Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts



Watumishi TIC watembelea Hospitali ya Ocean Road 

Watumishi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wametembelea wwgonjwa wa saratani katika hospitali ya Ocean Road na kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo kama sehemu ya kujitoa kwa jamii.


Akizungumza wakati walipotembelea hospitalini hapo, Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Wawekezaji Bi. Anna Lyimo akimuwakilisha Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) alisema TIC ilikuwa ikiadhimisha wiki ya utumishi wa umma na imehitimisha kwa kutembelea wagonjwa wa saratani.


“Tangu tarehe 16 Juni, 2022 tumepokea wananchi pamoja na wadau wa uwekezaji zaidi ya 70 kwenye ofisi zetu na kuwapa elimu juu ya fursa za uwekezaji na hitimisho lake ilikuwa ni jana na leo tukaona tushiriki kutoa msaada kwa  wagonjwa waliopo mahali hapa” alisema.


Aidha vifaa tulivyoleta leo ni pamoja na miswaki, dawa za meno, mafuta ya kupaka, sabuni, khanga, madera pamoja na maji ya kunywa na huu utakuwa ni utaratibu wetu kushirikiana nanyi kwakuwa tunafahamu uhitaji huo upo.


Chausiku Chapuchapu ni matroni wa wagonjwa wa saratani Ocean Road alieleza kuwa wapo wagonjwa waliolazwa ambao ndugu zao wako mbali hivyo wanakuwa na uhitaji mkubwa.


“Wagonjwa wetu wanashukuru kwa misaada wanayopokea kutoka kwa taasisi na watu mbalimbali kwakuwa waliowengi ndugu zao wako mikoani na hivyo misaada hii inawasaidia sana wawapo hapa”, alisema Chapuchapu


Watumishi wa TIC nao wamesema, wamepata faraja kusaidia wagonjwa wa saratani na wameahidi kurudi wakati mwingine. 





 

Post a Comment

0 Comments