendwa Dkt John Pombe Magufuli la Tanzania ya Viwanda, ujenzi wa viwanda hivi ni chachu ya kufikia maendeleo ya uchumi wa viwanda” alisema Profesa Shemdoe.



Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Dkt Fredric Sagamiko alisema ujenzi wa kiwanda cha viazi lishe pekee ambachi kina uwezo wa kukausha tani moja na nusu kwa siku umegharimu zaidi ya shilingi milioni 461.



Aliitaja changamoto ya uhaba wa vikaushio (Solar Dryier) pamoja na mtaji wa kuendeshea kiwanda hicho.

Post a Comment

0 Comments