Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

Kilimo cha Ufuta kuwainua Wakulima Ruvuma

Wakulima Mkoani Ruvuma wameanza kunufaika ambapo katika Mnada wa nane wa Mazao ya Ufuta na Soya ulioshirikisha Halmashauri tano za Mkoa wa Ruvuma na Vyama 11 vya Msingi vya Ushirika  umewawezesha Wakulima hao kuuza kilo zaidi ya 264,000 za ufuta na kuwaingizia zaidi ya sh. milioni 400.

Akizungumza katika mnada huo uliofanyika kwenye  soko la Mazao la Lilambo, Meneja wa Operesheni wa Chama cha Ushirika wa Mazao ya Kilimo Songea na Namtumbo (SONAMCU) Zamakanary Komba amesema wameboresha kanuni za manda huo na kwamba ni Halmashauri za Mbinga, Songea, Madaba na Nyasa ndizo zilizoshiriki katika mnada huo.

Vyama 11 vilivyoshiriki katika mnada huo ni pamoja na Kingambi, Tingi, Kilumba, Mpiki, Lina, Mugiso Nalisi, Songea West, Amkeni, Muungano na Tana ambapo kilo za ufuta zilizouzwa kwa bei ya juu iliyokubalika na Wakulima ilikuwa ni sh.1,930 na baada ya kutoa tozo mkulima anauza sh. 1759.

"Pesa ambayo wakulima ameipata katika manda huu ni zaidi ya sh.milioni 465 lakini kabla ya makato kwenda kwa Wakulima, fedha zilikuwa ni zaidi ya milioni 510" alisema Komba.

Komba alisema kupitia Mnada huo, tozo ya mfuko wa maendeleo katika Halmashauri zimepatikana shilingi milioni 7.9 na kwamba ushuru wa Halmashauri ni zaidi ya sh. milioni 20.6.

Hata hivyo katika mnada wa zao la Soya ambao ulishirikisha Halmashauri mbili, Wakulima hawakuridhishwa na bei ya Sao hilo ambayo ilikuwa ni sh 680 kwa kilo ambapo ikitolewa topo, Mkulima anabakiwa na sh 558.

Wakulima wa zoo la ufuta katika Wilaya za Namtumbo, Songea na Tunduru Mkoani Ruvuma wameanza kunufaika na Zao hilo baada ya kupokea sh. bilioni 16.8 tangu kuanza kuuza zoo hilo kwa mfumo wa stakabadhi ghalani April 30, mwaka huu.





Post a Comment

0 Comments