Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

Mkurugenzi Mpya wa TIC aripoti kazini, asema atahamasisha Ubunifu, Nidhamu na Kujituma, ni Dkt Kazi

Na Grace Semfuko, Dar Es Salaam.
Mkurugenzi Mpya wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC Dkt Maduhu Issac Kazi amesema ubunifu, nidhamu na kujituma ndio njia pekee ambayo itakifanya kituo hicho kuleta ufanisi katika kazi masuala ambayo amepanga kuyasimamia.


Mkurugenzi Mpya wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Dkt. Maduhu Isaac Kazi akisisitiza jambo kwa Wafanyakazi wa Kituo hicho mara baada ya kuripoti kituoni hapo Julai 13,2020 kufuatia uteuzi wake uliofanyika Julai 12, 2020 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Bombe Magufuli. (Picha na Grace Semfuko)

Dkt Kazi aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na Viongozi na Wafanyakazi wa TIC Julai 13, 2020, aliporipoti rasmi kwenye kituo chake kipya cha kazi alichopangiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Julai 12 mwaka huu.

“Kwa uwezo wangu nitakuwa nahamasisha zana ubunifu, kujituma na nidhamu, Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC imekuwepo muda mrefu, kina tamaduni zake na tuziishi tamaduni hizo, yaani kwamba ukiongea na mtu au watu lazima waseme huyu anatoka TIC” alisema Dkt Kazi.
 Mkurugenzi Mpya wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Dkt. Maduhu Isaac Kazi akisikiliza jambo kwa baadhi ya Wafanyakazi wa Kituo hicho Julai 13, 2020, Dkt Kazi alikuwa akizungumza na Wafanyakazi wa TIC mara baada ya kuripoti kufuatia kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Bombe Magufuli Julai 12,2020. (Picha na Grace Semfuko)

Alisema kutokana na Tanzania kuingia kwenye nchi ya uchumi wa kipato cha kati, wafanyakazi wa kituo hicho hawana budi kuendana na kasi ya hatua hiyo kwa kufanya kazi kwa bidi na nidhamu, ili kufanikisha adhma ya Serikali ya utendaji kazi wenye viwango.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji  mpya wa Kituo hicho Dkt. Maduhu Issac Kazi Julai 13, 2020 (Picha na Grace Semfuko)

“Nchi yetu imeingia katika uchumi wa kipato cha kati, ni hatua kubwa sana, sote tunafahamu kuwa tumefikia hatua hiyo miaka mitano kabla ya wakati tuliojiwekea, kwa hiyo tuchape kazi na utendaji wetu lazima ubadilike uendane na uchumi huo, ili hata aina ya wawekezaji tulionao wajiweke tofauti na wale tuliowazoea wakati tukiwa kwenye kipato cha chini, tunatakiwa tujiongeze ili tuendane na hatua ya uchumi huo”alisema. 

Baadhi ya Wafanyakazi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji  mpya wa Kituo hicho Dkt. Maduhu Issac Kazi Julai 13, 2020 (Picha na Grace Semfuko)

Alisema ni ushirikiano tu ndio utawezesha kufikia mafanikio ya utendaji kazi wa Kituo hicho na kuzitaka taasisi zinazoshirikiana na TIC kufanikisha uwekezaji, kuboresha na kuimarisha mifumo ya utendaji kazi wao.
 Baadhi ya Viongozi (Menejiment) wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wakiwa katika Picha ya Pamoja mara baada ya kumpokea Mkurugenzi Mpya wa Kituo hicho Dkt. Maduhu Issac Kazi alipowasili kituoni hapo Julai 13, 2020 kuanza kazi mara baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Julai 12,2020 (Picha na Grace Semfuko)

Mkurugenzi Mpya wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Dkt. Maduhu Isaac Kazi akisalimiana na baadhi ya Viongozi (Management) wa Kituo hicho mara baada ya kuwasili kituoni hapo kwa jailli ya kuanza kazi rasmi (Picha na Grace Semfuko)

“Kikubwa ni kwamba tuchape kazi, tushirikiane na kama kuna changamoto zozote tuendelee kuwasiliana, hiki chombo ni mtambuka, yaani  ni kwamba humo ndani kuna taasisi mbalimbali ambazo zinashirikiana,mfano TRA, BRELA, OSHA na nyinginezo,naomba tuwe kitu kimoja kwa lengo la kuisaidia TIC na wakati huo huo, mtimize  wajibu wenu kwenye taasisi zenu mlizotoka” alisema Dkt Kazi.

 Mwisho.





Post a Comment

0 Comments