Debora ni jina la binaadamu kama wengi tulivyozoea, Debora ni jina lilalowakilisha Binaadamu wa jinsia ya kike,lakini kitu cha kufurahisha katika hifadhi ya Taifa ya Mkomazi iliyopo Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro kuna Faru anaitwa Debora, Faru huyu ni wa jinsia ya kike na ana mtoto pia.
Faru huyu aanaonekana sana katika hifadhi hiyo. lakini Zaidi alionekana katika Ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe aliyetembelea hifahi hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya uwekezaji sambamba na kuibua fursa za uwekezaji zilizopo katika Kanda ya Kaskazini ambapo kwa Upande wa Hifadhi hiyo ya Mkomazi kumeibuka fursa nyingi katika Sekta ya Utalii.
Faru huyu aanaonekana sana katika hifadhi hiyo. lakini Zaidi alionekana katika Ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe aliyetembelea hifahi hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya uwekezaji sambamba na kuibua fursa za uwekezaji zilizopo katika Kanda ya Kaskazini ambapo kwa Upande wa Hifadhi hiyo ya Mkomazi kumeibuka fursa nyingi katika Sekta ya Utalii.
ninaposema ni faru wa maajabu ni pale anapokuwa katika harakati zake za kujitafutia chakula yeye na mtoto wake anakuwa busy kwa shughuli hiyo tu na unapomwita ikiwa hujashika kitu cha kumpa anakuangalia tu, wala hakusogeleo, lakini unapokuwa na kitu cha kumpa amakuja taratibu kwa maringo kabisa.
Faru huyu anatambua kuwa binaadamu ni Rafiki zake maana anakuja bila wasiwasi na anakusogelea, anapenda sana kula Karrot, na Watalii huweza kumpata na kupiga nae picha kutokana na kumpatia kile apendacho.
Faru huyu anawatambua binaadamu na akiitwa kwa jina lake la Debora anajua unamuhitaji na anakufuata mahali ulipo.
Kivutio hiki cha Utalii kinapatikana ndani ya hifadhi ya Taifa ya Mkomazi pekee ambapo kuna mpango wa kuongeza faru weusi waliokuwa hatarini kutoweka.
Faru Debora, Faru huyu ukimwita kwa jina lake la Debora anasikia na anakuja mahali ulipo, anakula Carrot pia
Kwa zaidi
miaka 20 hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ilikuwa na mradi wa uzalishaji faru lengo
likiwa Ni kuongeza idadi ya mnyama huyo ambaye alikuwa ametoweka katika maeneo
mengi.
kutoweka
kwa mnyama huo kunatokana na kushamiri wa vitendo vya ujangili mwanzoni mwa
miaka ya 80 ambapo waliobakia walihamishiwa Nchini Afrika Kusini na Jamhuri ya
Czech na baadae walianza kurudishwa na kuhifadhiwa katika mradi huo wa kukuza
Faru nchini.
Kamishina
msaidizi wa hifadhi hiyo, Abel Peter amesema matarajio ni kuwa na wageni
takribani 7,680 kwa mwaka.
Hifadhi
ya Mkomazi imezungushia uzio wa umeme katika eneo la kilomita za mraba 13,000
ambalo linatumikakwa utalii na mradi wa kukuza Faru weusi waliokuwa mbioni
kutoweka.
Utalii wa
Faru weusi ni wa kwanza hapa nchini kuwepo katika hifadhi ya Taifa ya Mkomazi
na ni wa Pili Duniani, Watalii sasa wanaweza kujionea kwa karibu Wanyamapori
hao waliokuwa hatarini kutoweka
0 Comments